emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Jisajili, Tukutambue, Tukutambulishe


USAJILI NIDA SASA KIMTANDAO

Katika kuboresha na kurahisisha huduma za Usajili na Utambuzi wa Watu nchini Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imejenga mfumo unaowawezesha wananchi kujisajili na kutuma maombi yao kwa njia ya mtandao badala ya kwenda katika ofisi za usajili za wilaya kwa ajili ya kuchukua na kujaza fomu za maombi ya vitambulisho vya Taifa.

Usajili kwa njia hii ya mtandao unamwezesha mwananchi kujisajili yeye mwenyewe katika hatua ya awali mahali popote alipo ndani na nje ya nchi bila kufika katika ofisi za NIDA hivyo kupunguza foleni na kuokoa muda na usumbufu wa kufuata huduma hiyo wilayani.

“Wananchi wamenufaika na uwepo wa huduma ya Usajili Kimtandao kwani inawawezesha kujaza taarifa zao kwa usahihi na kuepuka uwezekano wa taarifa za mwombaji kukosewa pindi zinapoingizwa kwenye mfumo” 

Mwananchi Kujisajili Kimtandao anakuwa amekamilisha usajili wake kwa asilimia 75 na kutakiwa kukamilisha sehemu iliyobaki kwa kwenda katika ofisi za NIDA, wilayani kwa ajili ya kuhakikiwa uraia wake katika dawati la Maafisa wa Uhamiaji kisha kuchukuliwa alama za kibailojia na Maafisa wa NIDA.

Manufaa mengine wananchi hao wanayoyapata kutokana na kuwepo kwa mfumo huu ni pamoja na kuokoa gharama za kufika ofisini kila mara na muda ambao sasa wanaweza kuendelea kuutumia kwenye shughuli zao za Uzalishaji.

Kila mwananchi anawajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za Tanzania kuwa ya kidigitali kwa kutumia huduma zilizoandaliwa kwa ajili ya kuwarahisishia kupata huduma kama hii ya Kujisajili Kimtandao.

UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025

Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura