Fahamu namna ya kujaza fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa
Comments on “Fahamu namna ya kujaza fomu ya maombi ya Utambulisho wa Taifa”
Leave a Reply
Taarifa Kwa Umma
22 April
2024
2024
19 April
2024
2024
14 April
2024
2024
Nataka kurekebisha taarifa zangu online nifanyaje?
Huwezi kurekebisha taarifa yoyote online. Tafadhali nenda Ofisi ya NIDA Wilaya uliyopo kwa Maelekezo na msaada zaidi
kama ulijaza taarifa hizo baada ya muda ukaipeleka ila tofauti na tarehe uliojaza form
Haina shida ili mradi taarifa ni sahihi
Wakati najisajili nilikua wilaya na mkoa mwingine ila kwa sasa nime hama kabisa sikai hiyo wilaya nime hamia kwingine nina hitaji kubadilisha taarifa kuwa za wilaya na mkoa ninao kaa kwa sasa,nitafanyaje katika hali kama hii?
Salaam Ndg.
Unatakiwa kufika kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA katika wilaya unakoishi sasa na barua ya Serikali ya Mtaa ulikotoka na unakoishi sasa kwa hatua zaidi.
Utapatiwa Namba ya malipo ya Serikali ili uchangie huduma hiyo – shilingi TZS 20,000/=
Shukrani na karibu kuwasiliana nasi.
Wale tuliojiandikisha 2020 vitambulisho vyetu tunavipata lini?
Salaam Ndg. Tafadhali unashauriwa kufika Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.
Unaweza kutuma ombi lako https://demo.emalalamiko.egatest.go.tz/complaint ili kuangaliziwa moja kwa moja kwenye mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu.
Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID kwa haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.
Shukrani.
Naomba mnipe fom niweze kujaza ili nipate kitambulisho
SalaamNDg. unaweza kupakua fomu ya Usajili kupitia kiunganishi hiki:- https://nida.go.tz/swahili/wp-content/uploads/2019/07/APPLICATION-FORM-2A-NIDA.pdf