NIDA: Yasajili, Yatambua na Kutambulisha Wananchi kwenye Maonesho ya Tamasha la Maendeleo Kitaifa

Na: Agnes Gerald – NIDA

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inashiriki katika Maonesho ya Tamasha la Kitaifa la Kutoa Huduma na Kutangaza Shughuli za Serikali na Wadau wa Maendeleo Tanzania (Tanzania Development Festival) yaliyozinduliwa leo 27 Aprili, 2023 katika Viwanja vya Leaders Club na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wanawake Dkt. John Jingu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo.

Bi. Lilian Ezekiel, Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kutoka wilaya ya Kinondoni, amesema NIDA imeshiriki na kutoa huduma ya Usajili na Utambulisho wa Watu kwa Wananchi na Wadau wanaotembelea Banda la NIDA, kwa kuwapatia Utambulisho wa Taifa, Unaowatambulisha na kuwawezesha kupata huduma za kijamii na kiuchumi kirahisi kwenye mabanda ya Taasisi shiriki, za Serikali na Binafsi.

Amesema, NIDA, inashiriki Ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kwa Kuwatambua na Kuwatambulisha wananchi kwa kuwapa Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN) ambapo makundi ya wanawake ni miongoni mwao kwani lengo la Maonesho hayo ni kuelimisha na kuhamasisha jamii kutambua fursa mbalimbali za kiuchumi na kuzitumia Ili kujikwamua kiuchumi pamoja na elimu kuhusu kupiga vita ya Ukatili dhidi ya wanawake na watoto, malezi chanya ya wazazi na umuhimu wa kuwa na Taifa lenye kuzingatia, maadili.

Maonesho hayo, yamepambwa na kauli mbiu “Zijue Fursa, Imarisha Uchumi” Kataa Ukatili, Kazi Iendelee (ZIFIUKU) na yameanza leo Aprili 27, 2023 na yanatarajiwa kuhitimishwa Aprili 29, 2023.

Bi Lilian Ezekiel, Afisa Usajili toka Ofisi ya Usajili ya NIDA, Wilaya ya Kinondoni pamoja na Watumishi wenzake, Wakitoa huduma ya Usajili na Utambuzi wa Watu kwa Wananchi waliotembelea banda la NIDA kwenye Maonesho ya Tamasha la Maendeleo Kitaifa, yanayoendelea katika Viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu