MAJUKUMU YA KITENGO:

  1. Kupitia, kuhakiki na kuifanyia majaribio mifumo mbalimbali ya uthibiti wa ndani ya Mamlaka (Internal Controls).
  2. Kupitia, kuhakiki na kuifanyia majaribio mifumo ya kujikinga dhidi ya vihatarishi ndani ya Mamlaka (Institutional Risk Management).
  3. Kupitia, kuhakiki na kuifanyia majaribio mifumo ya kiutawala na uendeshaji ndani ya Mamlaka (Governance Systems).
  4. Kuitaarifu Menejimenti juu ya hali halisi ya maeneo tajwa hapo juu na kuishauri jinsi ya kufanya maboresho kama yanatakiwa.
  5. Kufanya ukaguzi na kutoa taarifa kwa Kamati ya Ukaguzi ya Mamlaka na Wizara ya Fedha kupitia Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali kila robo mwaka.

UTEKELEZAJI:

Pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali, Kitengo kimekuwa kikitekeleza majukumu yake kama inayotarajiwa.

MAFANIKIO:

Tangu uwepo wake Kitengo kimefanikiwa kuwasilisha mada kwa Wajumbe wa Kamati ya Menejimenti kuhusu majukumu ya Kitengo na mchango wa kila mjumbe na kila mtumishi wa Mamlaka katika kuimarisha mifumo ya udhibiti na ulinzi wa rasilimali za Mamlaka.

  1. Kitengo pia kimefanikiwa kuendesha semina ya siku moja kwa watumishi wa baadhi ya Idara na Vitengo vya Mamlaka kuhusu umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazotawala utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo taratibu za malipo na manunuzi ya umma.
  2. Kitengo kimekuwa kikiendesha shughuli za ukaguzi kwa kila robo ya mwaka kama inavyotakiwa.
  3. Kitengo kimekuwa kikitoa ushauri kwa Menejimenti kupitia taarifa zake za ukaguzi za kila robo ya mwaka.
  4. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imeendelea kupata Hati Safi za Ukaguzi wa Hesabu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.

MATARAJIO KATIKA MWAKA UJAO WA FEDHA:

  1. Kusimika mfumo wa Kitaasisi wa Menejimementi ya Vihatarishi (Institutional Risk Management).
  2. Kusimika Mfumo wa Uhakiki wa Ubora wa Shughuli za Ukaguzi wa Ndani (Quality Assurance and Improvement Programme).
  3. Kutekezeza majukumu ya Kitengo na kutoa taarifa zote zinazotakiwa kwa wakati.
  4. Kujenga uelewa zaidi kwa watumishi wa Mamlaka kuhusu shughuli za Kitengo.
  5. Kujenga uelewa zaidi kwa watumishi wa Mamlaka kuhusu umuhimu wa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazotawala utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo taratibu za malipo na manunuzi ya umma ili kuimarisha udhibiti na ulinzi wa rasilimali za Mamlaka.