emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Jisajili, Tukutambue, Tukutambulishe
Ushirikishanaji Taarifa

Moja ya jukumu la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imekasimishwa ni pamoja na Kujenga Mfumo Mkuu wa Taifa wa Utambuzi wa Watu wa Kielektroniki kwa kukusanya taarifa sahihi za watu wanaoishi nchini raia, wageni wakaazi na wakimbizi kwa kushirikiana na Wadau katika utendaji kama vile Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGA), Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) na Jeshi la Uhamiaji..

Ziko njia tatu (3) zinazotumika kushirikisha taarifa kwa wadau:-

  Lango Kuu la Kushirikisha Taarifa (Common Interface Gateway) Njia hii humuwezesha mdau kuunganisha mfumo wake wa kutolea huduma na mfumo wa kushirikishana taarifa wa NIDA ili kuweza kuhakiki wateja wake kwa kutumia Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN), alama za vidole pamoja na maswali.

  Tovuti Salama (Secure Portal) Njia hii mdau hupatiwa akaunti maalum kwa ajili ya taasisi yake na akaunti hiyo hutumika kutengeneza akaunti ambazo huwawezesha wafanyakazi wa wake kufanya uhakiki wa wateja wao kwa kutumia taarifa za utambulisho wa Taifa. Njia hii hutumika kwa kumuuliza mteja maswali yanayotoka kwenye mfumo wa NIDA na akijibu kwa usahihi ndipo uhakiki unakamilika.

  Uhakiki kwa Njia ya Kadi (Offline Verification) Njia hii hutekelezwa kwa kuhusisha matumizi ya vifaa vya kusomea kadi (Card Readers) ambapo mdau anapatiwa kadi maalumu na NIDA yenye Mfumo wa Ufikiaji Salama (Secure Access Module - SAM Card) ili aweze kuhakiki na kusoma taarifa za mteja zilizopo kwenye kisilikoni (Chip) ya kadi ya Kitambulisho cha Taifa. Aidha mfumo huu humwezesha mdau kuhudumia wateja wake pasi na kuwa na huduma ya mtandao.

Taratibu za kuunganishwa kwenye Mfumo wa Utambuzi wa Watu (Data Sharing)

Zifuatazo ni taratibu za kuunganishwa kwenye Mfumo wa Utambuzi wa Watu (Data Sharing):-

1) Wasilisha barua ya ombi la hitaji la kushirikishwa taarifa za Usajili na Utambuzi wa Watu zilizoko kwenye Kanzidata inayosimamiwa na NIDA kwa Mkurugenzi Mkuu - NIDA, Ombi lako linatakiwa kuambatishwa na viambatisho vifuatavyo:-
   Leseni ya Usajili wa Biashara kutoka Mamlaka Simamizi/Dhibiti
   Namba ya Mlipa Kodi (TIN)
   Usanifu wa mtandao unaoonyesha uwekaji wa seva ya huduma iliyokusudiwa,
   Maelezo ya Kiungio (API) itakayotumika,

2) Nyaraka zilizowasilishwa zitatathminiwa ili kuthibitisha iwapo zinakidhi vigezo stahiki na ikiridhiwa, utaalikwa kwa kikao cha mashauriano ya kiufundi,

3) Nyaraka ya mkataba itatayarishwa baada ya hapo kuweka saini pande zote mbili, mazingira ya majaribio yatawekwa ili kuruhusu usanidi wa mfumo wa uendeshaji,

4) Huduma itatiwa saini na uzalishaji wa bili kuanzishwa,

5) Timu ya NIDA itasimamia Ufuatiliaji wa uendeshaji na Usaidizi wa API,

6) Taratibu tajwa hapo juu zikikamilika maunganisho na kanzidata huchukua angalau siku ...................

Iwapo utahitaji usaidizi zaidi, tafadhali usisite kuwasiliana nasi kushauriwa juu ya utoaji wa huduma ya kushirikishana taarifa unaodhibitiwa na Kanuni za Usajili na Utambulisho wa Watu (Kwa Ujumla wake) (Marekebisho), 2023 zisomwe kama moja na Kanuni za Usajili na Utambulisho wa Watu (Kwa Ujumla wake) za 2014.

Manufaa yanayotokana na kushirikishana taarifa (Data Sharing)

Yapo manufaa mengi yanayotokana na kushirikishana taarifa Mathalani:-

1) Usahihi wa taarifa kutokana na mifumo kuzungmza kwani sasa Mdau ana uwezo wa kumtambua mteja wake kimahsusi - NANI NI NANI?, YUKO WAPI? ANAFANYA NINI? NA ANAMILIKI NINI KATIKA TAIFA HILI?

2) Usalama wa Taariifa za Wateja, Mdau anapata fursa ya kutumia taarifa zilizohakikiwa ambazo zinakuwa salama zaidi kimatumizi,

3) Uharaka au wepesi wa kutoa huduma kwani sasa uhakiki na uingizaji taarifa kwenye mfumo hufanyika kwa muda mfupi na kwa wepesi zaidi hivyo urasimu kupungua kwa kiasi kikubwa,

4) Kupungua kwa uwezekano wa kutokea kwa matukio ya udanganyifu kutokana na mteja kutambulishwa kimahsusi kwa Namba ya Utambulisho wa Taifa isiyofanana na ya mteja mwingine vivyo hivyo kwa alama za vidole ama Kitambulisho cha Taifa kina Kisilikoni (Chip) inayohifadhi taarifa za mwombaji husika,

5) Inarahisisha kila kundi kupata huduma stahiki kwa gharama stahiki za huduma kwa mfano:- gharama za huduma mbalimbali kwa raia, wageni wakaazi na wakimbizi,

6) Kuongeza tija kiuzalishaji, Ufanisi kuongezeka huku gharama za Utambuzi wa wateja kupungua kutokana na kutumia taarifa za Utambuzi wa Watu kutoka kwenye Kanzidata ya NIDA.

7) Gharama za Utambuzi kupungua Ufanisi kuongezeka na kupelekea gharama za uendeshaji kushuka.

8) Kuondoa adha kwa wananchi ya kubeba utitiri wa Vitambulisho kwani sasa kupitia Mfumo wa Utambuzi wa watu/Kitambulisho cha Taifa wadau wataweza kuwatambua wateja wao NANI NI NANI?, YUKO WAPI? ANAFANYA NINI? NA ANAMILIKI NINI KATIKA TAIFA HILI? Maswali ambayo mfumo wetu unatoa majibu yake yanayomweka mdau na mteja kuwa katika sehemu salama kwani utambulisho na utambuzi unakuwa ni wa uhakika na sahihi.

9) Kichocheo cha utoaji haki na kurahisisha ufanyaji wa maamuzi sahihi na ya haraka kwa vyombo vinavyosimamia haki na vinginevyo kutokana na watu kutambulika kimahsusi kwa mfano kumtambua nani ni mmiliki wa laini ya simu, ardhi katika eneo fulani n.k.

Gharama za matumizi ya taarifa za Utambuzi wa Watu

Zipo gharama za matumizi ya taarifa za Usajili na Utambuzi wa Watu kama zinavyosomeka kwenye jedwali hapo chini:-

HUDUMA MHUSIKA GHARAMA
Kutumia taarifa zilizoko chini ya uangalizi wa mamlaka Raia 500 T.SH @ Mwombaji kubofya
Mgeni
Mwekezaji
Usd $1 @ mwombaji kubofya.
Mfanyakazi Usd $1 @ mwombaji kubofya.
Mmishenari Usd $1 @ mwombaji kubofya.
Mtafiti/Mwanafunzi Usd $1 @ mwombaji kubofya.
Mkimbizi Usd $1 @ mwombaji kubofya.