NIDA MSHINDI WA PILI RIADHA MITA MIA MOJA WANAUME

Na. Hadija Kombo – NIDA

Timu ya riadha ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imenyakua ushindi wa pili wa mbio za wanaume mita mia moja zilizofanyika Novemba 20, 2024 kwenye michezo ya SHIMMUTA inayoendelea katika Viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ufundi hapa Jijini Tanga.
Ushindi huo umepatikana baada ya timu hiyo kuongoza na kushika nafasi ya kwanza kwenye kundi lake katika hatua ya mchujo na kufanikiwa kuingia katika hatua ya fainali ya mbio hizo.
Akielezea umahiri ulioonyeshwa na mkimbiaji wa timu ya NIDA, Katibu wa NIDA Sports Club, Ndugu Sezari Migomba amesema wamefurahi si tu kwa kuwa wameshinda, bali wameshinda kwa mkimbiaji wa timu hiyo kumaliza kwa kasi bora zaidi ambayo wakimbiaji wengine kutoka timu pinzani zipatazo kumi walioingia fainali wameshindwa kufikia kasi hiyo “Tumefurahi sana kwa mkimbiaji wetu kuweza kutuletea ushindi kwa kukimbia kwa muda wa dakika 11 na sekunde 90 akizidiwa au kutanguliwa kwa sekunde Saba (7) tu na mshindi wa kwanza” Alisema Ndugu Sezari.
Aidha, mashindano ya riadha yatafanyika kwa muda wa siku mbili, ambapo Novemba 20, 2024 mbio za mita 5000, 400 na 100 kwa wanaume na wanawake zimefanyika. Mbio za mita 1500, 800, 200, mbio za magunia, kupokezana vijiti na watumishi wenye umri wa kuanzia miaka 50 (maarufu kama mbio za wazee) zitafanyika kwenye Viwanja hivyo Novemba 21, 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu