Usajili Vitambulisho vya Taifa karatu watia fora, zaidi ya wananchi 1200 kusajiliwa kwa siku

Si kwa idadi hii ya watu iliyofurika katika Wilaya ya Karatu Kata ya Rhotia ambako Usajili wa Wananchi Vitambulisho vya Taifa unaendelea.

Kwa mujibu wa Afisa Usajili Wilaya ya Karatu Bi. Rehema Ngomuo takribani wananchi 1200 wamekuwa wakisajiliwa kwa siku na wengine kushindwa kuwasajili na kulazimika kurejea makwao tayari kwa siku inayofuata bila manung’uniko wala ulalamishi; kutokana na umati mkubwa wa wananchi kufurika kwenye vituo vya Usajili kupata huduma hiyo.

Diwani wa Kata hiyo Bwana Marseli Roli (CCM) ambaye muda wote amekuwepo kituoni hapo kuhakikisha wananchi wake wote wanasajiliwa kwa kuzingatia utaratibu uliopangwa amesema imekuwa ni kawaida ya wananchi katika Kata yake kuitikia wito haraka haswa katika masuala ambayo yana manufaa ya moja kwa moja na maisha yao ya kila siku.

“ Hili suala la Vitambulisho ni suala muhimu na kila mmoja anatambua umuhimu wake na ndiyo maana hatukupata shida ya kuwahamasisha wananchi kufika kusajiliwa kwa kuwa kila mmoja anatambua thamani ya kuwa nacho. Wengine hapa kama unavyowaona wamefika tangu saa 11 alfajiri” alisema

Kwa Wilaya ya Karatu Kata ambazo zinashiriki zoezi hili kwa sasa ni Kata ya Rhotia ambayo baada ya siku saba itafuatiwa na Kata za Janakona na Karatu. Wilaya zingine za mkoa wa Arusha zinaendelea na Usajili zikiwemo Arusha, Arumeru, Longido na Loliondo huku Ngorongoro wakiwa tayari kuanza Jumamosi hii.

 

Umati  wa Watu uliofurika kupata huduma ya Usajili Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi hilo likiendelea katika Kata ya Rhotia. Hawa ni akinamama wajawazito na wenye watoto wachanga wakipatiwa huduma maalumu kwa utaratibu maalumu uliowekwa wa kusaidia wazee, wajawazito na wamama wenye watoto wachanga.

 

Afisa Usajili Wilaya ya Karatu Bwana STEVE MBALA akiendelea na taratibu za kuthibitisha uraia wa waombaji na kugonga muhuri wakati zoezi hili likiendelea. utaratibu huu umekuwa ukifanyika kabla ya mwananchi kuruhusiwa kupiga picha, kuchukuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki.

 

Foleni hii ni ya Watendaji Kata na Wenyeviti katika Vijiji vya Kata ya Rhotia wakithibitisha makazi ya kila mwananchi anayeishi katika Kata na Kijiji chake kabla ya kutoa idhini ya kuthibitishwa uraia.

 

Kushoto ni baadhi wa wazee ambao wanasubiri kuitwa kupata huduma ya Usajili baada ya umri wao kutoruhusu kukaa foleni muda mrefu kupata huduma ya Usajili. Utaratibu huo umetoa fursa kwa wazee wengi kupata huduma kwa haraka na kuwahi kuendelea na mapumziko na hivyo kuongeza idadi ya wazee wenye umri mkubwa kufika kusajiliwa.

 

Hawa ni baadhi tu ya wananchi walioweza kunaswa na kamera yetu wakiwa kwenye foleni ya kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa wakitokea Kata ya Rhotia Wilaya ya Karatu – Arusha

Comments on “Usajili Vitambulisho vya Taifa karatu watia fora, zaidi ya wananchi 1200 kusajiliwa kwa siku”

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg.

      Karibu kwenye ukurasa wetu wa Tovuti wa NIDA tukuhudumie kwa kukupatia elimu juu ya Usajili na Utambuzi wa Watu ambao matokeo yake ni kutoa Utambulisho wa Taifa (NIN) na hatimaye Kitambulisho cha Taifa kwa raia, wageni na wakimbizi wanaoishi nchini kihalali wenye umri wa miaka 18 na zaidi. Shukrani.

  1. contrave says:
    Your comment is awaiting moderation. This is a preview, your comment will be visible after it has been approved.

    Utilisez contrave selon les directives de votre mГ©decin. https://fr.ulule.com/contrave-en-ligne/ Il mai Г©galement ГЄtre utilisГ© pour d’autres conditions comme dГ©terminГ© par votre mГ©decin.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu