Namba ya NIDA ndio Utambulisho Wa kipekee wa Watanzania Kijamii, Uchumi

Na: Thomas Nyakabengwe – NIDA

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Namba ya Kipekee itakayomtambulisha kila raia nchini na kumwezesha kupata huduma mbalimbali za kijamii na kiuchumi kutoka serikalini na sekta binafsi ni Namba ya NIDA.

Waziri Mkuu alitoa maelekezo hayo wakati wa kufunga Kongamano la Nane la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

“Serikali imeelekeza kuwa namba ya NIDA ndio NAMBA JAMII ambayo itatumika katika utoaji na upokeaji wa huduma mbalimbali hapa nchini na kwa msingi huo niwahimize Watanzania wenzangu kuhakikisha wanapata namba ya NIDA ambayo ndio namba jamii.” alisema Waziri Mkuu.

Alisema kuwepo kwa namba ya kipekee inayomtambulisha kila raia nchini kuanzia anapozaliwa yaani jamii namba, ni utekelezaji wa mkakati wa kiuchumi wa kijiditali unaotekelezwa kwa tija na Serikali.

Kufikia Septemba, 2024 watu 21,191,608 (milioni 21.2) wamesajiliwa na kutambuliwa na kupatiwa Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) maarufu kama ‘NIDA Namba’.

NIDA pia imepanga kuanza usajili wa watu walio na umri wa nchini ya miaka 18 (Watoto) na kuwapatia namba ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ya kuhakikisha kila raia anakuwa na namba ya kipekee (NIDA Namba).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu