
WATUMISHI WA NIDA NYANDA ZA JUU KUSINI, WAMEASWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI.
WATUMISHI WA NIDA NYANDA ZA JUU KUSINI, WAMEASWA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI.
Na. Musa Kadiko
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), James Kaji amekutana na kufanya kikao na wafanyakazi wa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumapili 03 Agosti 2025.
Mkurungenzi Mkuu amewaasa na kuwasisitiza watumishi wa NIDA kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi ili kupunguza malalamiko yanatolewa na wananchi katika ofisi za usajili wakati wakupata huduma.
Katika hatua nyingine, James Kaji, amewapongeza viongozi ya NIDA kwa ushirikiano wanaotoa katika kutatua changamoto mbalimbali na amewataka kuongeza usimamizi zaidi ili kuboresha huduma za Mamlaka kwa wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala - NIDA, George Seni, ametoa maelekezo kwa Maafisa Usajili wa Mkoa na Wilaya wajitambue wao ni viongozi ambao wanamwakilisha Mkurugenzi Mkuu katika maeneo yao ya kazi, hivyo wahakikishe wanadumisha utawala bora, wanatunza ofisi pamoja na mali za Mamlaka.
Katika kikao hicho mwakilishi kutoka UTT AMIS, Dorice Mlenge, Afisa Masoko UTT AMIS - Dar es Salaam alipata nafasi ya kutoa elimu ya uwekezaji wa fedha na kukuza mitaji kwa watumishi wa umma, ambapo amewaeleza watumishi wa NIDA wawekeze UTT AMIS kwani sehemu sahihi na yenye faida katika kuweka akiba ya sasa na baada ya kusitaafu.