NIDA Wafunzwa Kujikinga na UKIMWI
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) imeendesha mafunzo kwa watumishi wa NIDA kuhusu VVU/UKIMWI na magonjwa sugu yasiyoambukiza katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu NIDA Dar es Salaam, Novemba 2024
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu NIDA, Aida Tesha amewataka watumishi hao kuzingatia mafunzo hayo na kuwa mabalozi kwa watumishi wengine kwa kuhakikisha wanapeleka elimu hii katika Idara, Vitengo na Ofisi zote za Wilaya nchini kwa lengo la kupambana na magojwa mahala pa kazi.
Alisema NIDA itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa watumishi ili kuhakikisha usalama wa afya ya mwili na kuendelea kutoa elimu kwa watumishi kupitia mafunzo mbalimbali pamoja na kuwawezesha kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya ya akili na mwili.
Kwa upande wake, Mwelimishaji Rika NIDA, Peter John alisema kuwa mara baada ya mafunzo haya kuisha wataenda katika Idara, Vitengo na Ofisi za Wilaya kwa ajili ya kutoa elimu hii kwa watumishi wenzao ili kuhakikisha NIDA inaendelea kuwa na rasilimali watu yenye afya na yenyekutegemewa katika majukumu ya kila siku.
Alisema kwamba watumishi wa umma wapo katika hatari kubwa ya kupata VVU/UKIMWI na magonjwa yasiyoambukiza ukiwemo ugonjwa wa shinikizo la damu, kansa, sukari na mengie mengi, kutokana na baadhi ya watumishi kutokuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara pamoja na ulaji wa vyakula usiozingatia lishe bora.
Alisema lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kuwahamasisha na kuwapatia elimu watumishi wengine katika meneo yao ya kazi na katika jamii inayowazunguka.