MAJUKUMU YA IDARA.
- Kutengeneza na kusimamia mifumo ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.
- Kuandaa mpango mkakati wa Idara.
- Kuwezesha mawasiliano ya kimtandao kutoka ofisi moja kwenda nyingine.
- Kuboresha mifumo ya Mamlaka.
- Kuandaa vifaa vya kielekroniki vya kufanyia mazoezi mbalimbali ya Mamlaka.
- Kusaidia uendeshaji wa mifumo na kutatua matatizo ya ki-mfumo pale inapotokea
- Kuhakikisha mifumo haiwi kikwazo katika ufanikishaji wa shughuli zote za Mamlaka
MAFANIKIO.
- Tangu kuwepo kwa Idara mifumo thabiti ya Usajili na Utambuzi wa watu imesimikwa.
- Tangu kuwepo kwa Idara mifumo mbalimbali inayosaidia kazi za kila siku za Mamlaka imetengenezwa na inatumika (HR Management System, Facility and Transport Management System).
- Idara imefanikiwa kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusu matumizi ya vifaa na mifumo mbalimbali inayotumika kwenye mazoezi mbalimbali ya Mamlaka.
- Idara imetengeneza Sera ya Matumizi ya vifaa na mifumo ya kompyuta.
- Taarifa za watumishi wa umma zimechukuliwa na kutumika kuchapishia Vitambulisho vya Taifa.
- Vitambulisho vya Taifa vimeanza kuchapishwa kwa kutumia mfumo wa Usajili na Utambuzi.
- Vitambulisho vya Taifa vimeanza kutolewa kwa kutumia vifaa vya utowaji vitambulisho na mawasiliano ya kimtandao.
- Idara imekuwa mstari wa mbele kutoa msaada wa ki-elektroniki katika muda unaotakiwa.
- Idara imefanikiwa kushauri idara nyingine ili kuweza kufanikisha mazoezi mbalimbali kwa kuzingatia kuwa matokeo ya mazoezi hayo yanaweza kuathiri idara yetu ki mfumo au mamlaka kwa ujumla.
- Idara imefanikiwa kuweka mazingira mazuri kwa watumishi wengine ili kuongeza ufanisi wa kazi hizo.
- Idara iko mstari wa mbele kuhakikisha watumishi wanakuwa salama muda wote wanapokuwa wakitumia mfumo wa ki-elektroniki.
- Idara imeweza kusaidia upatikanaji wa vitendea kazi (ICT equipments) kwa watumishi wa mamalaka.
UTEKELEZAJI.
Pamoja na kukabiliwa na changamoto mbalimbali, Idara ya Mifumo ya Uchambuzi wa Kompyuta imekuwa ikitekeleza majukumu yake kwa asilimia kubwa.
MATARAJIO.
- Kusimika mifumo mbalimbali inayowezesha (complement) mifumo mingine ya Mamlaka.
- Kujenga uelewa zaidi kwa watumishi wa Mamlaka kuhusu Sera ya matumizi ya vifaa na mifumo ya kompyuta.
- Kusomesha watumishi wa Idara katika fani mbalimbali.
- Kuboresha mifumo ya Mamlaka ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Tufuatilie