NIDA Yangara kwenye Maonesho ya Biashara na Utalii – Tanga, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Balozi, Batilda Buriani, akitoa Tuzo kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa kuwa Mshindi wa Kwanza
miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizoshiriki katika Maonesho ya 11 ya Biashara na Utalii ya Tanga, 2024, kutokana na kutoa Huduma Bora kwa Wateja. Maonesho ya Biashara na Utalii ya Tanga, yalihudhuriwa na Taasisi 109 za Kitaifa na Kimataifa na yalifanyika katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kuanzia tarehe 28 Mei – 06 Juni, 2024.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi, Dkt. Batilda Buriani, ambaye pia alikuwa Mgeni rasmi, akiitunuku NIDA, Tuzo na Cheti cha Ushindi, kutokana na kuibuka Mshindi wa Kwanza katika kutoa Huduma Bora kwa Wateja, miongoni mwa Taasisi za Serikali zilizoshiriki kwenye Maonesho ya 11 ya Biashara na Utalii ya Tanga, yaliyofanyika katika Viwanja vya Usagara, mkoani Tanga, kuanzia tarehe 28 Mei – 06 Juni, 2024. Kulia ni Hawa Maulidi, Afisa Usajili wa Ofisi ya Usajili ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), mkoani Tanga, katikati ni Agnes Gerald, Afisa Habari Mwandamizi kutoka NIDA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu