Na: Thomas W. Nyakabengwe – NIDA
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ally Senga Gugu ameipongeza Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kuzalisha asilimia 99 ya Vitambulisho kwa watu wenye Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN).
Pongezi hizo zimetolewa Juni 21, 2024 alipotembelea mabanda ya maonesho ya taasisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zinazoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park, Dodoma.
Kwa mujibu wa takwimu za NIDA, NIN zilizozalishwa ni 20,769,839 wakati vitambulisho vilivyozalishwa ni 21,322,098 na idadi ya watu waliosajiliwa ni 24,818,138.
Pamoja na pongezi hizo, aliwaasa wananchi kwenda kuchukua vitambulisho kwenye ofisi za Serikali za Mitaa ambako vimepelekwa ili kuwapunguzia umbali na foleni kwenye ofisi za NIDA.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma hufanyika kila mwaka Juni 16 – 23.
Naomba picha zangu za kitambulisho cha taifa
Picha zipi tena kaka Michael?
Naombeni msaada wa kubadilisha majina kwenye kitambulisho changu, Nimeshaandika barua lakini sijapata majibu imepita miezi miwili sasa👏
Tafadhali piga simu namba 0734220966 kufahamu status ya barua yako
Naomba ufafanuz Kuhusu wale waliofanya marekebisho ya taarf zao kweny nida an inachukua mda gani cadi mpya zitoke
Ndani ya siku 14 hadi 30 baada ya kuwa umepata kibali na kufanya mabadiliko
Naomba utaratibu wa kumchukulia kitambulisho cha NIDA, mzazi mzee na mgonjwa au mtoto ambaye yupo masomoni.
Mwenye kitambulisho aandike barua ya kukutambulisha na kukuruhusu umchukulie kitambulisho chake kisha nenda nayo ofisi za NIDA kwa hatua zaidi.Hakikisha una Kitambulisho chao au Namba yako ya NIDA unapoeenda kumchukulia.
Vipi kuhusu namba ya nida naambiwa Kwa maelezo zaidi nifike ofisin nilipojiandikisha sasa nafanyaje nami Niko mbali na Nina uhitaji wa huyo namba
Piga simu Kituo cha huduma kwa Mteja namba 0232210500 eleza shida yako utahudumiwa
Namba ya nida nimeshapata kupitia online ..baada ya wiki mbili toka nilipojiandikisha..sasa suala la vitambulisho kama vimetoka ntajuaje maana naweza nkaenda eneo husika nkaambiwa bado
Ndugu Edgar, huna haja ya kuhangaika. Unaweza kuangalia kama Kitambulisho kimetoka kwa kufungua link ifuatayo: https://vitambulisho.nida.go.tz kisha fuata maelekezo kufahamu kitambulisho chako kilipo.
Hi Nida, the link you shared is not connecting to know the location of your Nida Card. Kindly work on it.
Open this link https://vtambulisho.nida.go.tz to know where your ID is
Nahitaji kujua kama kitambulisho kimetoka
Tafadhali Fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz kujua kitambulisho chako kilipo
Naomba kujua utaratibu wa kurekebisha taarifa za NIDA kama mwaka wa kuzaliwa na jina
Andika barua kwa Mkurugenzi Mkuu, SLP 12324 Dar es Salaam ukiomba na kueleza sababu za kuomba mabadiliko hayo
Nahitaji kadi ya NIDA
Kama umejisajili tafadhali fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz kujua kitambulisho chako kilipo. Kama hujajisajili tafadhali fanya taratibu za kujaza fomu ya maombi
Najaribu kutafuta kitambulisho changu kilipo lakin website haikubal kufunguka
Fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz
LINK KUJUA KITAMBULISHO HAIFUNGUKI
Inawezekana ni shida ya mtandao
Mimi nilikuwa nilienda kulekebisha jina kwenye nidda yangu toka mwezi wa6 adi Leo mwezi wa8 haijafanikiwa nilikuwa naomba kueleweshwa kwann imekuwa hivi
Tafadhali fuatilia katika Ofisi za NIDA wilayani utafahamishwa shida ni nini
Najaribu kutafuta namba zangu za nida sipati nimejiandikisha yapata mwezi sasa
Fungua link ifuatayo https://services.nida.go.tz kisha chagua Fahamu NIN na kufuata maelekezo kupata namba yako ya NIDA. Kama bado haijatoka tafadhali tembelea ofisi ya NIDA ulikojiandikishia kwa usaidizi zaidi.
Nimepoteza kitambulsho changu naweza kupata kipyaa??
Ndiyo unapata. unachotakiwa hakikisha una loss report ya polisi, kisha nenda nayo Ofisi yoyote ya NIDA kwa ajili ya kupata Namba ya malipo, baada ya hapo rudi tena hapo NIDA ukiwa na hiyo loss report na pay slip kwa hatua zinazofuata ili kuchapishiwa kitambulisho kingine
naomba kujua namna ya kurekebisha taarifa, mfano jina la katikati na mwaka wa kuzaliwa
Naweza kupeleka vielelezo ili kubadilishiwa taarifa?