emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Jisajili, Tukutambue, Tukutambulishe
Marekebisho ya Taarifa

Mwongozo wa Marekebisho ya Taarifa za Usajili na Utambuzi wa Watu umeainisha sifa stahiki, aina ya taarifa zinazoruhusiwa kurekebishwa na vigezo hitajika kuwasilishwa na mwombaji kwenye ofisi ya Usajili wilayani ili ombi liwe na sifa ya kuanza kufanyiwa kazi:-

Sifa Stahiki kwa Mwombaji Mwenye Hitaji la Kuboresha Taarifa za Usajili: -

(i) Mwombaji aliyeolewa na kubadilisha jina kwa kutumia taarifa za ukoo wa mume/mwenza wake,

(ii) Mwombaji aliyeolewa na kuachika kisheria anaweza kuruhusiwa kubadilisha taarifa zake na kurudia kujiandikisha kwa majina yake ya awali ya kabla hajaolewa kulingana na vyeti/nyaraka zake

(iii) Mwombaji aliyekosea kuandika baadhi ya taarifa zake yeye mwenyewe ambazo aliziandikisha wakati wa zoezi la Usajili na Utambuzi.

(iv) Mwombaji ambaye taarifa zake hazikuingizwa kwa usahihi kwenye mfumo wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na Watendaji wake wakati wa utekelezaji wa majukumu husika (Operational issues),

(v) Mwombaji ambaye aliandikisha taarifa/majina yake yoyote kwenye kipengele cha majina mengine/maarufu na baadaye akahitaji majina yake hayo yaandikwe kwenye kipengele cha majina ya kwanza basi ataweza kurekebishiwa bila kuathiri utambulisho wake wa awali au taarifa zilizohifadhiwa katika mfumo.

(vi) Jina la ukoo iwapo mwombaji ataamua kutumia jina ambalo tayari lipo kwenye upande wa majina ya wazazi wake mfano jina la Babu ambalo hapo awali hakulitumia.

Afisa Usajili wa Wilaya (DRO) anaweza akaridhia kubadilisha taarifa ambazo ziko kwenye fomu ya maombi ya Mwombaji ambazo ziliandikishwa hapo awali mfano katika sehemu ya majina mengineyo na iwapo mabadiliko hayo hayana nia ovu au yenye lengo la kuficha Utambulisho wake wa awali.

Taarifa za Maombi ya Utambulisho wa Watu zinazoruhusiwa kubadilishwa

Mwongozo wa marekebisho ya Taarifa za Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa unaelekeza juu ya taarifa zinazoruhusiwa kubadilishwa iwapo m waombaji kakidhi vigezo vya msingi vinavyo hitajika ni pamoja na; -

(i) Jina la kwanza, la kati, au la Mwisho (Ukoo) baada ya kukidhi vigezo na kuwasilisha uthibitisho unaotakiwa,

(ii) Tarehe na mwezi wa kuzaliwa,

(iii) Makazi ya mwombaji,

(iv) Namba ya simu baada ya Afisa Usajili kujiridhisha ya kwamba Namba ya Simu imesajiliwa kwa kutumia NIN ya Mwombaji.

(v) Uraia kwa yule aliyebadilisha uraia kwa nyaraka zinazokubalika kwa kufuata mwongozo wa Uhuishaji wa Taarifa za Uraia

(vi) Taarifa ya ndoa,

(vii) Taarifa ya kazi pamoja na

(viii) Kumbukumbu binafsi (taarifa hizi zinapatikana kwenye kipengele F cha fomu ya Usajili na Utambuzi wa Watu Na. 47- 58.)

Taarifa za Mwombaji zisizoruhusiwa kubadilishwa isipokuwa kwa kibali maalumu baada ya kufanyiwa kazi na Kamati ya Usajili na Utambuzi na kupata idhini ya Mkurugenzi Mkuu

(i) Taarifa za Wazazi

(ii) Makazi ya Kudumu

(iii) Mahali pa kuzaliwa

(iv) Majina mawili/ matatu

(v) Mwaka wa kuzaliwa na

(vi) Saini ya mwombaji

Taratibu mbalimbali za kufanya marekebisho ya taarifa kutokana na aina ya taarifa au usajili

Mabadiliko ya Majina

Mwombaji yoyote anayehitaji kufanya mabadiliko ya majina anahitajika kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

Soma Zaidi

Mabadiliko ya Tarehe ya Kuzaliwa

Mwombaji anayehitaji kufanya mabadiliko ya tarehe ya kuzaliwa anahitajika kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

Soma Zaidi

Mabadiliko ya Taarifa za Makazi

Mwombaji yoyote anayehitaji kufanya mabadiliko ya taarifa za makazi anahitajika kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

Soma Zaidi

Kundi la watumishi wa umma/watumishi wa umma waliostaafu

Mwombaji ambaye ni mtumishi wa umma anayehitaji kufanya mabadiliko ya taarifa anahitajika kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

Soma Zaidi

Mabadiliko ya Taarifa kwa waombaji waliofanya udanganyifu wa taarifa

Mwombaji yoyote ambaye alifanya udanganyifu wa taarifa na anahitaji kufanya mabadiliko..

Soma Zaidi

Mabadiliko ya taarifa kwa wageni wakazi/wakimbizi

Mgeni mkazi au mkimbizi anayehitaji kufanya mabadiliko ya taarifa anahitajika kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

Soma Zaidi