Idara hii ni miongoni mwa Idara Kuu zilizopo katika Muundo wa Mamlaka uliopitishwa mwaka 2011 ambao unatokana na mabadiliko yaliyofanywa katika Muundo wa Mamlaka wa mwaka 2009. Hapo awali shughuli za Idara hii zilikuwa zinafanywa chini ya Idara ya Utawala na Fedha.
Idara hii sasa hivi inaongozwa na Mkurugenzi wa Mipango, Bajeti, Ufuatiliaji na Majengo. Idara hii ina vitengo vitatu ambapo vinaongozwa na Mameneja vitengo hivyo ni
- Mipango na Bajeti.
- Ufuatiliaji na Tathmini.
- Majengo.
MAJUKUMU
Idara hii ni miongoni mwa Idara zilizojitegemea ambayo ina majukumu makuu yafuatayo;
- Kuandaa Bajeti ya matumizi ya kawaida na yale ya maendeleo ya Mamlaka.
- Kuandaa taarifa za utekelezaji wa Bajeti kwa kipindi cha kila robo mwaka ya Mamlaka.
- Kuandaa taarifa za Mipango ya utekelezaji Mamlaka.
- Kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano wa Mamlaka.
- Kufanya tathimini na ufuatiliaji wa rasilimali fedha na rasilimaliwatu zinavyotumika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu na jinsi zinavyosaidia Mamlaka kufikia malengo yake.
- Kufanya tafiti mbalimbali zikazoibua chachu ya maendeleo na kusaidia kutatua matatizo mbalimbali ya Mamlaka.
- Kutunza takwimu za Mamlaka.
- Kutafuta majengo ya kukodi, kununua, kusimamia masuala ya upatikanaji wa viwanja kwa Mamlaka za jinsi ya kuviendeleza.
- Kusimamia masuala yote ya ujenzi, ukarabati.
- Kufuatailia nyaraka mbalimbali za Mamlaka.
MAFANIKIO
Idara hii haina muda mrefu tangu kuanzishwa kwake lakini imefanikiwa kufanya mambo mengi ambayo yameleta tija na manufaa kwa Mamlaka. Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na ;
- Idara imefanikisha maandalizi ya Bajeti ya Mamlaka kwa mwaka wa fedha 2012/2013 na kuwasilisha Wizarani na hatimaye kuweza kusomwa Bungeni na Mh. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
- Idara imekamilisha kuandaa mpango mkakati wa miaka mitatu wa Mamlaka 2012 – 2015 ambao ndio utakuwa dira ya Mamlaka katika kutekeleza na kufanikisha malengo yake.
- Idara imefanisha kuandaa taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Bajeti ya maendeleo na ile ya matumizi ya kawaida.
- Idara imefanikiwa kuendelea na mpango wa tathimini na ufuatiliaji, mpango ulitumika katika kuhakikisha rasilimaliwatu na rasilimali fedha zinatumika ipasavyo katika zoezi la uandikishaji na utambuzi wa watu lililofanywa katika Mkoa wa Dar es Salaam na mpango huo ndio utakuwa dira itakayotumika katika Mikoa mingine.
- Idara imefanikisha upatikanaji wa majengo ya kukodi kwa ajili ya ofisi za Mamalaka katika Wilaya zote za Mkoa wa Dare es Salaam na upatikanaji wa ofisi kwa baadhi ya Mikoa na Wilaya zake Tanzania Bara.
- Idara imefanikisha kusimamia ukarabati wa ofisi ya jengo lililokuwa Makao Makuu ya Magereza.
MATARAJIO.
Idara inatarajia kuwa Idara ya mfano kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ambao utaleta tija kwa Mamlaka. Aidha Idara inatarajia kwamba itakuwa ni kiunganishi kikubwa kati ya Idara nyingine zilizo katika Mamlaka pamoja na Idara katika Wizara nyingine. Pia inatarajia kuweka mipango endelevu katika kuhakikisha matumizi sahihi yanayofuata kanuni na sheria ya rasilimali watu na rasilimali fedha ili kuleta maendeleo kwa Mamlaka pamoja na Taifa kwa ujumla.
Tufuatilie