Vijana Wahimizwa Kujisajili Kimtandao ili Kuepuka Adha ya Foleni Kwenye Ofisi za Usajili za Wilaya – NIDA

Na: Agnes Gerald – NIDA

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA inaendelea kuwahimiza Vijana wanaofikisha miaka 18 na makundi mengine pia Kujisajili Kimtandao kupitia https://eonline.nida.go.tz ili kuondokana na adha isiyo ya lazima ya Kupanga foleni kwenye ofisi za Usajili za NIDA.

Ameyasema hayo Bw. Geofrey Tengeneza, Msemaji wa NIDA na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Juni 09, 2023 alipokuwa akitoa taarifa kwa umma kukumbushia wananchi hususan kundi la Vijana kutumia huduma hiyo ya Usajili Kimtandao ili waweze kufanya Usajili wa awali (Biographic Data Registration) ili wakifika kwenye ofisi za Usajili iwe ni kukamilisha hatua ya pili ya Biometric Data Caprturing) hatua ambayo haichukumi muda mrefu ikilinganishwa na Usajili kwa njia ya kawaida.

“Ninawahimiza vijana waliofikisha umri wa miaka 18 ambao wengi wao ni wahitimu wa Kidato cha sita wanaotaka kujiunga na JKT/elimu ya Juu na kuomba mikopo toka Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu na lile kundi la wanao omba ajira kujisajili kimtandao kupitia https://eonline.nida.go.tz ili kuepuka adha ya foleni isiyo ya lazima”

Amewaasa vijana kuachana na mwenendo wa kujitokeza kusajiliwa pindi panapokuwa na matukio yanayowalazimu kuwa na Utambulisho wa Taifa na badala yake wakishafikisha tu miaka 18 wajitokeze Kusajiliwa ili pindi wanapokutana na fursa waweze kuziendea pasipo kupata usumbufu kwa kutokuwa na maandalizi ya kuwa na Namba ya Kumtambulisha yeye ni Nani!.

Ameongezea kusema kuwa “vijana wengi wana simu janja lakini wengi wao huzitumia kwa vipaumbele vingine pekee badala ya kuzitumia pia Kujisajili Kimtandao” jambo hili husababisha foleni zisizo za lazima kwenye ofisi zetu za Usajili wilayani na kuibua malalamiko yasiyo ya lazima,

Aidha amewataka wanafunzi kutumia fursa vizuri pindi NIDA inapokuwa inaendesha mazoezi ya Usajili kwa kusogeza huduma kwenye shule za sekondari na vyuo kwani baadhi yao wenye sifa za kuwa na miaka 18 hupuuza na kusubiria matukio ya kuwalazimu kuhitaji Utambulisho yatukie ndipo hukimbilia kwenye ofisi za Usajili za NIDA wilayani na kusababisha foleni isiyo ya lazima kwa kutowajibika kutimiza wajibu wao pindi waliposogezewa huduma “Haki inaambatana na Wajibu” amesema Bw. Tengeneza.

Ametumia fursa hiyo pia kuwakumbusha wanafunzi wote wa sekondari na vyuoni ambao walisajiliwa siku za nyuma na wakajulishwa kuwa Vitambulisho vyao vimeshatoka na hadi hivi sasa bado hawajaja kuchukua  ili kuipunguzia NIDA malalamiko yasiyo ya lazima.

Jisajili, Tukutambue, Tukutambulishe!

Bofya: https:eonline.nida.go.tz


Bw. Geofrey Tengeneza, Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akitoa msisistizo kwa Vijana kuhakikisha wanatumia huduma ya Usajili Kimtandao ambayo Serikali kupitia NIDA imefanya jitihada za kuianzisha nchini Desemba 2022, alipokuwa akitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya Habari, NIDA Makao Makuu, Juni, 2023.


Bw. Geofrey Tengeneza, Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) akitoa msisistizo kwa Vijana kuhakikisha wanatumia huduma ya Usajili Kimtandao ambayo Serikali kupitia NIDA imefanya jitihada za kuianzisha nchini Desemba 2022, alipokuwa akitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya Habari, NIDA Makao Makuu, Juni, 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu