Kitengo cha Uratibu wa Ofisi za Wilaya kina jukumu la kuhakikisha kuwa shughuli zote za Mamlaka katika ngazi ya Wilaya na Mikoa zinafanyika kama ilivyokusudiwa. Katika kulitekeleza hili, Mamlaka imepanga kuanzisha ofisi katika Wilaya zote za Tanzania Bara na Zanzibar ili kufikisha huduma karibu na wananchi.

MAJUKUMU YA KITENGO:

Jukumu kuu la Kitengo ni kuhakikisha kuwa Mamlaka inakuwa na Ofisi za Wilaya ambazo zinakidhi mahitaji kimiundombinu, rasilimali watu na kiufanisi. Majukumu mengine ni:

  1. Kuratibu uanzishwaji wa Ofisi za Wilaya
  2. Kuhakikisha ofisi zilizoanzishwa zina samani na vitendea kazi vinavyotakiwa
  3. Kuhakikisha Ofisi zilizoanzishwa zina idadi ya watendaji wanaotakiwa
  4. Kuratibu utendaji kazi wa maofisa wa Wilaya.

MAFANIKIO.

Mpaka sasa jumla ya Ofisi za Wilaya arobaini na tano (45) zimeanzishwa katika Mikoa tisa (9). Mikoa hiyo na idadi ya ofisi katika mabano ni ifuatayo:

  1. Dar es Salaam (3),
  2. Pwani (6),
  3. Lindi (5),
  4. Mtwara (5),
  5. Morogoro (6),
  6. Tanga (8),
  7. Kilimanjaro (6),
  8. Ruvuma (5) na
  9. Arusha (1).

Aidha kutokana na wingi wa watu katika Jiji la Dar es Salaam, Mamlaka ilianzisha Ofisi za Tarafa ili kuweza kuwafikishia wananchi huduma karibu na maeneo yao na kupunguza msongamano katika ofisi za Wilaya. Hivyo, Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya ofisi nane (8) za Tarafa. Mchanganuo wa ofisi hizi ni kama ifuatavyo:

Wilaya ya Kinondoni: Goigi, Mikocheni na Kijitonyama

Wilaya ya Temeke: Kigamboni

Wilaya ya Ilala: Kariakoo, Bungoni, Tabata na Gongo la Mboto.

Katika ofisi zote (45) zilizoanzishwa tayari kuna Maofisa Wasajili wa Wilaya. Hata hivyo kuna baadhi ya Wilaya ambazo zina maafisa wasajili wawili hivyo kufanya Idadi ya maafisa wasajili kuwa (48). Wilaya hizo ni Ilala, Kinondoni na Kibaha. Aidha kila Wilaya ina Maafisa Wasajili Wasaidizi wawili (2). Idadi ya Maafisa Wasajili Wasaidizi walioko mikoani ni sabini na saba (77) kati yao saba (7) wako Dar es Salaam.

Kwa upande wa Zanzibar, kuna ofisi tisa (9) za wilaya hivyo kufanya jumla kuu ya ofisi zilizoanzishwa kwa nchi nzima kufikia hamsini na nne (54).

MATARAJIO:

Kitengo kina matarajio ya kuanzisha ofisi katika wilaya zote mia moja na arobaini na tatu (143) za Tanzania. Ikiwemo 133 Tanzania Bara na 10 Zanzibar.