NIDA Yatoa Mwongozo Mpya kwa Wanaohitaji Kubadilisha
Taarifa za Usajili.
Na: Agnes Gerald
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imetoa mwongozo mpya kwa wananchi wanaohitaji kubadilisha taarifa zao za usajili kwa sababu moja ama nyingine kwa lengo la kutoa maelekezo ya jinsi ya kubadilisha taarifa za mmiliki wa Kitambulisho/Utambulisho wa Taifa, kuzuia mabadiliko yenye lengo la kuficha na kupotosha ukweli ili kulinda maslahi ya wadau wengine wanaotumia taarifa zilizoko kwenye kanzidata ya Mamlaka, kulinda usahihi wa taarifa zinazotunzwa katika kanzidata ya NIDA, kuainisha vigezo vya anayestahili kubadilishiwa taarifa na ukomo wa maombi yanayoombewa mabadiliko husika pamoja na kuanisha nyaraka zinazohitajika katika kubadilisha taarifa za Mwombaji ambaye anaomba taarifa zake kufanyiwa mabadiliko.
Akizungumza na mwandishi wa Makala hii ofisini kwake Afisa Usajili Mwandamizi Bw. Ayoub Mwenda, amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa kuzingatia Sheria ya Usajili na Utambuzi wa watu ya mwaka 1986, Marejeo ya Mwaka 2012, Kanuni za Usajili na Utambuzi za mwaka 2014, Sheria ya Viapo ya mwaka 1966 inayotumika katika ubadilishaji wa taarifa na Sheria ya Vizazi na Vifo ya mwaka 1920 (Marejeo ya Mwaka 2012).
Ameongeza kusema, taarifa sahihi za mwananchi ni muhimu katika kukidhi hitaji la Utambuzi na namna ambayo mmiliki wa Kitambulisho/Utambulisho wa Taifa anavyoweza kutambuliwa katika jamii husika. Kutokana na sababu mbalimbali taarifa za mwananchi zinaweza kubadilika tofauti na zile za awali alizotoa wakati anajisajili na hivyo kuwepo haja ya kubadili taarifa zake. Baadhi ya sababu hizo ni kama vile sababu za kuolewa, kupata uraia wa Tanzania (kwa wale waliopata uraia wa kujiandikisha), kubadilisha makazi anayoishi mhusika, kubadilisha namba ya simu iliyosajiliwa awali, kukosewa kwa jina lililosajiliwa awali, mabadiliko ya taarifa za ajira (kazi) pamoja na marekebisho ya tarehe na mwezi wa kuzaliwa.
Kwa kuzingatia hayo Mamlaka imeona ni vema kuweka utaratibu ambao mmiliki wa Kitambulisho/Utambulisho wa Taifa anaweza kufanya mabadiliko ya baadhi ya taarifa zake alizoziwasilisha awali wakati wa Usajili na ambazo kwa sasa tayari ziko kwenye mfumo (kanzidata/hifadhi data) ya NIDA ili kukidhi hali na mazingira yake ya sasa lakini kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Chini ya mwongozo huo mabadiliko yatakayoruhusiwa kufanywa yanahusu jina la kwanza, au la kati, au la mwisho (ukoo) baada ya Mwombaji kukidhi vigezo na kuwasilisha nyaraka zinazo hitajika kwa mujibu wa mwongozo huo wa kubadilisha taarifa ambazo ni uthibitisho wa kisheria katika kubadilisha taarifa hizo. Taarifa nyingine zinazoweza kubadilishwa ni kama vile taarifa kuhusu hadhi ya Ndoa mfano aliyeolewa na kubadilisha jina kwa kutumia taarifa za ukoo wa mume/mwenza wake, Mwombaji aliyeolewa na kuachika kisheria anaweza kuruhusiwa kubadilisha taarifa zake na kurudia kujiandikisha kwa majina yake ya awali ya kabla hajaolewa kulingana na vyeti/nyaraka zake, Mwombaji aliyekosea kujaza baadhi ya taarifa zake yeye mwenyewe kwenye fomu ya Usajili na Utambuzi wa Watu wakati wa zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu, Mwombaji ambaye taarifa zake hazikuingizwa kwa usahihi kwenye mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu na Watendaji wake wakati wa Usajili.
Eneo jingine ni Mwombaji ambaye aliandikisha taarifa/majina yake yoyote kwenye kipengele cha majina mengine/maarufu na baadaye akahitaji majina yake hayo yaandikwe kwenye kipengele cha majina ya kwanza basi ataweza kurekebishiwa bila kuathiri utambulisho wake wa awali au taarifa zilizohifadhiwa katika mfumo na Jina la ukoo iwapo mwombaji ataamua kutumia jina ambalo tayari lipo kwenye upande wa majina ya wazazi wake mfano jina la Babu ambalo hapo awali hakulitumia.
Hata hivyo Bw. Mwenda amesema kuwa kuna taarifa za Usajili zisizoruhusiwa kubadilishwa isipokuwa kwa kibali maalumu cha Mkurugenzi Mkuu wa NIDA baada ya kufanyiwa kazi na Kamati ya Usajili na Utambuzi wa Watu. Taarifa hizo ni zile za Wazazi, makazi ya kudumu, mahali pa kuzaliwa, majina mawili/matatu, mwaka wa kuzaliwa na saini ya mwombaji.
Kwa upande wa watumishi wa umma utaratibu uko tofauti kidogo kwani mtumishi wa umma atakayehitaji kubadilisha majina au taarifa zake nyingine kama umri na kadhalika pamoja na kuambatanisha nyaraka za uthibitisho wa mabadiliko wanayotaka kufanya ni lazima wawe na kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Bw. Mwenda amewataka wananchi wote wenye kuhitaji huduma ya kubadili taarifa kufika kwenye ofisi za Usajili wilayani na kutoa ushirikiano kwa Maafisa Usajili katika ofisi hizo kwa kuwasilisha mahitaji yote stahiki na kuhakikisha kuwa mabadiliko hayo ya taarifa hayana lengo la kuficha utambulisho wa awali wa Mwombaji kwani ikibainika vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Mimi mbna nimejiandikisha lakin nida imeshindikana mpaka nimesha jaza fomu marambili ila nimekosa sijui tatizo nn
SALAAM NDG. HUTAKIWI KUJISAJILI ZAIDI YA MARA MOJA, HIVYO FIKA KWENYE OFISI YA USAJILI YA NIDA ULIKOFANYA USAJILI KWA MARA YA KWANZA KWA UTATUZI.
SHUKRANI.
Naitwa Dismas festus joseph naomba msaada wenu. Nikiingiza namba ya nida ajira portal naambiwa namba imeshatuma. Hii imetokana na sababu niliibiwa kitambulisho ndani ya nyumba na wezi walivunja mlango. Swali langu je naweza patiwa namba mpya?
Namba yako ni utambulisho wako huwa haibadiliki. Unashauriwa kufika kwenye ofisi za Usajili kwa msaada zaidi. Shukrani.
Habar yako ndugu Geofrey,
Kwa majina ni Ramadhani saidi Ramadhani, nilifanya taratibu za kubadili jina langu la mwsh kwenye Nida yangu Ambalo linasomeka,, Ramadhani saidi mwambashi instead of Ramadhani saidi Ramadhani, nashukuru nimefanya hatua zaidi ya kuikamilisha nimepita mpka kwa mkuu wa mkoa nimeshalipia kila kitu,, sas nimefika ofc Za Nida Tanga wamenitaka ni tangaze kwenye Gazeti la serikali kwamba natumia jina la Ramadhani saidi Ramadhani instead of Ramadhani saidi mwambashi, je kuna haja kwely ndugu yangu kubadili jina tu ambalo ni la ukoo, na mimi sio mtumishi nitangaze kwenye Gazeti la serikali Na likae mwezi mzima
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Habar mm naitwa Allen nilifanya zoezi la kujisajili nida toka mwenz wa 1 namba nimeshapata ila kitambuliaho ndo bado je changamoto ni nin??
Tafadhali Fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz kujua kitambulisho chako kilipo
Habari! Jina langu lililotoka kwenye kitambulisho cha NIDA lipo tofauti na majina yangu ya kwenye vyeti vyangu vyote mpaka TIN na Leseni ya gari, kwenye vyeti vingine vyote linasomeka Seif Saba Rajabu, Lakn kwenye kitambulisho cha NIDA linasomeka Seif Saba Mdee hivyo linanikwamisha kwenye mambo mengi hasa yanayohitaji kitambulisho cha NIDA, naomba kujua taratibu za kubadilisha hilo jina la kwenye kitambulisho cha NIDA lisomeke Seif Saba Rajabu. Cheti cha kuzaliwa ninacho
Salaam Ndg.,
Maaboresho ya Jina kwa Mtumishi wa Umma
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Barua ya Utambulisho kutoka kwa Mwajiri wa Mwombaji ikithibitisha taarifa ya ombi la kubadili taarifa.
ii. Kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Utumishi akiridhia mabadiliko hayo ya jina kufanyika.
iii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi
iv. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
v. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
vi. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
vii. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=.
Habari Mimi nilisajili au andikisha usajili toka mwaka 2017 sijapata kitambulisho lakini Namba imesha toka na tatizo jingine ni kuwa majina nitofauti kidogo yaani jina la mwisho liko katikati,na nimejalibu kwenda ofisi za nida hapa dodoma jibu analonipa huyu mdada ndo nakata tamaa kabisa anadai mpaka niwe na kadi ndo udumiwa na mimi Niko mbali sana na niliko andikisha je nifanyeje mkuu
Salaam Ndg. ili uhudumiwe kwenye Ofisi ya Usajili katika Wilaya nyingine mbali na ulikosajiliwa awali ni mpaka uwe na Kitambulisho cha Taifa, lah inawezekana iwapo utafika kwenye ofisi ulikosajiliwa na kutimiza vigezo. Shukrani.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Samahani nilikuwa naomba kuuliza ukishamaliza kufanya taratibu zote za kubakisha jina na ukalipia shilingi 20000 nida na kukabidhi taarifa naomba kuuliza inachukuwa mda gani mpaka jina hilo kubadilika na jina hilo likabadilika lenyewe au na namba ya nida inabadilika
Salaam Ndg.
Taarifa hubadilika lakini si namba ya NIDA. Shukrani.
Mm pia nna changamoto ya majina .Swali langu ni kama kunauwezekano wa kubadili jina la ili lifanane na vyeti vya elimu?
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu. ombi lako linaweza kukubaliwa ama kutokubaliwa kulingana na kukidhi vigezo na nia ya kubadili taarifa.
Msaada kwa tuliokosewa majina yetu badala ya masanja / naandikwa masaja nafanyaje rekebishiwa jina langu
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
hapo kuhusu viambatanishi , kina kinatakiwa kimoja wapo tu kwenye hiyo namba moja hata cheti cha kidato cha nne inatosha au vyote kwa pamoja naomba kujua hilo
Kwa kadiri unavyoambatisha vingi zaidi ndivyo zoezi linarahisishwa na kuharakishwa. Shukrani.
Naitwa AZON AYUBU AYUBU Nina shida moja mkuu, nilijiandikisha ili kupata kitambulisho mnamo mwaka 2017 nikiwa shuleni Musoma ila mpaka Sasa nimepata namba ya nida ila kitambulisho sijapata ni pia nilipokuwa najisajili kwenye ajira portal jina langu likatokea AZON AYUB AYUB badala ya AZON AYUBU AYUBU najiuliza nifanye nini au halitaleta shida kwenye ajira,, na mpaka sijapata kadi
Salaam Ndg.
Tafadhali fika Ofisi ya NIDA katika wilaya ulikosajiliwa au piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua kisha anza taratibu za kubadili taarifa kwani italeta shida.
Shukrani.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Hello Nida .Naomba msaada wenu nilipoteza kitambulisho changu nikafanya kuomba tena kwenu kupitia ofisi ya Wilaya ya Chato toka mwaka jana lakini hadi sasa sijapatiwa kitambulisho naambiwa bado hakijatoka.!
Salaam Ndg, huduma hiyo imeshasitishwa.
Kufahamu iwapo Kitambulisho Kimeshazalishwa
Tafadhali fika kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au unaweza kupiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimeshachapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.
Iwapo utafahamishwa kuwa NIN/Kitambulisho chako bado hakijazalishwa, utatakiwa kuendelea kusubiri huku ukifanya ufuatiliaji baada ya muda. Kwa mwenye uhitaji wa haraka unatakiwa kuwasilisha ombi na vielelezo vya kuthiitisha sababu ya uharaka ulionao kwa Afisa Usajili.
Shukrani.
Sorry kiongozi katika namba yangu ya NIDA Mwaka wangu wa KUZALIWA na Herufi za majina zimekosewa niliomba kujuwa utaratibu wa kubadrisha upoje
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa na jina ombi litashughulikiwa kwa utaratibu hapo chini pamoja na kutakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na
vii. Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
viii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
ix. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Mbona mtoto wangu mwaka wa kuzaliwa ulikosewa na makosa yalikuwa upande wa NIDA kwa sababu aliambatanisha nyaraka zote pamoja na cheti cha kuzaliwa. Lakini cha kushangaza hadi leo hakuna marekebisho yoyote yaliyofanyika badala yake wanamlazimisha kutumia NIDA namba waliyompatia kitu ambacho hakiwezekani kwa vile mwaka wa kuzaliwa uko tofauti na kwenye cheti cha kuzaliwa,vyeti vyake vyote. Kila siku wamebakia kumpiga tarehe kwenda kufuatilia japo alishapewa na fomu za kufanya marekebisho.
Salaam Ndg. Anashauriwa kufuata taratibu za kubadili taarifa. Namba ya Utambulisho wa Taifa huwa haibadiliki bali kinachobadilika ni taarifa za kwenye mfumo. Shukrani.
OMBI LA KUBORESHEWA TAARIFA
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Salaam Ndg. Anashauriwa kufuata taratibu za kubadili taarifa. Namba ya Utambulisho wa Taifa huwa haibadiliki bali kinachobadilika ni taarifa za kwenye mfumo. Shukrani.
Kwa majina naitwa Erick Benjamin naomba kufahamu taratibu za kubadilisha taarifa zangu katika kitambulisho cha taifa NIDA
Je Unahitaji kubadilisha taarifa gani?
Naulizia vigezo na viambatanisho vinavyohitajika kubadili jina la kwanza na tarehe ya kuzaliwa yaliyokosewa
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Badiliko la Tarehe na Mwezi wa Kuzaliwa
Mwombaji anahitajika kuwakilisha nyaraka zifuatazo Cheti cha kuzaliwa, Ikiwa Mwombaji tayari alishawasilisha cheti chake cha kuzaliwa hapo awali wakati anasajiliwa na kuja kuwawasilisha cheti kingine kipya cha kuzaliwa chenye utofauti wa taarifa; Afisa Usajili husika anaweza kuomba uthibitisho wa nyaraka hiyo toka kwa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) na Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (The Zanzibar Civil Status Registration Agency-ZCSRA).
Mwombaji aambatanishe na nakala ya Tangazo kutoka katika Gazeti la Serikali lenye taarifa za mabadiliko husika
Afisa Usajili Wilaya anaruhusiwa kuomba nyaraka nyingine yoyote ambayo ataona inafaa katika kuthibitisha maombi husika.
Hilo tangazo linapatikanaje
kwenye ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali. Shukrani.
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Samahani naitwa sebastian Johnbosco Chuhila, taarifa zimekosewa jina la baba na mama yaani Johnbosko, badala ya Johnbosco na Cecilia badala ya sesilia naomba kujua utaratibu WA kufatilia hili suala likoje maana tukipokuwa tunafanya usajili tulifatwa shuleni kwahyo sielewi kama naweza kwenda makao makuu ya NIDA mkoa au la maana Kila cheti ninacho kwaajili ya uthibitisho WA taarifa za majina yangu na wazazi pia. Pia nahitaji kupata kitambulisho chale. Ahsante
Salaam Ndg.
Unashauriwa kwenda kwenye ofisi ya Usajili katika wilaya uliyojaza wakati unasajiliwa (makazi unayoishi) ili kufanya marekebisho ya herufi. fika na nyaraka hizo pia.
Shukrani.
Habari,
Kwa mabadiliko ya taarifa tafadhali fika kwenye Ofisi ya NIDA ya Wilaya kwa msaada zaidi.
Asante.
Please let me kno the procedure to get copy of NIDA Id.
Salaam Ndg,
Kufahamu iwapo NIN imeshazalishwa
Ingia kwenye uwanja wa kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms), kwenye simu yoyote ya kiganjani kisha andika jina lako la 1*jina la mwisho*tarehe mwezi mwaka wa kuzaliwa*jina la 1 la mama*jina la mwisho la mama kama ulivyojaza kwenye fomu ya Usajili ya nida, kisha tuma kwenda na. 15096,
Mfano wa sms: Juma*Alli*02051995*Mariamu*Mwakabile (hakikisha unajaza taarifa kwa usahihi la haitoleta majibu)
Tafadhali piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja na: 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006, 0677 146 666,
Ingia kwenye tovuti ya NIDA (www.nida.go.tz), fungua neno Kitambulisho cha Taifa kwenye menyu kuu kisha fuata maelekezo au fungua link -https://services.nida.go.tz/nidportal/get nin.aspx au
Fika kwenye Ofisi ya Usajili ya Wilaya iliyo karibu nawe.
Shukran.
Mimi naitwa SAMWEL B CHIPILA. Taarifa zangu nilikosea jina na mwanzo kwenye kitambulisho limeandikwa SAMWELI. na mwaka wa kuzaliwa kwny kitambulisho kimeandikwa 1996 badala ya 1999. Na vyeti vyangu vyote nimetumia jina la SAMWEL na mwaka 1999. Sijui mtanisaidiaje
Tafadhali fika kwenye Ofisi ya Usajili NIDA na nyaraka zinazothibitisha ombi unalowasilisha. Aidha Afisa Usajili atajiridhisha juu ya nyaraka zilizoko kwenye mfumo. iwapo zintaarifa unazohitaji zibadilishwe atakupatia fomu Na. 3 na kuendelea na utaratibu wa mabadiliko. Unashauriwa kutoa ushirikiano kwa kufuata maelekezo yote msingi utakayopatiwa na Afisa Usajili. Shukrani.
Tafadhali rejea majibu tuliyokupatia kupitia mitandao yetu ya kijamii.
Habari,
Kwa majina naitwa Lusiano Prosper Mfalingundi nilileta barua yangu ya maombi ya kubadilisha jina na mwaka tangu tarehe 22/12/2021 lakini mpaka sasa sijapata majibu nilikua nauliza labda ni lini naweza yapata hayo majibu maana mambo mengi yanakwama na taratibu zote nimezifuata tunaombeni mtusikilize kama wananchi tuna shida sana
Tafadhali fanya ufuatiliaji kwenye ofisi ulikowasilisha barua, Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Habari
Kwa majina naitwa Ngazi Richard
Nilikuwa Nahitaji kubadilisha Jina langu la kwanza kwa kuwa Sasa ninatumia Jina la ubatizo Je nifuate utaratibu gani ili Jina langu hili la ubatizo litambulike kisheria pia..
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Mkuu samahan, ukisema “Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika”,una maana ipi, nashindwa kuelewa hapa.
Taarifa unayobadilisha kwa mafano kama ni ya jina kwenye cheti cha kuzaliwa lazima utoe tangazo la mabadiliko hayo kwa mp[iga chapa Mkuu wa Serikali (Government Printers) na kuambatisha hilo tangazo pia na ombi lako. Shukrani.
Habari!
Je kama niko mbali na ofisi ya mkoa nilioandikisha naweza kwenda ofisi ya nida ya mkoa niliopo na nikafanyiwa kazi?
Salaam Ndg. Sara Ngole, USajili wa awali mwombaji wa Utambulisho wa Taifa anapaswa kufika kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA katika wilaya anakoishi kuanzia miezi 6 na zaidi. baada ya Usajili huduma zingine unaweza kupatia katika ofisi yoyote ya Usajili. shukrani
.
mimi sina cheti Cha darasa la saba na Cha kidato Cha nne napaswa kufuata utaratibu upi ilikuweza kubadilishiwa jina kwenye kitambulisho
mimi sina cheti Cha darasa la saba wala cha kidato Cha nne napaswa kufuata utaratibu upi ilikuweza kubadilishiwa jina kwenye kitambulisho cha taifa
Habari, nilikuwa nahitaji niulize nawezaje kubadilsiha signature/sahihi kwenye kitambulisho changu process zake zikoje?
Salaam Ndg. Neema, tafadhali wasilisha ombi lako kwenye ofisi ya Usajili ukiambatisha nyaraka zako zenye Saini ya awali na utapewa fomu Na. 3 ambayo utaweka Saini Mpya ungependa iwekwe kwa sasa. Iwapo itaafikiwa na kamati maalumu ndipo kibali kitatolewa ILI afisa Msajili aendelee na hatua zaidi. Nje ya HAPO hatoruhusiwa kubadilisha. Shukrani
Nyaraka za awali kama zipi please i mean ni documents gani wanataka
Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha taarifa hizo.
Habari, nawezaje kubadilisha sahihi/signature kwenye kitambulisho changu?
Mimi nahitaji kubadilisha jina la mzazi wangu ,mara ya kwanza jina limebadilishwa. Lakini sio hilo ambalo limekusudiwa kwa maana lilikosewa kwenye didipol na nida ilikuwa tayari imebadilishwa sasa nikafata didipol nyingne ambayo naambiwa siwezi kubadili jina mara mbili ,hapo kwa msaada mnanisaidiaje na ni muhimu kwa mzazi wangu sababu nahitaji kumkatia bima ya afya .nashukuru
Salaam Ndg.Sadam, Utekelezaji wa shughuli yetu ya Usajili inategemea taasisi nyingine ikiwemo Wizara ya Ardhi kuthibitisha Kiapo cha Kubadili Jina. Kwetu tutaweza kukuhudumia pindi unapokuwa umekamilisha mahitaji yetu yote na SI vinginevyo. Shukrani
Habari
Naomba mawasiliano yako Kaka Geofray
Maelezo yangu ni Mengi kidogo
Salaam, tafadhali kituo cha huduma kwa mteja kuwasiliana nao ni Na: 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006, 0677 146 666
Ndugu
Geofrey Tengeneza
Samahani Sana naomba kuwasiliana na wewe
0658772356
Salaam, tafadhali kituo cha huduma kwa mteja kuwasiliana nao ni Na: 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006, 0677 146 666
Ndugu
Geofrey Tengeneza
Samahani Sana naomba tuwasiliane
0658772356
Salaam, tafadhali kituo cha huduma kwa mteja kuwasiliana nao ni Na: 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006, 0677 146 666
mimi sina cheti Cha darasa la saba wala cha kidato Cha nne napaswa kufuata utaratibu upi ilikuweza kubadilishiwa jina kwenye kitambulisho cha taifa naomba majibu mwanzo sikujibiwa
Salaam Ndg. tafadhali wasilisha nyaraka nyingi katika zilizo orodheshwa hapo chini.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
habar inachukua muda gani kupata namba baada ya kujiandikisha
Salaam, ili upate NIN, tangu kusajiliwa inachukua muda wa kuanzia wiki na kuendelea.
Naomba kujua utaratibu wa kubadilisha jina kwa mara ya pili ,maana mara ya kwanza nilibadilisha lkn limekosewa nataka kubadili tena kwa mara ya pili
Yangu mbona sipati jibu
Salaam Ndg. Sadam, unamaanisha hupati kitu gani?
Nimeuliza kuwa nataka kubadili jina kwa mara ya pili maana mara ya kwanza walikosea kwenye deed pol na tulikuwa tayari tumeitumia hiyo deed pol ya kwanza ,sasa nimechuka deed pol ya pili ambayo no jina sahihi ndio nataka kubadili tena ,je utaratibu upoje
Mimi naitwa braight sinkonde nilikuwa natatizo la utofauti wa majina katika kitambulisho cha NIDA naomba nisaidiwe kwa hilo
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Mimi nilikuwa naomba kubadilisha jina langu la kwanza na la mwisho pamoja na tarehe ya kuzaliwa lakini cheti cha kliniki ndo sina.nifuate utaribu upi?
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Badiliko la Mwaka wa Kuzaliwa
kuhusiana na badiliko la jina la tatu/ukoo nyaraka tajwa hapo juu zitatumika lakini mpaka kibali maalumu kitolewe na kamati maalumu baada ya kujiridhisha ndipo Afisa Usajili ataweza kuendelea na Utaratibu wa kubadili jina la tatu pia.
Kuhuu kubadili tarehe nyaraka za awali hapo juu zitatumika. Shukrani.
Nauliza kadi ya cliniki(Cheti cha kuzaliwa) inasomeka MBAVU ALLY lakini vyeti vyangu vyote vya shule vinasomeka MBAVU MBAVU ALLY je apo kuna uhitaji wa kwenda mahakamani kuapa
Salaam Ndg. Je unahitaji huduma gani?
Salaam Ndg. huduma inayotolewa ni ya Kitambulisho halisi. tafadhali fuatilia ukipatiwa ndipo utadurufu, tafadhali fika Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.
Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.
Shukrani.
Habari ?
mimi nilikua nataka kubadilisha picha ila nilienda ofc za wilaya ya ilemela nikaambiwa mpaka niwe nimepata kitabulisho kwanza na matumaini ya kukipata siyaoni napo nilifaniliwa kupata online copy mwanzoni
nafanyaje ili niweze kubadilisha picha ?
Salaam Ndg. kwa sasa huo ndio utaratibu unaofuatwa ili kubadili picha mpaka wakati wa kuhuisha Kitambulisho kinapoisha muda wake ama wakati wa kufanya “replacement”.
Kufahamu iwapo Kitambulisho Kimeshazalishwa
Tafadhali fika kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au unaweza kupiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimeshachapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.
Iwapo utafahamishwa kuwa NIN/Kitambulisho chako bado hakijazalishwa, unatakiwa kuendelea kusubiri huku ukifanya ufuatiliaji baada ya muda. Kwa Mwombaji mwenye uhitaji wa haraka unatakiwa kuwasilisha ombi na vielelezo vya kuthiitisha sababu ya uharaka ulionao kwa Afisa Usajili.
Shukrani.
Habari majina naitwa Abdallah msonga nahitaji kubadili jina la ukoo nifanyaje
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Angalizo: kubadili majina mawili, matatu ni mpaka kibali kitolewe na kamati maalumu.
Endapo mwaka was kuzaliwa umekosewa nyaraka gani natakiwa kuambatanisha Ili niweze kufanyiwa marekebisho.
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Nikitaka kubadili mahali pa kuzaliwa nafanyaje? aliyenisajilia awali aliandika nimezaliwa wilaya ya Morogoro mjini wakati mimi nilizaliwa wilaya ya Ulanga.Kadi yangu ya kliniki ninalo
Salaam ndg. mahali pa kuzaliwa mara nyingi ndipo makazi ya kudumu. unapaswa kufika na vielelezo vyako ofisini ikiwemo kadi ya kliniki. ombi lako likipokelewa litafanyiwa kazi baada ya kupatiwa kibali na kamati maalumu ya Usajili na Utambuzi wa Watu.
Shukrani.
Habari Nida nahitaji kubadilisha tarehe ya kuzaliwa ambayo iko tofauti na kwenye cheti cha kuzaliwa
Asante
Salaam Ndg, Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya tarehe/mwezi wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha tarehe/mwezi wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Iwapo nyaraka hitajika ulishawasilisha awali na ziko kwenye mfumo wa Utambuzi wa Watu wa NIDA, Afisa Usajili atafanya uhakiki kupitia taarifa ulizowasilisha awali zenye tarehe na mwezi unaohitaji usomeke.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika.
viii. Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho baada ya mwombaji kulipia shilingi 20,000/=
Habari; nahitaji kubadilisha jina langu la kwanza nataka kutumia jina la ubatizo, lakin taarifa zengine zote zipo sawa sibadilishi, ni Hilo jina TU la kwanza
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Mimi nilikosea taarifa zangu mwenyewe za mwezi tarehe n mwaka nitafanyaje ili kubadilisha taarifa zangu zifanane n vyeti vingne
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya tarehe, mwezi au mwaka wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha tarehe/mwezi wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Iwapo nyaraka hitajika ulishawasilisha awali na ziko kwenye mfumo wa Utambuzi wa Watu wa NIDA, Afisa Usajili atafanya uhakiki kupitia taarifa ulizowasilisha awali zenye tarehe na mwezi unaohitaji usomeke.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika.
viii. Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho baada ya mwombaji kulipia shilingi 20,000/=
Ndugu mimi nida yangu imekosewa terehe mwezi na mwaka nimejaribu kufatiria ila nimeambiwa tarehe na mwaka havi wezi badilika je ni kweli haviwezi badilika au maana leaving certificate ninazo pamoja na cheti cha kuzaliwa nimeambiwa haiwezekani kubadilishwa naomba msaada kweli haviwezi kubadilika
Habari,
Maombi ya mabadiliko ya Mwaka wa Kuzaliwa hayatoruhusiwa isipokuwa yamepata kibali maalum kutoka kwenye Kamati ya Usajili na Utambuzi. Aidha,
Mwombaji atatakiwa kuonyesha nyaraka zifuatazo; –
a) Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana kipindi cha awali kilichotafutwa na
Wazazi/Walezi wake,
b) Cheti cha kumaliza Shule ya Msingi
c) Kadi ya Kliniki (CLINIC)
d) Cheti cha kumaliza shule za Sekondari (Leaving Certificate)
e) Nyaraka yoyote ya awali yenye uthibitisho wa miaka yake husika iliyopatikana kabla ya kutambuliwa na kuandikishwa na kupata Kitambulisho cha Taifa.
f) Aidha, maombi yote yanayohusu kubadili mwaka wa kuzaliwa yanatakiwa kuwasilishwa kwa meneja wa Utambuzi na Usajili. Na yatumwe kwa email ya mir@nida.go.tz yakiambatanishwa na cheti cha kuzaliwa kutoka RITA/ZCSRA pamoja na mapendekezo ya Afisa Usajili wa Wilaya husika.
) Mabadiliko ya Taarifa ya Tarehe na Mwezi wa Kuzaliwa
Mwombaji anahitajika kuwakilisha nyaraka zifuatazo Cheti cha kuzaliwa,
a) Ikiwa Mwombaji tayari alishawasilisha cheti chake cha kuzaliwa hapo awali wakati anasajiliwa na kuja kuwawasilisha cheti kingine kipya cha kuzaliwa chenye utofauti wa taarifa; Afisa Usajili husika anaweza kuomba uthibitisho wa nyaraka hiyo toka kwa Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) na Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar (The Zanzibar Civil Status Registration Agency-ZCSRA).
b) Mwombaji aambatanishe na nakala ya Tangazo kutoka katika Gazeti la
Serikali lenye taarifa za mabadiliko husika
c) Afisa Usajili Wilaya anaruhusiwa kuomba nyaraka nyingine yoyote ambayo ataona inafaa katika kuthibitisha maombi husika.
Asante.
namna ya kupata hio page ya gazeti kwasababu naona ninahitaj kukosoa tarehe na jina.
.
Gazeti linapatikana kwenye ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikal
NAITWA GODWIN GODFREY MAPERA ,nataka kubadilisha mwaka wa kuzaliwa ilitokea makosa kwenye kitambulisho cha mpiga kula nikaenda nayo ivyo ivyo sikuwa najua nini cha kufanya,naomba process za kufata ili nibadilishe mwaka wangu wa kuzaliwa
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
viii. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
nipo manispaa ya Ilala ofisi zenu zipo sehemu gani ili niweze kuhudumiwa? au mpaka nije kwenye ofisi zenu kibaha?
Manispaa ya Ilala ni makazi yako ama ni kituo chako cha kazi>
naishi upanga ndo makazi yangu kwa sasa japo taharifa zangu zilichukuliwa wilaya ya bukoba mkoa wa kagera.
Tafadhali fika kwenye Kaunta yetu iliyoko kwenye Kituo cha Huduma Pamoja kilichopo Jengo la Posta na Simu, Posta Mpya, Dar Es Salaam.
Nataka kubadilisha jina la kati limerudiwa mara mbil,pia tarehe na mwaka wa kuzaliwa n tofaut na kwenye vyet vyang,kwan nilikosea kipind naandika bado sijapata kitambulisho naweza kubadilisha taarifa ofisi zozoze za Nida au mpaka nilipojiandikishia?…
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
viii. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Mwongozo uliotumiwa mwanzo unahusisha maboresho ya tarehe, mwezi au mwaka.

Huo ndo utaratibu wa kubadili jina au majina. iwapo unalenga kubadili majina mawili na zaidi, Afisa Usajili ataweza kufanya mabadiliko pindi ombi lako linapopatiwa kibali kutoka kwenye kamati maalumu lah hatoweza kufanya mabadiliko. kumbuka ombi lako linaweza kuafikiwa ama lah. msaada wowote utakaopatiwa kiofisi unazingatia misingi, taratibu,, sheria na miongozo iliyopo ya kutuongoza katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku ikiwemo katika kutoa huduma ya Usajili na Utambuzi kwenu wateja wetu. Shukrani.
Nimeelewa maelekezo yote ahxanteni. Lakini naomba kuuliza kama nahitaji kubadili majina mawili kama yote yalikosewa je mnanisaidiaje nyinyi kama ofisi?.. maana sina namna majina yote mawili yalikosewa
iwapo unalenga kubadili majina mawili na zaidi, Afisa Usajili ataweza kufanya mabadiliko pindi ombi lako linapopatiwa kibali kutoka kwenye kamati maalumu lah hatoweza kufanya mabadiliko. kumbuka ombi lako linaweza kuafikiwa ama lah. msaada wowote utakaopatiwa kiofisi unazingatia misingi, taratibu,, sheria na miongozo iliyopo ya kutuongoza katika kutekeleza majukumu yetu ya kila siku ikiwemo katika kutoa huduma ya Usajili na Utambuzi kwenu wateja wetu. Shukrani.
Habari za saiz nida. Mimi ninashida kitambulisho changu kimekosewa jina la kati na mwaka wa kuzaliwa je vitu gani ambavyo natakiwa kuwa navyo ili niweze rekebishiwa hili tatizo.
Asante
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
viii. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
je ukipata kiapo kutoka kwa mwanasheria kuhusu kubadili jina na tarehe kinapokelewa au lah?
Salaam Ndg. Hapana.
Nauliza kwamba kwenye usajiri wa kitambulisho just mwombaji kwenye jina la kati anaweza kuweka kifupi
Mfano. Adriano j. Simon
Hapana.
Nauliza majina kwenye Nida yangu yamekosewa jina la ukoo nifuate muongozo upo niweze kubadilishiwa mana napata changamoto hasa kwnye Nida kusoma majina tofauti na kwenye vyeti vyangu
Salaam Ndg. Nanjinga, Je jina la ukoo limekosewa kwa maana lililojazwa kwenye fomu ni lingine tofauti na unalotaka lijazwe sasa au ni herufi imekosewa?, pili makosa hayo ulifanya wewe wakati unajaza fomu ya Ombi la Utambulisho wa Taifa ama yalifanyika upande wetu . Shukrani.
Habari ndg.
Majina yangu kwenye kitambulisho cha NIDA ni SABAS AUGUST SHAYO.na kwenye vyeti vya taaluma ni SABAS SHAYO AUGUST.
JE kuna uhitaji wa kubadilisha hilo jina la kwenye NIDA liwe sawa na majina ya vyeti vya taaluma? Msaada tafadhali
Salaam Ndg. August, ukitumia majina yanayofanan ni vizuri zaidi ili utambulike kirahisi. uamuzi uko kwako kuamua kutumia yaliyo kwenye vyeti vya taaluma yafanane na kadi ya NIDA ama taarifa zilizoko kwenye kadi ya NIDA zibadilishwe na kufanan na zilizoko kwenye vyeti vyako vya taaluma kwani majina yote yapo isipokuwa ni mpangilio. Shukrani.
Ahsante. Nilikuwa na wasi wasi labda inaweza kuonekanana majina ni tofauti endapo nitaenda kufanya kazi taasisi za serikali.
Utaratibu wa kubadilisha taarifa ukifuatwa, rejea ya uthibitisho pindi inahitajika itakuwepo. kikubwa kufuata utaratibu.
Salaam Ndg. Sabas, tafdhali fuata maelekezo tuliyokupatia kupitia njia zetu nyingine za mawasiliano na wateja ambako pia uliuliza swali hili. Shukrani.
Jina langu mm nimekosewa vyeti vyangu vyote ni Emmanuel victor mpelwa afu jina la nida victor Emmanuel Robert pia na mwaka umekosewa naomba msaada nifanyeji
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na
vii. Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
viii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
ix. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Kumbuka kuwa NIDA hunakili taarifa zilizoko kwenye viambata vyako, hivyo lazima wewe mwenyewwe utakuwa umehusika katika kuwasilisha nyaraka zenye taarifa tofauti. Shukrani.
Mimi naitwa godlisten John mollel kutoka arumeru Arusha nimepeleka document zangu kwaajili ya kufanyiwa marekebisho taarifa zangu za kitambulisho Cha taifa Ili ziendane na taarifa za vyeti vyangu wakaniambia nitumie makao makuu maana wao hawawezi
Salaam Ndg. Ni taarifa gani ulikuwa unalenga kubadilishiwa?. Shukrani.
Naomba kuuliza, ikiwa nahitaji kubadili jina je ni lazima niwe na kitambulisho ambayo jina limekosewa
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina si lazima uwe na Kitambulisho cha awali kwani watarejea kwenye mfumo.
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Je tangalo la gazeti la serikali litachukua muda gani kutoka
Hi
Salaam Ndg. Godlisten, karibu kwenye ukurasa wetu wa Tovuti tukuhudumie. Shukrani.
KWA JINA NAITWA ISSA MOHAMED ISSA,NAMBA YANGU YA NIDA INAONYESHA NIMEZALIWA TAREHE 12.05.1981 NA MM CHETI CHANGU CHA KUZALIWA PAMOJA NA VYETI VYANGU VYOTE VYA ”ACAMDEMIC CERTIFICATES” VINAONYESHA TAREHE YA KUZALIWA 30.12.1985..NAOMBA MSAADA PLEASE
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya tarehe, mwezi au mwaka wa kuzaliwa ombi litashughulikiwa kwa utaratibu hapo chini pamoja na kutakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na
vii. Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
viii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
ix. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Mimi naitwa godlisten John mollel kutoka arumeru Arusha nimepeleka document zangu kwaajili ya kufanyiwa marekebisho taarifa za kitambulisho Cha taifa Ili ziendane na taarifa za vyeti vyangu wakaniambia nitume makao makuu nikatuma kwa EMS mpaka na leo sijapata majibu
Maombi yote ya aina hiyo yanafanyiwa kazi katika ofisi ya Usajili wilayani isipokuwa kwa machache ambapo ni Afisa Usajili katika Ofisi husika atapaswa kutuma maombi hayo Makao Makuu kwa njia ya barua pepe kwenye kamati maalumu ili apatiwe kibali cha kubadilisha taarifa kama za makazi ya kudumu, mwaka wa kuzaliwa, saini, taarifa za wazazi. n.k
Mimi naitwa godlisten John mollel kutoka arumeru Arusha nimepeleka document zangu kwaajili ya kufanyiwa marekebisho ya taarifa za kitambulisho Cha taifa Ili ziendane na taarifa za vyeti vyangu wakaniambia nitume makao makuu nikatuma document zangu kwa EMS mpaka na leo sijapata majibu
Maombi yote ya aina hiyo yanafanyiwa kazi katika ofisi ya Usajili wilayani isipokuwa kwa machache ambapo ni Afisa Usajili katika Ofisi husika atapaswa kutuma maombi hayo Makao Makuu kwa njia ya barua pepe kwenye kamati maalumu ili apatiwe kibali cha kubadilisha taarifa kama za makazi ya kudumu, mwaka wa kuzaliwa, saini, taarifa za wazazi. n.k
Mimi nilikuwa nataka nibadilishiwe mwaka na herufi isomeke godlisten badala ya godlistern japo nimepeleka document zote na wakaniambia nitume makao makuu
Hello! Nlikuwa nataka kubadilisha signature, what are the procedures?
Salaam Ndg. Utafika kwenye Ofisi ya Usajili Wilaya iliyo karibu nawe na kuwasilisha ombi lako kwa kujaza fomu Na. 3 ambapo utapata fursa ya kuonyesha saini yako mpya ungependa ionekane vipi na kuambatisha nyaraka zenye taarifa ya saini ya awali. Afisa Usajili atawasilisha ombi lako kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu kwa kibali. Kamati ikijiridhisha na kupitisha ombi lako ndipo mabadiliko yatafanyika.
Muhimu:- Ombi lako linaweza kukubliwa ama kutokubaliwa kutegemeana na nia ya mteja kutaka kubadili taarifa hiyo pamoja na sababu mbalimbali za kiusalama kuzingatiwa. Shukrani.
Nilisomea jina la mwezi wangu toka darasa la kwanza, kwenye Eneo la kibarua nikalazimika kusajili kwa jina hilohilo la mwezi. Sasa nimebahatika kukutana na ndugu zangu na kuhitaji kubadilisha Nina la baba yangu ambalo ndio lipo kwenye kadi ya clinic kwa Usajili. Mwaka wakuzaliwa, iko sahihi, jina langu lipo sahihi isipokua middle and last name ndio nahitaji mabadiliko vipi linawezekana?
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina hususan la mwisho ni mpaka kibali kitolewe baada ya kuwasilisha ombi lako. linaweza kukubaliwa ama kutokubaliwa kutegemeana na lengo la ombi la kubadilisha jina na nyaraka utakazowasilisha.
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Nahitaji kubadili jina nililosajilia Nida kwa kutumia majina yaliyomo kwa kadi ya mpiga kura, nahitaji kuweka majina yaliyo kwenye kadi ya kuzaliwa msaada.
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Hello mr Geofrey hongera kwa kazi nzuri ya kutoa elimu mtandaoni naomba kuuliza kama kuna uwezekano wa kubadili sain inanisumbua sana hiyo chorachora natamani niibadilishe iwe ya kuandika tu kawaida
Salaam Ndg.
Utnatakiwa kufika kwenye Ofisi ya Usajili Wilaya iliyo karibu nawe na kuwasilisha ombi lako kwa kujaza fomu Na. 3 ambapo utapata fursa ya kuonyesha saini yako mpya ungependa ionekane vipi na kuambatisha nyaraka zenye taarifa ya saini ya awali. Afisa Usajili atawasilisha ombi lako kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu kwa kibali. kamati ikijiridhisha na kupitisha ombi lako ndipo mabadiliko yatafanyika.
Muhimu:- ombi lako linaweza kukubaliwa ama kukataliwa kutegemeana na uzito wa sababu uliyotoa na nia ya kutaka kubadili saini.
shukrani.
Habari,nachangamoto ya taarifa zangu za NIDA kwenye sehemu ya PLACE OF BIRTH imeandikwa KONDOA ambayo sio sahihi. Sehemu sahihi iliyopaswa kurekodiwa ni KONGWA. Nafanyaje kubadilisha taarifa hizo ?
Salaam Ndg. Unapaswa kuwasilisha nyaraka yenye kuthibitisha maelezo yako hususan iliyotafutwa wakati umezaliwa si sasa kama cheti cha kuzaliwa, tangazo, kadi ya kliniki …. ombi lako litafanyiwa mapitio na kamati maalumu, iwapo watajiridhisha ndipo mabadiliko yatafanywa. Kumbuka ombi lako linaweza kukubalika ama lah kutegemeana na utoshelezi wa nyaraka za kuthibitisha maelezo yako.Shukrani
Habari naitwa shivji nahitaji kubadilisha namba ya simu kwenye taarifa za nida kwani wakati natuma maombi ya kupata namba ya nida sikua na simu hivoo niliweka namba ya mzazi wangu
Salaam Ndg. Shivji, tafadhali fika kwenye Ofisi yoyote ya Usajili ya NIDA iliyo karibu nawe, wilayani. Afisa Usajili atajiridhisha iwapo namba ya simu unayotaka ibadilishwe imesajiliwa kwa alama za vidole kwa kutumia Namba yako ya Utambulisho wa Taifa ndipo atabadilisha. Shukrani.
Habari nahitaji kubadikisha jina la ukoo na tayari Nina deedpoll ,je inawezekana !? Naitajika kwenda ofisi ya wilayani au makaoo makuu!?
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Kuhusiana na Jina la ukoo, ni mpaka kibali maalumu kitakapotolewa na Kamati Maalumu ndipo Afisa Usajili ataruhusiwa kubadilisha taarifa yako ya jina la ukoo. Shukrani.
Habari,Jina langu la katikati limewekwa mwisho na kina la mwisho limewekwa katikati hivyo nahitaji kufanya marekebisho:Badala yakisomeka,DAVID ELIAS MKULAGO basi lisomeke DAVID MKULAGO ELIAS
Tafadhali fika kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA katika wilaya iliyo karibu nawe kufanya uhakiki juu ya unachokieleza ili aweze kuendelea na taratibu za mabadiliko. tafadhali unaombwa kutoa ushirikiano kwa maelekezo yoyote ya nyaraka atakazohitaji uwasilishe. Shukrani.
Habari, Mimi kwenye kitambulisho changu marekebisho yalikuwa ni mwezi wa kuzaliwa na jina kuwepo la tatu(ambalo ndo natumia kwenye nyaraka zangu nyingi) na sio la nne. Sasa nilifanya taratibu zote na malipo mwaka 2019 pamoja na kurudisha kile cha zamani kwahiyo nikawa nasubiri kitambulisho kipya. Sasa kwa kipind chote hichi nilikuwa nimesafiri nje ya nchi na sasa hivi nimerudi nataka nifuatilie nione lakini maswali yangu makuu ni mawili, 1. je pamoja na mabadiriko ya mwezi wa kuzaliwa namba yangu ya NIDA itabadirika ? NA 2. je uwepo wa jina langu la nne badala ya la tatu ni kikwazo maana yote yanasoma kwenye my Birth Certificate?. Asante
Salaam Ndg. Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN) maarufu namba ya NIDA , haibadiliki kwani ni Utambulisho wako wa Taifa.
Ni vizuri zaidi majina yanavyosomeka kwenye Kitambulisho cha Taifa yakafanana na ya kwenye nyaraka zako. Shukrani.
Habari zenu. Samahani naomba kuuliza utaratibu wa kubadilisha majina maana langu lilikosewa
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Samahan mimi naitwa Isack naitaji kujua ditails zangu zote nilizojazaga kwenye nida ili nione wapi kuna kosa nafanyaje
Salaam Ndg. mwenye uwezo wa kuona taarifa zote ni NIDA, wakati wa kuhuisha Kitambulisho kuna ruhusa ya kuhuisha baadhi ya taarifa kama zimebadilika kwa mfano za elimu, ndoa makazi n.k kwa utaratibu maalumu na vigezo vilivyowekwa kuzingatiw. hakuna anayeweza/kuruhusiwa kubadilisha taarifa zote Shukrani
Habari ,Jina langu naitwa IVONA KAUMBYA EMMANUEL kwenye usajili wa nida nilitumia IVONA ASIMWE EMMANUEL nataka kubadili ilo jina la katikati maana vyeti vyangu vyote vya shule kila kitu kina jina Hilo moja kasolo tu kwenye kitambulisho Cha nida nataka kubadili lisomeke kama vyeti vingine.
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
NAITWA MATHAYO KIVINGA NAOMBA KUJUA UTARATIBU WA KUBADILI SIGNATURE KWANI MIMI NI MTUMISHI NINAONA WAZEE WASTAAFU WANAVYO TAABIKA BAADA YA SIGNATURE KUTOFAUTIANA
Salaam Ndg.
Utnatakiwa kufika kwenye Ofisi ya Usajili Wilaya iliyo karibu nawe na kuwasilisha ombi lako kwa kujaza fomu Na. 3 ambapo utapata fursa ya kuonyesha saini yako mpya ungependa ionekane vipi na kuambatisha nyaraka zenye taarifa ya saini ya awali. Afisa Usajili atawasilisha ombi lako kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu kwa kibali. kamati ikijiridhisha na kupitisha ombi lako ndipo mabadiliko yatafanyika.
Muhimu:- ombi lako linaweza kukubaliwa ama kukataliwa kutegemeana na uzito wa sababu uliyotoa na nia ya kutaka kubadili saini.
Shukrani.
naitwa PETER KATANAGE THELESPHORY jina langu la kati lilikosewa na Msajili akaandika KATANANGE hivyo baadhi ya taarifa zangu zimegoma MFANO TRA NA Brela je nifanyeje
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Hbar bw goddfrey hii namba 1 kkkatika hivi ulivyoviorodhesha cjui chet cha là7,cha kuzaliwa,tangazo,cārd ya clinic,kidato cha nne na living certf,so tunachagua kimoja wapo?au mpaka vyote?
Vinapokuwa vingi ndipo uwezekano wa kubadilishiwa unakuwa rahisi zaidi.
Hichi kipengele cha kwanza katika hivi ulivyoviorodhesha cjui chet cha là7,cha kuzaliwa,tangazo,cārd ya clinic,kidato cha nne na living certf,so tunachagua kimoja wapo?au mpaka vyote?
Reply
Salaam Ndg. Iddi, viambatisho vinapokuwa vingi ndipo uwezekano wa kubadilishiwa unakuwa rahisi zaidi.
Hichi kipengele cha kwanza katika hivi ulivyoviorodhesha cjui chet cha là7,cha kuzaliwa,tangazo,cārd ya clinic,kidato cha nne na living certf,so tunachagua kimoja wapo?au mpaka vyote?
Salaam Ndg. Iddi, vipengele vyote vianahusika na ni vya lazima. Shukrani.
Mimi nimezaliwa mwaka 1986 ila kitambulisho kinaonyesha 1988,lakin tin namba,kitambulsho cha mpiga kura na leseni ya udereva ni mwaka 86.ila hvyo vitambulsho vyote vimepatkana kbla ya nida.sasa nafanyaje kubdlsha mwaka kutoka 88 kwnda 86 na namb za simu pia,kitambulisho nlkpatia temeke ila kwa sasa nimehamia mwanza
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa ombi litashughulikiwa kwa utaratibu hapo chini pamoja na kutakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya Kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Usajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na Afisa Usajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
viii. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Hello mimi nina shida moja nahitaji msaada nilifanya usajili wa Namba ya NIDA since 2017 leo ndo nimepata namba baada ya kurudia usajili haukupokelewa shida iko nilifanya change of Name na deedpoll ninayo kinahitajika nini ili niweze kubadili jina kwenye NIDA ambayo nililifanyia mabadiliko
Mabadiliko yanaweza kukubaliwa kufanyika ama yasifanyike kutegemeana na vigezo
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Habari.
Kwa jina naitwa DENIS lakini nida wametoa jina limeandikwa DEENIS maana yake wameongeza E kwenye jina langu tofauti na nilivyojaza taarifa zangu kwenye fomu yenu.nifanye nini ili kurekebisha taarifa zangu hizo ziende sawa na documents zangu?
Salaam Ndg. tafadhali fika kwenye Ofisi ya Usajili kuhakikiwa kwanza juu ya unachokieleza. iwapo ndivyo marekebisho yatafanyika kulingana na atakavyokuelekeza nyaraka za kuwasilisha.
Nataka kuuliza namna ya kupata kitambulisho cha nida
Je umeshajitokeza Kusajiliwa?
Habri,nataka kuongeza herufi ya jina langu kwenye kitambulisho cha nida ili ifanane na vitambulisho vya shule msaada tafadhali
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Samahani kiongozi, taarifa zangu za NIDA zinafanana na cheti cha kuzaliwa lakini hazifanani na vyeti vya elimu maana kwenye elimu nilitumia majina mawili lakini kwenye nida yapo matatu nifanyaje?
Salaam Ndg. Ni vizuri wewe ukajieleza unahitaji huduma gani kutoka kwetu!
Nimependa kuuliza
Salaam Ndg. karibu kwenye ukurasa wetu wa Tovuti tukuhudumie kwa kukupatia elimu kuhusiana na Usajili na Utambuzi wa Watu ambao matokeo yake ni kutoa Utambulisho wa Taifa (NIN) na hatimaye Kitambulisho cha Taifa kwa raia, wageni na wakimbizi. Shukrani.
Marekebisho ni Hadi kitambulisho kitoke au
Salaam NDg. Shelua, marekebisho ya taarifa yanaweza kufanyika iwapo mwombaji kakidhi vigezo pasipo kuwepo kwa ulazima wa Kitambulisho cha Taifa kuwa kimeshachapishwa. Shukrani.
Sijapata kitambulisho Hadi Leo nimejisajiri mwaka 2017 walikuja shuleni nimependa ofisi za ni wamesema Hadi cheti Cha kuzaliwa wakati wengine wamepata
Salaam Ndg. fika Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.
Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.
Shukrani.
Samahani Kwa majina naitwa Hashim Abdallah Nyagawa, nilijiandikisha NIDA mwaka 2017 mwanzo kabisa was uandikishaji lakini jina langu halikutoka wanaotakiwa kupata vitambulisho na mpaka leo na sijapata mlejesho hata nikifatilia
Salaam Ndg. fika Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.
Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.
Shukrani.
Je? Naweza kusaidiwa kubadilishiwa taarifa zangu kwenye kitambulisho change cha nida ikiwemo tarehe ya kuzaliwa na mwaka
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya tareha/mwaka wa kuzaliwa ombi litashughulikiwa kwa utaratibu hapo chini pamoja na kutakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha tarehe/mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na
vii. Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
viii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
ix. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Nahitaji kuzihakiki taarifa nilizojaza wakati wa kujiandikisha Ili kupata kitambulisho Cha taifa
je unahitaji kuhakiki taarifa gani? maana si rahisi kuhakiki zote. Wakati wa kuhuisha Kitambulisho cha Taifa kuna hiyo fursa pia kwa baadhi ya taarifa kama vile za makazi, ndoa elimu n.k
Habari NIDA poleni na majukumu pia hongereni kwa kujibu maswali ya wadau.Nimepata majibu kwenye hatua za kubadilisha majina.
Nilikuwa na swali lifuatalo;
1.(i) Tangazo la gazeti la serikali lipo vipi na mchakato wake upo vp na unaanzia wapi?
(ii) Mahali nilipojiandikishia hadi kupata kitambulisho ni wilaya ya KILOSA-MOROGORO
Je naweza kufuatilia mchakato wa kubadilisha majina makao makuu kwa maana kwa sasa nipo Dar es salaam?
Tangazo la gazeti la Serikali linatolewa na Ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, kwa Dar Es Salaam wako barabara ya Nyerere, ukiwasiliana nao watakujulisha taratibu za ofisi yao juu ya huduma unayoihitaji.
Iwapo umeshapata Kitambulisho cha Taifa, unaweza kubadili taarifa katika Ofisi yoyote ya Wilaya lah itakulazimu kufanyia Kilosa.
Shukrani kuwasiliana nasi.
Naomba kuuliza kwa mtu ambae alizaliwa mtaani hamjui baba na hakubahatika kusoma shule, na akaolewa na akahitaji atambukike kwa majina ya mume wake sehemu ya baba. Je kwenye sehemu ya baba anaweza kujaza jina la mume wake miaka na taarifa zingine?
Jina langu la Kati na la kwanza limekosewa nifanye nn
Mimi majina ya mama kwenye NIDA ni tofauti na cheti cha kuzaliwa kwani mama alibadilisha dini akabadilisha majina
Habari mm tarehe yangu ya kuzaliwa kwenye nkitambulisho cha NIDA ni03/06 na chet cha kuzaliw ni 06/03 ntabadili vip ikiwa tarehe yangu ni 06/03
Jamani mm nilijiandikisha lakin nida haijatoka tatizo Nini AALPHONCE DAMIANO KAHAVUYE mnisaidie
Samahani process zakubadili herufi za jina kwenye nida zinachukua mda gani kama umeisha kamilisha vitu vyote vya muhimu
Muda wowote ndani ya miezi mitatu pindi badiliko linapokamilika kufanyika. Shukrani.
Mi nashida mkuu ivi majina yaliyopo kwenye vitambulisho vyote ni sawa isipokuwa tu kwenye kitambulisho cha nida ndo hayafanani na yaliyoko kwenye vyet vingine kwenye vyet yanasomeka osca jackison sayon kwenye nida yanasomeka Oscar sayoni bugereka apa nafanyaje msaada please
Salaam Ndg. unashauriwa kuwasilisha cheti cha kuzaliwa chenye taarifa ya majina hitajika namna yanavyosomeka.
Maaboresho ya Jina nyaraka na mambo mengine muhimu ya kuzingatiwa.
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Samahani mi niliandikisha ila majina yangu tote yalikosewa ila taarifa zote zipo sahihi kasoro majina waliingiza ya mutu mwingine kabisa ila picha zote zangu na taarifa za mama na baba naweza kusaidiwa???
Salaam Ndg, kwa namana suala lako lilivyo, unashauriwa kufika ofisini kwanza uhakikiwe juu ya unachokieleza kisha utashauriwa nini cha kufanya. Shukrani.
Μy ѕpouse and I stumbled ⲟver here coming from a
different wеb address and thought І should check things out.
I like what I see so now i am following you. Lοok forward to looking at your web page rеpeatedly.
Thanks.
Habari za leo poleni na majukumu. Nilikua napenda kuuliza ni taratibu gani nifuate ili kurekebisha jina lililokosewa ki uandishi(typing error) mfano. SHEDRACK badala ya SHADRACK. Naomba isaidizi tafadhari..
Tafadhali unashauriwa kufika ofisi ya Usajili ya NIDA ili uhakikiwe unachokieleza, iwapo ndivyo, nyaraka ulizowasilisha awali wakati wa Usajili iwapo zinajitosheleza zitatumika kufanyia kazi ombi lako pamoja na kutakiwa kuwasilisha Hati ya kiapo ya badiliko la jina. Shukrani.
Hello.
Jina langu kwenye vyeti ni LUCIA PROTAS SHIRIMA.
Ila kwenye NIDA ni
LICIA PROTAS SHIRIMA.
Nitumie taratibu gani kubadilisha hilo jina la NIDA.. maana kuna “I” badala ya “U” inakuwa shida kuomba ajira za ualimu
Habari!
Jina langu ni HAMILTONI DAUDI EZEKIEL kwenye cheti changu cha kuzaliwa pamoja na vyeti vingine vya elimu ila changamoto ni kwenye kitambulisho cha NIDA inasomeka HAMILTON DAUDI EZEKIEL yaani “I” inatakiwa iondolewe Je? naweza tumia njia gani?
Njema
sijakuelewa, unataka I iondolewe wapi wakati kwenye kitambulisho cha NIDA haipo hiyo I. na kama ni hivyo vyeti vingine tafadhali wasiliana na Mamalaka zilizotoa vyeti hivyo.
Habari Mimi ningependa kusaidiwa juu ya tatizo la mwaka wangu wa kuzaliwa umekosewa kwenye kitambulisho badala ya 1997 imeandikwa 1992 lakin tarehe na mwezi vipo sawa kwaio mwaka upo tofauti na cheti changu Cha kuzaliwa naomba msaada juu ya hilo
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Habari,nahitaji kubadili jina langu la mwisho katika NIDA na jina hilo nililitumia Kama jina maarufu katika kujaza Taarifa za nida..je utaratibu ukoje?
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Habari za muda huu naombeni ufafanuzi kidogo naitwa PETRO EDWARD MEIGARU MOLLEL
lakini jina linalo onekana kwenye kitambilisho Cha mida ni PETRO EDWARD MOLLEL na vyeti vyangu vyote vya taaluma bima jina ninalo tumia kazi na hata lililopo kwenye payrol system ni PETRO EDWARD MEIGARU.jenifanyeje ili ni badili Hilo la ukoo like MEIGARU Jana nilikosa huduma kwa kadhia hiyo naombeni Cha kufanya .japo yote ni majina yangu sahihi kabisa
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Naomba kuuliza kuna garama za awali pale mtu anapotaka kujiandikisha kwa mara ya kwanza
Salaam Ndg. hakuna gharama za awali pale mwananchi anapohitaji huduma ya Utambulisho wa Taifa kwa mara ya kwanza isipokuwa kwa kundi la wageni wakaazi na wakimbizi. Shukrani.
Habari,
Kwa majina naitwa Lusiano Prosper Mfalingundi tunashukuru kwa ushirikiano wako Bwana Geofrey ila nina changamoto kama ifuatavyo apo mwanzo utaratibu wa kubadilisha jina na mwaka wa kuzaliwa niliupata kupitia hapa na nikafanya kama inavyostahili kwa kutafuta nyaraka zote zinazohitajika na nikafanikiwa kuzipata sasa kwenye ofisi za wilaya ukisema suala la kubadili mwaka wa kuzaliwa afisa usajili anajibu hapa hatufanyi na anakupa tu anuani ukaitume kwa Afisa usajiri makao makuu kwa EMS sasa ni miezi miwili sasa hakuna majibu na sijui nifanyaje na nashindwa elewa utaratibu huu ndio ulivyo au kuna namna nyingine maana maafisa wao wanasema hawawezi kutushughulikia na nikirejea unasema afisa usajili wa wilaya anatakiwa atume maombi yetu kwa njia ya barua pepe na wao wanatuambia tukatume kwa EMS hapa hatuelewi kaka
Je umepatiwa huduma ktika wilaya gani?
Naam kaka nimepatiwa huduma wilaya ya atusha
Wilaya ya Arusha kaka ndio nimepatiwa iyo huduma
Mimi Kitambulisho changu kimekosewa Mwaka Mimi nimezaliwa 28/06/1990 lakini nilivyopewa Kitambulisho kinasomeka nimezaliwa 28/06/1960 na nilishafuatilia mpaka kwenye ofisi za usajili wakacheki taarifa zangu wakaona ziko sahihi ila Kitambulisho nilichopewa Mwaka uko tofauti.
OMBI LA KUBORESHEWA TAARIFA
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Habari za muda huu mimi nahitaji kubadili jina langu moja lakwanza tu ndilo niliandikisha kimakosa taarifa nyingine zipo sahihi kabisa na cheti cha kuanzia darasa la saba kipo cha kidato cha nne kipo na hata cheti cha chuo pamoja na chakuzaliwa ninacho je naweza kusaidiwa?
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Viambatanisho kwaajili ya maboresho ya jina kwenye NIN ni cheti cha kuzaliwa, kadi ya kliniki, cheti cha kidato vmcha nne. Ni vyote au kimojawapo?
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Ukiwa navyo vyote ni vizuri zaidi.
Shukrani.
Habari inachukua mda gani majina kubadilika online na je nawezaje kujua majina yangu yamekwisha badilika?
Salaam Ndg. ombi la kubadili taarifa hupokelewa kwenye ofisi za Usajili wilayani na iwapo maombi ya mteja yamekidhi vigezo ndipo mabadiliko hufanyika. Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake, hivyo iwapo bado kupatiwa majibu yawezekana bado linafanyiwa kazi lah usichoke kuendelea kufuatilia ofisini kila baada ya muda kupita. Shukrani.
Salaam Ndg,
Kufahamu iwapo Maboresho ya taarifa yameshafanyika:-
Ingia kwenye uwanja wa kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms), kwenye simu yoyote ya kiganjani kisha andika jina lako la kwanza *jina la mwisho*tarehe mwezi mwaka wa kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama kama ulivyojaza kwenye fomu ya Usajili ya NIDA, kisha tuma kwenda na. 15096.
Mfano wa sms: Juma*Alli*02051995*Mariamu*Mwakabile (hakikisha unajaza taarifa kwa usahihi la hutopata jibu),
Tafadhali piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja Na: 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666,
Unaweza kutuma ombi lako https://demo.emalalamiko.egatest.go.tz/complaint ili kuangaliziwa moja kwa moja kwenye mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu
Ingia kwenye tovuti ya NIDA (www.nida.go.tz), fungua neno Kitambulisho cha Taifa kwenye menyu kuu kisha fuata maelekezo au fungua link -https://services.nida.go.tz/nidportal/get nin.aspx au
Fika kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA katika Wilaya iliyo karibu nawe.
Shukran.
Kwa wale ambao wako nje ya nchi mnashauriwa mara mtakapokuja nchini kufanya maombi ya utambulisho wa taifa na kuwasilisha maombi yenu yatashughulikiwa kwa haraka zaidi kwa nyie Diaspora
Habari Mimi nimelelewa na mama na nilisomeshwa na mama baada ya kujitambua niliamua kumtafta baba ambaye nilipewa maelezo kuwa ndiye baba yangu nilipompata kweli alinipokea lakini baada ya muda aliniambia kuwa yeye si baba yangu kipindi tunaandikisha vyeti vya kupigia kura niliandika ubini wake kitu ambacho kilipelekea na nida kujazwa hivyo sasa mazala yamekuja muda ambao nida ishatoka na ninahitaji kubadili ilo jina liwe LA kwenye chet cha kuzaliwa ambalo Lina ubini wa mama je itawezekana na kama itawezekana ni ghalama kiasi gani?
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Asantee mungu akubarik
Shukrani.
clomid uk cost
Salaam Ndg.
Karibu kwenye ukurasa wetu wa Tovuti wa NIDA tukuhudumie kwa kukupatia elimu juu ya Usajili na Utambuzi wa Watu ambao matokeo yake ni kutoa Utambulisho wa Taifa (NIN) na hatimaye Kitambulisho cha Taifa kwa raia, wageni na wakimbizi wanaoishi nchini kihalali wenye umri wa miaka 18 na zaidi. Shukrani.
seroquel tabs diflucan generic brand
Salaam Ndg.
Karibu kwenye ukurasa wetu wa Tovuti wa NIDA tukuhudumie kwa kukupatia elimu juu ya Usajili na Utambuzi wa Watu ambao matokeo yake ni kutoa Utambulisho wa Taifa (NIN) na hatimaye Kitambulisho cha Taifa kwa raia, wageni na wakimbizi wanaoishi nchini kihalali wenye umri wa miaka 18 na zaidi. Shukrani.
viagra without script

Mimi nilijisajili lakini kuna makosa yametokea kwenye jina la mwisho kuna herufi zimerukwa kwajiyo jina linasomeka tofauti na jina langu kwa herufi moja nifanyaje??
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Habar yako ndugu Geofrey,
Kwa majina ni Ramadhani saidi Ramadhani, nilifanya taratibu za kubadili jina langu la mwsh kwenye Nida yangu Ambalo linasomeka,, Ramadhani saidi mwambashi instead of Ramadhani saidi Ramadhani, nashukuru nimefanya hatua zaidi ya kuikamilisha nimepita mpka kwa mkuu wa mkoa nimeshalipia kila kitu,, sas nimefika ofc Za Nida Tanga wamenitaka ni tangaze kwenye Gazeti la serikali kwamba natumia jina la Ramadhani saidi Ramadhani instead of Ramadhani saidi mwambashi, je kuna haja kwely ndugu yangu kubadili jina tu ambalo ni la ukoo, na mimi sio mtumishi nitangaze kwenye Gazeti la serikali Na likae mwezi mzima
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Jamani Mimi pia majina yangu yalikosewa yaani jina la kati na la mwisho badala ya Ng’oko paschal kanyelema )yakawa hivi Ng’oko kanyelema paschal napatata changamoto sana nifanyeje?
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Tafadhali inachukua mda gani kwa majina kuweza kubadilishwa?
Salaam Ndg. ombi la kubadili taarifa hupokelewa kwenye ofisi za Usajili wilayani na iwapo maombi ya mteja yamekidhi vigezo ndipo mabadiliko hufanyika. Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake, hivyo iwapo bado kupatiwa majibu yawezekana bado linafanyiwa kazi lah usichoke kuendelea kufuatilia kila baada ya muda kupita. Shukrani.
Habar ndugu shida yangu jina herufi moja ya jina la katikati imekosewa je nifanyeje ili niweze kubadilisha
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Nida mnasema mtu akibadili umri anatakiwa atumie namba ilele ya. mwanzo kuwa taarifa hazibadiliki zinabadilika kwenye mfumo tu,sasa hapo atatumiaje namba ilele wakati kwenye vyeti ni tofauti na hataonekanaje kuwa mkweli wakati taarifa ni tofauti ndugu maelezo tafadhari.
Salaam Ndg. kimsingi kila namba kwenye NIN ina maana, na inapaswa kufahamika ama kutafsiriwa zaidi na NIDA na si mteja ama mdau. kinachopaswa kuangaliwa ni taarifa zinavyosomeka kwenye mfumo na si vinginevyo. Shukrani.
Habari, nilitaka kujua je itawezekana kitambulisho cha NIDA kiwe na majina mawili tu yaani mfano EMIL FRANCIS badala ya EMIL FRANCIS KIPOSI? Kama ndiyo, taratibu zikoje?
Salaam Ndg. kwa utaratibu uliopo sasa, hapana haiwezekani kwa usajili wa raia isipokuwa kwa wageni wakaazi. Shukrani.
samahan naomba kuuliza mimi cheti changu cha kuzaliwa kimetofautiana majina na cheti cha shule cheti cha kuzaliwa kinasomeka kama joseph malila ila shule mzee wangu alikataa akasema litumike jina la ukoo ambapo nilitumia malila kitako ila kwa sasa nahitaji kubadiri jina la vyeti vyangu vya shule visomeke kama nida yangu inavosomeka.samahani inawezekana? naomba muongozo
Wanaohusika na kubadili taarifa za vyeti vya shule ni taasisi husika na ulikopatia elimu.mabaraza na wizara husika. unashauriwa kuwasiliana nao kupata msaada na mwongozo zaidi, Shukrani.
Naitwa Irene Audax
Samahani nilikabidhi nakala zote zilizokuwa zinahitajika kubadili majina,naomba kufahamishwa nitajuaje kama yamebadilishwa tayari iwapo sina urahisi wa kufika ofisi za nida?
Salaam Ndg. Tafadhali piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja Na:- 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666,
Ingia kwenye tovuti ya NIDA (www.nida.go.tz), fungua neno Kitambulisho cha Taifa kwenye menyu kuu kisha fuata maelekezo au fungua kiunganishi (link) -https://services.nida.go.tz/nidportal/get nin.aspx. Shukrani.
Jina langu la mwisho limekosewa limeandikwa mabinya badala ya mabihya…
Je wanaweza kufanya marekebisho
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Naomba tarehe yangu ya kuzaliwa wamekosea badala ya tarehe 26/06/1986.saiv inasomeka 006/06/1986…

Naomba msaada tarehe yangu ya kuzaliwa wamekosea badala ya tarehe 26/06/1986.saiv inasomeka 06/06/1986…
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
lyrica 300 mg
Habari, nimesoma maelekezo, Jina langu la kwanza lilikosewa/halikujazwa kwenye kanzi data kiusahihi, Nilijiandikishaga Arusha, lakini kwa sasa nipo mkoa mwingine, je, ninatakiwa kwenda ofisi za Arusha au hata za huu mkoa wa sasa nitasaidika?
Salaam Ndg. unaweza kusaidika kwa sehemu kwa maana ya kuhakikiwa na kushauriwa zaidi vya kujiandaa navyo. iwapo umeshapatiwa Kitambulisho cha Taifa, unaweza kuboresha taarifa zako katika ofisi yoyote ya Usajili lah utapaswa kuripoti Arusha. Shukrani.
Samahani naomba kujua Hilo tangazo la serikali linapatikana wapi? Ni makao makuu dar es salaam au naweza nikalipata kwa mtandao? Màana kiufupi tu sijaelewa maana yake ,na swali jingine hiyo deepol inaweza patikana kwa mwanasheria yeyote? Au mpk ofisi za ardhi?
Ndg. Gazeti la Serikali linapatikana kwenye ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dodoma na Dar pia wana ofisi. Deedpol inapatikana Wizara ya Ardhi ama kwa mawakala wao ambao wako katika mikoa yote nchini. Shukrani
Salaam Ndg. Gazeti la Serikali unashauriwa kufika kwenye ofisi ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, ofisi ziko Dodoma na Dar Es Salaam. Kuhusiana na Deedpol, Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi wana ofisi katika mikoa yote nchini. Kupata taarifa zaidi unashauriwa kuwasiliana na wahusika. Shukrani
Naombeni Msaada nilifanikiwa kupata namba yangu ya NIDA ila baada ya mda niligundua kuwa taarifa za mwaka wangu wa kuzaliwa zimekosewa na nilipeleka cheti cha kuzaliwa wakati wa usajili , na sasa nataka nirekebishe naombeni utaratibu nafanyaje fanyaje??
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Habari nilikuwa na shida ya kubadili taarifa kipengele cha mwaka hatua ni zip maana kila NIDA nayoenda wananielekza tofauti
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa ombi litashughulikiwa kwa utaratibu hapo chini pamoja na kutakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya Kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Usajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na Afisa Usajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
viii. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Shukrani.
Helo habari
Mimi naitwa Joyce nnipo Arusha, nina shida ya kubadilishwa jinna na tayari nmekamilisha kila kitu isipokua tangazo kwenye gazeti la serekali,kuna no nilipewa kwaajili ya kupata contol namba Ila haipokelewi kabisa nikipigga ni mwezi mmoja Sasa nammba yenuewe ni0718847730
Salaam Ndg. Pole kwa usumbufu uliojitokeza. unashauriwa kuipakua Namba ya Malipo ya Serikali kupitia huduma ya jihudumie(self service) kupitia Tovuti yetu – http://www.nida.go.tz. Shukrani na pole kwa usumbufu uliokutana nao.
Kwa majina naitwa SHABANI BIKIZ KOMBO (Academic certificates) ,Kwenye NIDA Ni SHABANI KOMBO BIKIZ ,nimefanya mchakato mzima wakubadilisha ilo jina lifanane na vyeti vyangu vya taauluma ikiwemo deed poll ,gazeti la serikali, na vyeti vyote ikiwemo chakuzaliwa ,pamoja nakulipa sh 20,000 lakini yaelekea mwezi sasa,je yachukua mda gani kubadilisha kwa jina hilo
Salaam Ndg. ombi la kubadili taarifa hupokelewa kwenye ofisi za Usajili wilayani na iwapo maombi ya mteja yamekidhi vigezo ndipo mabadiliko hufanyika. Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake, hivyo iwapo bado kupatiwa majibu yawezekana bado linafanyiwa kazi lah usichoke kuendelea kufuatilia kila baada ya muda kupita. Shukrani.
Kwa majina naitwa SHABANI BIKIZ KOMBO (academic certificates) Kwenye NIDA jina ni SHABANI KOMBO BIKIZ, nimefanya mchakato mzima wakubadilisha ilo jina lifanane na vyeti vyangu ikiwemo deed poll, Gazeti la serikali na vyeti vyangu vyote ikiwemo chakuzaliwa pamoja nakulipa sh 20000, inachukua mda gani kubadilishika ikiwa yaelekea mwezi sasa
Salaam Ndg. ombi la kubadili taarifa hupokelewa kwenye ofisi za Usajili wilayani na iwapo maombi ya mteja yamekidhi vigezo ndipo mabadiliko hufanyika. Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake, hivyo iwapo bado kupatiwa majibu yawezekana bado linafanyiwa kazi lah usichoke kuendelea kufuatilia kila baada ya muda kupita. Shukrani.
Habari Ndugu!! Naweza sema finally done..ila process ni ndefu angalieni namna nyingine,maana kuna sehemu ofisi za mpiga chapa wa serikali hamna ,na sehemu zingine Ni mbali mno
habari ndugu, naitwa wilson isack mtua nilikuwa naomba kufahamu jinsi na njia ya kupata na kulipokea gazeti kutoka kwa mchapa mkuu wa serikali
Salaam Ndg. Unashauriwa kuwasiliana na Ofisi husika ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali. Shukrani.
Habari, mimi na shida ya majina
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Habari naitwa michael nilikosea kujaza taarifa ya tarehe ya kuzaliwa je inawezekana kufanyiwa marekebisho
Salaam Ndg. Tafadhali fika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi. Huduma ya kuboresha taarifa za mwombaji hufanyika ofisini na si kwa njia ya mtandao kwani mteja anahitajika kwa mahojiano zaidi na uhakiki wa nyaraka kujiridhisha juu ya ombi hilo.
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Kabla ya kufanya malipo ya huduma na utekelezaji wa hatua yoyote, unashauriwa kufika ofisini kwanza kupatiwa kibali cha kuendelea na malipo.
Shukrani.
Habari, mimi na shida ya jina. Nataka kubadili jina la mwisho la kwenye Nida ili lisomeke sawa na kwenye vyeti vya shule. Na majina hayo yote yapo kwenye cheti cha kuzaliwa ila tu lililopo kwenye Nida la mwisho halipo kwenye vyeti vya shule na mimi nataka lililopo kwenye vyeti vya shule liwepo kwenye Nida. Je hapo ni lazima nije na deed poll au Affidarvit. Kwasababu mimi sikatai jina ila nataka la kwenye vyeti vya shule lisomeke hivyo hivyo kwenye Nida.
lopressor 10 mg
Nilifanya mabadiliko kwenye Taarifa za nida.. inachukua mda gani kuwa tayari kwa taarifa kufanyiwa kazii
Salaam Ndg. Ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake hivyo linaweza kukubaliwa ama lah hivyo ni ngumu kukupatia muda halisi kwani uhakiki unategemea na asili na yaraka mtu alizowasilisha dhidi ya ombi lake. Shukrani.
Habari yako ,,,
Mimi namaombi jaman nliandika jina lingine na ya baba mwingine yan majina yote matatu ambayo nmesajili nida ni tofauti na ambayo yapo kweny vyeti vyangu vyote vya shule sa nifanyeje jmn nshahangaika sana bila mafanikio
Salaam Ndg. Hakuna utaratibu wa kubadili majina yote na hasa kama hakuna nyaraka za rejea. Shukrani.
Hakuna huo utaratibu kwani serikali inafanya kazi kimaandishi na si kwa rejea ya maelezo ya mdomo pekee. Shukrani.
Nahitaji kubadili namba ya simu(kwa kua OTP hua zinatumwa kwenye namba ya simu inayotumiwa na mtu mwingine) na sahihi yangu (kwa kua inanisumbua kuirudia hasa nikiwa bank)
Salaam Ndg. Unashauriwa kuripoti suala lako ofisini kwa msaada zaidi. Shukrani.
Kaka nataka nibadili Jina ila viambatanisho Sina hata kimoja kama cheti cha kuzaliwa,vyeti vya shule pia Sina. Nifanyeje kaka
Salaam Ndg. ili ufanikishe jitahidi kuzingatia vigezo na masharti. Shukrani.
Nida yangu Ina majina manne nataka kufuta moja la mwisho ili liendane na vyeti vya elimu je baada ya kukamilisha taarifa zote zinazohitajika kunachukua muda gani kufutwa?
Salaam Ndg. inategemea kwani ombi lako linaweza kukubaliwa ama kutokubaliwa. Shukrani.
Boss naomba kuuliza ni vitu gani vya kuambatanisha ili uweze kubadilishiwa majina ya nida
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Mm majina yangu hayafanani na ya kwenye vyeti naomba msaada
Salaam Ndg. Unashauriwa kuripoti kwenye Ofisi ya Usajili Wilayani kwa uhakiki na msaada zaidi. Shukrani.
Mm nashida nahtaj kubadili majina matatu nafanyaje
S
Salaam Ndg. Hakuna utaratibu wa kubadili MAJINAatatu isipokuwa hilo linaweza fanyika iwapo nyaraka zako Zilizopatikana awali na wazazi au kabla ya Kusajiliwa NIDA Zina taarifa hizo. Shukrani.
Mm shida yangu ni majina yapo tofauti na vyeti vyangu naomba msaada pia majina niliyoandikisha sikuelimishwa vzr maana hata cheti cha kuzaliwa,cha la saba,na kidato cha nne skuombwa kuambatanisha
Salaam Ndg. Viambatisho vimeorodheshwa kwenye fomu ya Usajili hata cheti Cha kidato Cha nne hivyo ni WAJIBU wako kuambatisha. Kuhusu kubadili Taarifa unashauriwa kuripoti kwenye Ofisi ya Usajili Wilayani kwa uhakiki juu ya unachokisema kwa wao kuangalia taarifa kwenye mfumo Kisha utashauriwa unachopaswa kufanya. Shukrani.
je kiapo cha mwanasheria kinapokelewa kuhusu kubadili taarifa kama jina la mwanzo na mwaka wa kuzaliwa ?
Salaam Ndg. Hapana
Habari mr Geofrey, kwa majina naitwa Juma shabani,changamoto yangu ni moja tu tarehe ya kuzaliwa kwa maana ya siku ikisomeka 02.03.2000 kwenye NIDA yangu badala ya kusomeka 01.03.2000 kama ilivyo kwenye vyeti vyangu je kuna haja yoyote ya kubadili tarehe na kama kuna haja ni procedures zipi natakiwa kufuata ili kuondoa changamoto hiyo.
Salaam Ndg. Unashauriwa kuripoti Ofisini kuwasilisha ombi lako. Iwapo kuna nyaràka ipo NIDA yenye taarifa ya tarehe unayoitaka kubadilishwa, zoezi no rahisi zaidi. Itatumika nyaraka hiyo kurekebisha taarifa hiyo pamoja na nyingine utakazoelezwa iwapo zitahitajika pia. Shukrani.
Samahani msaada, Mwanzo nilijisajili kwa majina yaliyokuwa kwenye kitambulisho Cha mpiga kula Cha zamani kwa majina: Simion mniko kitarisya na badae kubadili majina kwenye kitambulisho kipya na kusomeka marwa moseti Simion ntafanyaje kuyatumia haya majina mapya
Salaam Ndg. Unapaswa kuripoti Ofisi ya Usajili ya NIDA wilayani, hakikosha unafika na nyaraka zenye MAJINA unayohitaji yasomeke kwa Sasa. Nyaraka hizo ziwe zilizotafutwa na wazazi awali kama kadi ya kliniki, Tangazo, cheti Cha darasa la vii, ubatizo, falaki ama “leaving certificate” ya kidato cha iv. Wakisha hakiko mahitaji mengine zaidi watakueleza iwapo wataona umekodhi vigezo vya kuendelea mbele zaidi. Shukrani.
Kwema kiongozi,Jina langu ni majura marumbo Hassan Lakin Jina lililotokea kwenye kitambulisho ni majura makongoro marumbo, na makongoro ni Jina la ukoo upande wa mama naomba Kujua itachukua mda gan kubadilisha ili Jina?, na vigezo gan vnaitajika?
Salaam Ndg. Muda ni wakati wowote ombi lako litakapoonekana kukidhi vigezo. Fika Ofisini kwanza kwa uhakiki na andaa nyaraka zilizotafutwa na wazazi awali kama vile cheti cha kuzaliwa, darasa la vii, ubatizo, falaki, kadi ya kliniki na leaving certificate. Nyaraka zingine vyema kufuatilia baada ya kuhakikiwa na kuruhusiwa kuanza na taratibu kama vile deed poll na Tangazo la gazeti la Serikali. Shukrani.
Habari za asubuhi nilikosea kujaza fomu ya nida nikajaza nimezaliwa 2000 badala yà 2001 nisaidie hatua zipi ninatakiw nizifuate nibadili?
Salaam Ndg. Ni vizuri kuripoti kwanza kwenye Ofisi ya Usajili Wilayani kwa uhakiki Ili kujua kama viambatisho ulivyowasilisha awali vinatosheleza kutumika kuboresha taarifa zako ama utalazimika kuongeza vingine. Shukrani.
Nimetuma barua mbili kwa mkurugenzi mkuu kuomba kubadilisha majina mawili lkn mpaka sasa sjajibiwa. Naomba kujua ni msaada gani zaidi naweza kupata kwani km mtanzania nashindwa kufanya kazi yoyote ya kuajiriwa bila namba ya NIDA.
Habari za muda huu , ninachangamoti ya kukosejana jwa herufi moja kwenye kitambulisho na nupo mbali na ofisi niliyo katia NIDA je naweza kufanya marekebisho kwenye ofisi ya mkoa mwengine
Salaam Ndg. Rekebisho hilo dogo linawezekana kama ulivyouliza. Shukrani.
Unaweza kubadirisha taarifa zako wilaya tofauti na uliyojiandikishia
Salaam Ndg. Iwapo umeshapatiwa Kitambulisho cha Taifa, iwapo bado unalazimika kufika kwenye ofisi ya Usajili katika wilaya ulikosajilia. Shukrani.
NILIPATA CHANGAMOTO YA KATIKA KADI YA MPIGA KULA WALIKOSEA MWAKA WA KUZALIWA NA WAKATI WA KUANDIKISHA NIDA NA LESENI YA GARI MIAKA IMEKOSEWA VILEVILE HII IMEKUJA MPAKA KWENYE NIDA NIFANYE NINI ILI KUBADILISHA MWAKA WA KUZALIWA ILI UFANANE NA MIAKA YA KWENYE VYETI VYANGU VYA MASOMO?
Habari kwajina naitwa Hadija Ramadhani Jumbe nipo Dar es salaam naomba kujua ofisi
za NIDA zipo wapi ili niweze kuwasilisha nyaraka zangu za kubadilisha jina
Naomba kuuliza majibu ya barua ya Maombi ya marekebisho kwenye namba ya NIDA 20000402333040000120 kipengele cha mwaka
Barua nmeileta NIDA HQ apo ubalozini toka 26/10/2022.
Ningeomba kuwepo na taarifa kama maombi yakikubalika au ya kikataliwa au nini kimekosekana muda unaenda na taarifa nyingi zinazidi kutofautiana unapo attach KITAMBULISHO KINGINE NA NAMBA YA NIDA
Mm naitwa EMMANUEL VICTOR MPELWA Jana nimeenda kwenye ofisi za nida nzega Tabora kuweza kupata kitambulisho changu Cha nida lakini sikupata nikataka kuabdilisha taarifa zangu za awali ili niweze kufanya maombi ya kazi jamn mm mnanisaidiaje nida nimejiandikisha victor Emmanuel Robert na mm natakiwa niwe EMMANUEL VICTOR MPELWA naomba msaada wenu jamn naumia sana kukosa huduma
Naitwa EMMANUEL VICTOR MPELWA ndio jina langu linalotakiwa kusomeka mpka kwenye vyeti vyangu vyote lakini kwenye nida linasomeka victor Emmanuel Robert nahitaji kubadilisha ,je nifanye nini maana nimeenda kwenda kwenye ofisi za nida wanasema haiwezekani kubadili je mamlaka naomba msaada wenu jamn
Samahani naomba kuuliza ukimaliza taratibu zote za ubadilishaji wa jina,jina hilo linachukuwa mda gani kubadilika?. mwezi au wiki msahada wa swari hilo tafadhali
Salaam Ndg. ombi linaweza kamilika kwa muda wa kuanzia mwezi na zaidi. Shukrani.
Naomba kubadilisha jina lakini sioni majibu
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Mkuu mimi ukoo wetu tunatofautiana majina hasa jina la mwisho wanaume wanajilao pia wanawake tunajina letu mfano kama kwa muheshimiwa jokate. Nilipoomba kitambulisho nida nilijaza majina nayotimia kwa usahii ila yamekuja tofauti nimewekewa jina la mwisho la baba ambalo ssisi wanawake hatutumii na halipo kwenye vyeti vyangu vyote unanisaidoaje kubadisha
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Habari..
Nimejibiwa na ofisi ya mkurugenzi kuwa ombi langu la kubadili majina mawili la kati na la mwisho ambayo ni ya kwangu yote lakini hayaendani na yale niliyotumia shuleni haliwezi kutekelezwa.Hivyo naomba kufahamu ni nini natakiwa kufanya mm km mtanzania wa kawaida ambae mpk sasa nimeshindwa kuomba ajira yoyote kutokana na kutokuwepo kwa mfanano wa majina yangu na ukizingatia ukomo wa vitambulisho vya taifa umeondolewa
Niliandikisha nida toka mwezi wa Kwanza mpaka leo haijatoka na nida inahitajika kwa haraka nifanyeje mm kama kna uwezekano wa kufuta taarifa niandikishe upya nisaidieni
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Niliandikisha nida toka mwezi wa Kwanza mpaka leo haijatoka na nida inahitajika kwa haraka nifanyeje mm kama kna uwezekano wa kufuta taarifa niandikishe upya nisaidieni maana nimeenda wilayani nilipo jiandikishia wamesema wao hawawezi kfuta hadi makao makuu maana washatuma taarifa nisaidieni
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Niliandikisha kwa kutumia kadi ya mpiga kura Naya imekosewa herufi imeandikwa shija Marco masaru baadara ya shija Marco masalu naombeni mnifutie taarifa niandikishe upya maana nateseka frusa za kazi zikitoka nashindwa kutuma maombi kwa sababu cina namba ya nida nawaomba sana mnisaidie wazazi wamenisomesha wananitegemea Sana siku moja niwasaidie naomba msaada kwenu sana
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Niliandikisha mwanza wilaya ya nyamagana kwa ktumia namba ya simu 0627923993
Salaam Ndg.
Karibu tukuhudumie!
Shukrani.
Naomba kujua je kuna madhara ya herufi kwenye jina lililopo Nida na vyeti vingine
Mfano vyeti vyangu vimeandikwa HALIMA MASUDI KIDAYA ila kwenye NIDA wameandika HASLIMA MASUDI KIDAYA.
Japokua taarifa zingine ziko sahihi
Na ninataka ku apply ajira naogopa je itakua na madhara katika kupata ajira.
Naomba msaada wenu tafadhali
Salaam Ndg. Ndiyo.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake,
Nahitaji kubadilisha jina la mwanzo ambalo ni victor Emmanuel Robert ndio nida iñavyosomeka lakini majina yangu kamili ni EMMANUEL VICTOR MPELWA ndio ninayohitaji kwenye nida yangu nifanyaje ili niweze kupata huduma 19961012454380000126 ndio nida yangu
Kusitisha huduma nilizo jiandikishia nifanyeje maana nilipo jiandikishia wamesema washazituma makao makuu nataka niandikishe upya maana niliandikisha mwezi wa Kwanza had leo hii haijatoka nataka ktumia cheti cha kuzaliwa na cha form form mwanzo nilitumia kadi ya mpiga kuraafu kimekosewa herufi
habari naitwa Miriam mwakifuna nataka kujua ni kwa namna gani naweza pata taarifa zilizoambatana na namba yangu ya NIDA maana imetokea naomba kazi ila taarifa zangu za nida nnazoingiza zinagoma na ni vitu ambavyo sio vya mtu kusahau kama majina ya mama ,bikini cha makazi ya kudumu na taarifa nyingine za kawaida kabisa ila inasema nmekosea wakat zilo sahihi
Salaam Ndg.
Unashauriwa kuwasilisha ombi lako kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi.
Shukrani.
Naitwa Sula Mabula ninahitaji kubadlisha majina mawili ya Paulo Yusuph Kama lilivyotumika kwenye kitambulisho cha taifa na kuwa Sula Mabula Sinzi nifanyeje ili kuweza kuomba kazi 19911026331040000125
Habari, Samahani nilikua nauliza Utaribu wa kubadili Taarifa za NIDA upande wa Eneo ulilozaliwa, kwa maana wakati najaza Taarifa za NIDA nilikosea kuandika Mahali sehemu Ya kuzaliwa Badala ya kuandika Nimezaliwa Wilaya ya Nyagamagana nikaandika wilaya Ilemela na Hii ndo sehemu ninayoishi napenda kujua jinsi ya kufanya , na Gharama yake Ni Kiasi Gani?, au Ni bure , Utaratibu Tafadhari ili Taarifa zangu ziwe sawa Na zifanane na Nyaraka zingine. Mfano ukieenda Bank wakiprinti Inaleta Nimezaliwa Ilemela, huku Nimezaliwa
Salaam Ndg.
Kuna taarifa kama za mahali pa kuzaliwa huwa hatubadilishi lah kuna vithibitisho toshelezi.
Shukrani.
Habari, Samahani nilikua nauliza Utaribu wa kubadili Taarifa za NIDA upande wa Eneo ulilozaliwa, kwa maana wakati najaza Taarifa za NIDA nilikosea kuandika Mahali sehemu Ya kuzaliwa Badala ya kuandika Nimezaliwa Wilaya ya Nyagamagana nikaandika wilaya Ilemela na Hii ndo sehemu ninayoishi napenda kujua jinsi ya kufanya , na Gharama yake Ni Kiasi Gani?, au Ni bure , Utaratibu Tafadhari ili Taarifa zangu ziwe sawa Na zifanane na Nyaraka zingine. Mfano ukieenda Bank wakiprinti Inaleta Nimezaliwa Ilemela, huku Nimezaliwa Nyamagana.
Salaam Ndg.
Kuna taarifa kama za mahali pa kuzaliwa huwa hatubadilishi lah kuna vithibitisho toshelezi.
Shukrani.
habari, nauliza jinsi ya kubadili wilaya ya kuzaliwa, kwa maana wakati najaza nilikosea kuandika wilaya badala ya kuandika Nyamagana nikaandika Ilemela sehemu ninanyoishi, imekua inaniasiri sana kwa taarifa zangu zinakua tofauti kwenye nida na kwenye cheti cha kuzaliwa, na Gharama ni kiasi gani? pia nafanyeje ili nibadilishe asante
Salaam Ndg. Ronald,
Taarifa za mahali ulipozaliwa huwa hazibadilishwi lah una nyaraka ya kuthibitisha hilo iwasilishe kwenye ofisi ya Usajili.
Shukrani.
Mm imekosewa herufii moja kwenyejina langu na namba nimepata sina hata mwezii je nitaratibu zipi natakiwa kuzifata ili nirekebishe??
Salaam Ndg.
Unashauriwa kuripoti kwenye ofisi ya Usajili katika wilaya ulikosajiliwa kufanya marekebisho ya herufi husika. fika na cheti cha kuzaliwa n.k
Shukrani.
Mimi nina shda ya tarehe ya cheti changu cha kuzaliwa na namba ya nida ziko tofauti
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya tarehe/mwezi wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha tarehe/mwezi wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Iwapo nyaraka hitajika ulishawasilisha awali na ziko kwenye mfumo wa Utambuzi wa Watu wa NIDA, Afisa Usajili atafanya uhakiki kupitia taarifa ulizowasilisha awali zenye tarehe na mwezi unaohitaji usomeke.
vii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika.
ix. Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho baada ya mwombaji kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake.
Habari ninaitwa Regan Temba Niko Arusha Tanzania Nina shida na kitambulisho changu Cha nida kilikosewa taarifa moja ya jinsia badala niandikewe mwanaume nimeandikwa Mwanamke.. Sasa nafanyaje maana hiyo taarifa haifanani na taarifa zangu nyingine..
Mimi anita ally abasi naomba kubadilixha tarehe, mwezi n mwaka nafanyje ili niweze badilixhiwa
Salaam Ndg.
Maaboresho ya tareh/mwezi au Mwaka wa kuzaliwa:-
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya mwaka wa kuzaliwa unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, kilichotafutwa na wazazi awali,
cheti cha darasa la saba, kidato cha iv ama ‘ leaving Certificate
Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi na Afisa Usajili wilaya.
iwapo itaonekana kukidhi vigezo baada ya kuwasilisha nyaraka hitajika kwa Afisa Usajili, utapatiwa namba ya malipo ya serikali (Controll Number) na utapaswa kulipia shilingi 20,000/= ikiwa ni gharama kwa ajili ya kufanya maboresho hayo.
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa za tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa anapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo:
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi na chenye mabadiliko ya sasa, ambapo NIDA tutajiridhisha mabadiliko hayo kupitia RITA.
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa za mabadiliko husika.
vi. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vii. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
viii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa iwapo nyaraka tajwa hazijaambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
Nataka nisitishe tarifa zangu nifanyeje maana niliandikisha nida haikutoka nifanyje mm msaada jameni
Habari,
Karibu NIDA tukuhudumie.
Asante.
Nataka kujua inatumia muda gani kuweza kufanyika marekebisho ya jina kwenye kitambulisho cha nida maana imepita miezi miwili Kila nikenda naambiwa Bado approve
Habari,
Tafadhali tutumie taarifa zako na nyaraka zako zote kwenye email yetu ya info@nida.go.tz
Asante.
Nataka kujua inatumia muda gani kuweza kufanyika marekebisho ya jina kwenye kitambulisho cha nida maana imepita miezi minne(4) sasa Kila nikenda naambiwa Bado approve
Nataka kujua inatumia muda gani marekebisho ya jina kwenye kitambulisho cha nida kufanyika maana imepita miezi minne(4) sasa Kila nikenda naambiwa Bado approve
Habari,
Tafadhali tutumie nyaraka zako zote za maombi kwenye email yetu ya info@nida.go.tz
Asante.
Habari naitwa said kadonya martine, napenda kuuliza naweza lubadilisha mwaka wa kuzaliwa kwenye namba ya nida ofisi zozote za nida au hadi niende ofisi nilizojiandikishia. Asante
Hallo fuata maelekezo uliyopewa kwenye email.
modafinil price comparison
where can i buy elimite
albuterol over the counter usa
price of augmentin 375 mg
Poleni na majukumu pia poleni na kazi ya ujenzi wa Taifa mimi naitwa Noel mkanga kutoka mkoa wa njombe niliwasilisha maombi ya kubadilisha jina la kati kwenye nida ili liendane na vyeti vya chuo, nida inasoma NOEL RICHARD MKANGA lakini kwenye kwenye vyeti vya chuo na kuzaliwa ni NOEL KITA MKANGA na aliyeniandikisha Malawi alitumia NOEL KITA MKANGA leaving certificate hatukupewa cheti cha la Saba kilipotea naombeni msaada wenu Ili niweze kupata ajira za ualimu
Wenu katika ujenzi wa Taifa
Tafadhali fuatilia kwenye ofisi ambayo uliwasilisha maombi yako kupata mrejesho
naitwa mathew peter geay ila kwenye nida inasoma mathew peter geayi nataka kurekebisha herufi tu ili ifanane na vyeti vyangu vya shule
Tafadhali fika ofisi yoyote ya NIDA kwa maelekezo na usaidizi zaidi
Kwa majina naitwa Boniface mgeko mkenge lakini kwenye taarifa zangu za nida jina linasomeka BINIFACE badala ya BONIFACE.naomba msaada wenu .haya makosa yalifanyika na afsa nida wilaya katika kujaza taarifa zangu
Tembelea Ofisi ya NIDA kwa Maelekezo na utaratibu wa kubadilisha jina
Mm ni mtumishi naanzaje mchakato au ni viambata vipi vinahitajika Kwa karibu mkuu utumishi
Samahani unataka huduma gani?
Habari iwapo IIwapo nimeandikisha Nida kwa majina mengine tofauti na majina niliyoyatumia kwenye vyeti vyangu vya taaluma,Mamlaka ya taaluma inanihitaji niwe na majina halisi ya kwenye cheti cha kuzaliwa yafanane ja ya kwenye Nida je naweza kupata msaada wa kubadilisha?
Unaweza kubadilisha. Tafadhali fika ofisi ya NIDA kwa maelekezo na utartaibu wa kubadilisha taarifa
Samahani, Taratibu gani nizifuate ili nibadili tarehe ya kuzaliwa?
Andika barua kuomba mabadiliko hayo ukieleza na sababu kwa nini ubadilishiwe pamoja na kuweka viambatisho vya nyaraka zinazosupport mabadiliko hayo unayooomba
Habari, Je naweza kufanya mabadiliko ya namba taarifa za jina kwenye NIDA, kutoka kutumia majina matatu hadi kuwa majina mawili ili yalingane na majina ya kwenye vyeti vya elimu??
Kaongeze kwenye cheti, NIDA lazima yawe matatu
Salaam Ndg.
Usajili wa NIDA kwa raia unamhitaji kuandika majina matatu
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake.
Habari kiongozi
Nam mim nina tatizo la mwaka KATIKA NIDA yangu .JEE kuna uwezekano WA KUFANYA marekebishoo na hali yakuwa Tayar kitambulisho kimeshatoka.Bimaana kwenye cheti changu Cha kuzaliwa ni tar 7/12/2002 LAKINI kwenye NIDA kuna 7/11/2001.Naniliebda NILIPO jisajili nikaambiwa haiwezekani sasa NAOMBA msaada JUU ya hilo.
Unajua tunaamini mtu hazaliwi mara mbili, hata hivyo andika barua kuomba kufanyiwa hayo mabadiliko ukieleza sababu pamoja na kuambatisha nyaraka zinazothibitisha hayo maombi yako utajibiwa
Kubadili jina na mwaka
Mwombaji anayehitaji kuboreshewa taarifa ya mwaka wa kuzaliwa ombi litashughulikiwa kwa utaratibu hapo chini pamoja na kutakiwa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya NIDA ya Usajili ya Wilaya:-
i. Cheti cha kuzaliwa kilichopatikana awali na wazazi/walezi
ii. Cheti cha kumaliza shule ya msingi,
iii. Kadi ya Kliniki,
iv. Cheti cha kumaliza shule za sekondari (Leaving Certificate),
v. Nyaraka yoyote ya awali yenye kuthibitisha mwaka wa kuzaliwa kabla ya kusajiliwa NIDA.
vi. Ombi la mteja litawasilishwa kwenye kamati ya Usajili na Utambuzi wa watu, iwapo watajiridhisha kuwa ombi limekidhi vigezo ndipo watatoa kibali ili Afisa Msajili aweze kuendelea na hatua ya kufanya maboresho, ombi lisipokidhi vigezo, kibali hakitatolewa na
vii. Afisa Msajili hatoweza kuendelea na hatua yoyote ya maboresho.
viii. Mteja unaombwa kutoa ushirikiano kwani ombi halitakiwi kupokelewa na Afisa Usajili iwapo nyaraka tajwa hazija ambatishwa/kukamilika kwa Idadi tajwa.
ix. Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi na Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika ya jina lako
Shukrani.
Naomba kubadilisha majina yangu Jina Emmanuel saipi Hokore ndio limekosewa kwahyo naomba iondolewe Jina Emmanuel
Ibaki haya majina Sangwa Saipi Hokore
Nenda kwenye Ofisi ya NIDA kupata utaratibu wa kubadilisha taarifa
Salam ndugu yangu habari za mda huuu pole na majukumu naomba msaada ya mabadiliko ya majina yangu ambae Jina la mwanzo sio sahihi ni tofauti na majina mengine yalioko kwenye cheti Cha kuzaliwa na kuanzia shule ya msingi Hadi chuoni
Majina yalio kosewa ni Emmanuel saipi Hokore
Jina Emmanuel liondolewe ili ibaki sangwa saipi Hokore
Namba ya NIDA 19931212276070000125
Tafadhali fika Ofisi yoyote ya NIDA kwa maelekezo na usaidizi zaidi
Habari nawezaje kupata taarifa za mzazi nilizo andika nida
Tafadhali fika Ofisi yoyote ya NIDA kwa usaidizi zaidi
Salaam Ndg.
Unashauriwa kuripoti kwenye ofisi ya NIDA ulikosajiliwa kwa msaada zaidi.
Shukrani.
Samahani nimetoka ofisi za nida Mbeya, jina langu la kwanza lilikosewa lakini wamesema haiwezekani kubadilisha jina la kwanza shida inakuwa wapi cheti ninacho pia vitamburisho vingine ninavyo kwanini wagome kubadilisha jina
Andika barua kwa mkurugenzi Mkuu ukiomba kubadilisha jina hakikisha unaambatisha nyaraka zinazosupport maombi yako wasilisha kupitia info@nida.go.tz utahudumiwa
Habar mkuu majina yangu ni yametofautiana kidogo naitwa mika david fihavango lkn kwenye vyet vyangu natumia michael david fihavango mtanisaidiaje hili mana napaata tabu
Salaam Ndg.
Maaboresho ya Jina
Ili ombi lako lifanyiwe kazi juu ya maboresho ya jina, unapaswa kuwasilisha nyaraka zifuatazo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA:-
i. Kadi ya kliniki, tangazo, cheti cha kuzaliwa, cheti cha darasa la vii, kidato cha iv ama ‘leaving Certificate’
ii. Kiapo ‘Deedpoll’ kilichotolewa na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
iii. Tangazo la gazeti la serikali lenye taarifa ya mabadiliko husika,
iv. Iwapo utaombwa nyaraka nyingine na Afisa Usajili ya kuthibitisha umri utatakiwa kutoa ushirikiano,
v. Mabadiliko yoyote ambayo hayana ushahidi wa nyaraka sahihi na zote zilizo orodheshwa hayatapokelewa wala kuruhusiwa kufanyiwa kazi.
Iwapo makosa yamefanyika upande wetu, Afisa Usajili atajiridhisha na kuendelea na maboresho pasipo kulazimika kulipia gharama yoyote lah utapaswa kulipia shilingi 20,000/=
Muhimu:- ombi la mteja linaweza kuafikiwa ama lah kutegemea na sababu na nia ya mteja kutaka kufanya maboresho ya taarifa zake.
Habari je NIN mpya baada ya marekebisho inachukua mda gan kutoka?
Kwa kawaida NIN huwa haibadiliki. wewe ulibadilidha taarifa gani?
Mimi ni Juliana james Hoja namba yangu ya nida ni 19941003-37302-00001-16 Nliandika barua ya kuomba mama angu arekebishiwe jina ambalo lilikua limekosewa na hivo kusababisha
kufungiwa kutumia kadi ya Nhif ambayo nilimkatia ila sijapata majibu hadi leo, Mzazi wangu anahangaika na matibabu kisa jina kukosewa Naomba msaada wenu
Naomba msaada
Kama ni mama anabadilisha jina anatakiwa yy mwenyewe ndio afanye mabadiliko sio mtu mwingine. fuatilia kujua hatua iliyofikiwa
Samahani mkuu, Taratibu gani nizifuate i.e. nianzie wapi iwapo nataka kubadili Tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa katika taarifa za NIDA?
Mimi ni Juliana james Hoja namba yangu ya nida ni 19941003-37302-00001-16 Nliandika barua ya kuomba mama angu arekebishiwe jina ambalo lilikua limekosewa na hivo kusababisha
kufungiwa kutumia kadi ya Nhif ambayo nilimkatia ila sijapata majibu hadi leo, Mzazi wangu anahangaika na matibabu kisa jina kukosewa Naomba msaada wenu
Naomba msaada
Kama ni mama anabadilisha jina anatakiwa yy mwenyewe ndio afanye mabadiliko sio mtu mwingine. fuatilia kujua hatua iliyofikiwa
Naitwa STANSLAUS KAJERU MKAMA lakini msajili wa NIDA aliandaka STANSILAUS KAJERU MKAMA naomba kujua je naweza kusaidiwa kuondo hiyo “I”iliyo kwenye jina la Kwanza?
Tafadhali Nenda Ofisi yoyote ya NIDA wilayani kwa maelekezo na usaidizi zaidi
Nahitaji kufahamu jina mzazi wangu alikua anatumia jina la babu yake mzaa mama kwenye vitambulisho vyake sasa kwenye cheti changu chakuzaliwa akaniandikisha majina yake rasmi lakin kwenye jina la babu akaniandikia jina la babu mzaa mama ake nlipoanza shule mpaka sasa mimi sikuwahi kutumia hlo jina nikitaka kubadilisha inakuaje.
Tafadhali Fika Ofisi ya NIDA wilaya yoyote iliyo karibu na wewe kwa maelekezo na usaidizi zaidi. Hakikisha una nyaraka zinazothibitisha usahihi wa majina yako
Mwaka 2020 nilianza harakati za kutafuta namba ya nida nilikuwa na vigezo vyote vilivyo hitajika kikiwemo cheti Cha kuzaliwa mwaka 2021 nikapata namba yangu ya NIDA, bad enough ilikuwa na makosa ila nikajaga kujua mwaka 2022 nilipoambiwa kuwa mwanzoni huanzaga na mwaka wa kuzaliwa ndio nikajua kweli namba imekosewa, 2022 nikifika ofisi za NIDA mbeya nikalipoti kweli wakakubali kuwa ni kweli walikosea wao maana cheti Cha kuzaliwa kilikuwepo kwenye taarifa ambazo nilileta mwanzo ilikupata namba ,nikaandika kwenye daftari wakasema watarekebisha from there nikawa nimetingwa na chuo 2023 nikaambiwa na mtendaji kadi yangu imetoka nikitarajia kua taarifa zitakuwa zimerekebishwa lakin still Bado kadi ikawa na makosa namba ya nida mwanzoni inaanza na 2000 bila ya kuanzia 2002 na Cha ajabu sasa pale pale kwenye ile kadi ya NIDA tarehe za kuzaliwa zipo sawa ila ishu ni namba ya nida wamekosea nilivyopata mda tena nikaenda ofisi za NIDA mbeya nikaeleza upya wakaniambia Etty wamerekebisha kwenye mifumo hiyo namba ikiingizwa itareta mwaka 2002 ambayo ni correct na sio 2000 ambao ni makosa , sasa Mimi nyie NIDA naona kama mnanichanganya na mnaniweka matatani how possible is it kwamba namba iwe hivi na taarifa za ndani zipo hivi nahitaji kuelekezwa vizur maana nimeenda tena juzi nikaambiwa the same na jamaa wa kule ni wakali hawaelekezi Zaid ya kufoka foka hovyo , hivi vitu ni sensitive Kwa baadae nisije pata shida , nahitaji maelekezo ya kueleweka maana kule hawaelekezi vizur Zaid ya kufoka na kunyenyua kwenye kiti haraka. Na kama Kuna uwezekano wa kuanza upya process za hiyo nida nipo radhi nianze kuliko kuishi kwenye makosa then baadae ni suffer kivyangu.
Samahanini Kwa ujumbe mrefu.
habari naomba kufahamu nimechukua nida yangu lakini hata mwezi haujafika namba zimeanza kufutika je utaratibu wa kubadilisha nipate card nyingine ukoje
Tafadhali kirejeshe Ofisi ya NIDA wilaya uliyojisajilia ili uchapishiwe kingine
Mm Gibson naomba kujua kama taalifa zangu zimebadilishwa au inachukua mda gani kubadilishiwa jina kama limekosewa??
Tafadhali fuatilia Ofisi ya NIDA wilaya iliyo karibu nawe kufahamu kama mabadiliko ya jina yameshafanyika