emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Jisajili, Tukutambue, Tukutambulishe


NIDA Yawafuata Diaspora

Na Alfan Mlacha-NIDA 

Katika kutekeleza majukumu yake ya utambuzi na usajili, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) haijawasahau Watanzania Wanaoishi Nje ya Nchi (Diaspora). 

Hii ni kwa sababu ni haki yao kutambuliwa, kusajiliwa na kupatiwa Vitambulisho vya Taifa ili viwawezeshe kupata huduma mbalimbali kama  kumiliki ardhi, kuhuisha hati za kusafiria pamoja na kusajili kampuni kwa kuzitaja chache. 

Meneja Usajili na Utambuzi, Andeshi Kiyoya akitoa ufafanuzi juu ya usajili wa Diaspora, alisema zaidi ya watu 1465 wamesajiliwa na kupatiwa Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) na Vitambulisho katika nchi saba.

Amezitaja nchi hizo kuwa ni Marekeni, Uingereza, Uholanzi, Canada, Comoro, Ubeligiji na Falme za Kiarabu (U.E.A) na kusisitiza kwamba dhamira ya NIDA ni kuendelea kuwafikia Diaspora wengi zaidi.

Utaratibu wa maombi ya usajili kwa Diaspora ni kama ulivyo kwa watanzania wengine ambapo mwombaji anatakiwa kujaza fomu ya maombi ya utambulisho na kuambatisha barua ya utambulisho, cheti cha kuzaliwa, Vitambulisho vya Taifa vya wazazi, pasi ya kusafiria (paspoti) na vyeti vya shule ya msingi au sekondari.

NIDA imeandaa kituo maalumu cha usajili wa Diaspora. Kituo hicho kipo katika jengo la Posta, Dar es Salaam (One Stop Center). 

Waombaji wanaweza kupata fomu ya usajili kupitia tovuti www.nida.go.tz au kufanya usajili mtandaoni kupitia kiunganishi  https://eonline.nida.go.tz