WANANCHI WANUFAIKA NA FURSA ZILIZOKO NCHINI KWA KUWA NA VITAMBULISHO VYA TAIFA
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa - NIDA imewezesha raia wa Tanzania, wageni wakaazi na wakimbizi waishio nchini kihalali kutambulika na hivyo kunufaika na huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Mfumo Mkuu wa Taifa wa Utambuzi wa Watu hapa Nchini uliojengwa na kusimamiwa na NIDA, umewezesha watu wote waliosajiliwa na Kutambuliwa kunufaika na fursa mbalimbali kama vile ajira, huduma za afya, elimu, umiliki wa ardhi, kilimo, ardhi, Mawasiliano na huduma nyingine za kijamii na kiuchumi.
Kitambulisho cha Taifa, kinamwezesha mwananchi kusajili laini ya Simu, kusajili Namba Maalumu ya Mlipa Kodi (TIN), kusajili Biashara/Kampuni - BRELA, kukata Hati ya kusafiria ya kielektroniki (E-Passport), kukata leseni ya udereva, kupata huduma ya Afya, kufungua akaunti ya Benki, kukopesheka Kirahisi kwenye taasisi za fedha, kujiunga na elimu katika ngazi mbalimbali, kupata mkopo wa Elimu ya Juu, Hati Miliki ya kiwanja na nyumba, kujidhamini na kudhamini Wengine.
Kitambulisho cha Taifa kimewasidia wananchi pia kupata ruzuku za pembejeo za kilimo kirahisi, kujisajili kwenye chama cha ushirika (wakulima, wavuvi, wafugaji na makundi mengine), Kupata msaada wa TASAF unaotolewa kwa kaya masikini, kuomba ajira Serikalini na kwenye sekta binafsi.
Jumla ya wananchi 20.6 wameshapatiwa Vitambulisho vya Taifa vinavyo wawezesha kunufaika na huduma hizo.
“Miundombinu muhimu ya kutolea hudumaza Usajili na Utambuzi wa Watu, imeboreshwa kulikoiwezesha NIDA, kutekeleza jukumu hili muhimu kwa ustawi na maendeleo ya wananchi katika sekta mbalimbali bila kusahau ulinzi na usalama wa nchi yetu”

