Usajili Vitambulisho vya Taifa waanza kwa Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu (Machinga)

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), RITA na Uongozi wa Wilaya ya Ilala umeanza rasmi zoezi la Utambuzi na usajili wa wafanya Biashara ndogo ndogo maarufu (Machinga) katika Wilaya ya Ilala.

Lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa Wafanya biashara wote wadogo wanatambuliwa na kusajiliwa ili kuweza kuwa na mfumo rasmi wa kuwatambua na kuwawezesha kufanya biashara zao kwa uhuru zaidi huku wakichangia kodi stahiki kulingana na aina ya biashara zao.

Zoezi hili litaisaidia serikali kuwatambua na kuwawezesha Machinga kufanya biashara kwa uhuru zaidi, kurahisisha mikopo na kupanua biashara zao sambamba na mifumo rasmi ya Serikali kubadilishana taarifa kwa lengo la kuimarisha mfumo wa biashara nchini na kuwajengea miundombinu bora ya kuendesha shughuli zao.

Kwa sasa zoezi hili limeanza kwenye Wilaya ya Ilala na baaadae litaendelea katika Wilaya zingine za Mkoa wa Dar-es-salaam kabla ya kuhamia kwenye mikao yote ya Tanzania.

 

Afisa wa NIDA Grace Mwambungu akiendelea na uingizaji taarifa kwenye mfumo wakati wa zoezi la usajili wa machinga

 

Afisa wa RITA Mzee Balele akifanya mahojiano na Machinga kuhusu uhakiki wa Umri wake kabla ya kusajiliwa.

 

Afisa wa NIDA Edna Mgema akiendelea na uingizaji taarifa kwenye mfumo wakati wa zoezi la usajili wa machinga

 

Maafisa wa NIDA wakiendelea na mchakato wa kuingiza tarifa kwenye mfumo

 

Maafisa wa NIDA wakiendelea na mchakato wa kuingiza tarifa kwenye mfumo

 

Afisa wa NIDA Grace Mwambungu akihakiki taaarifa katika Fom ya mwombaji

 

Afisa Eveline Malya akimuelekeza Machinga kutia saini ya kielectronic kwenye mfumo.

 

Afisa Huba Ponda akimwelekeza mmoja wa Wamachinga namna ya kujaza fomu za Vitambulisho vya Taifa

 

Afisa wa NIDA Etropia Kimaro akiendelea na mchakato wa kuingiza tarifa kwenye mfumo

 

Afisa wa NIDA Sekosia Moshi akimwelekeza Machinga kuweka alama za vidole kwenye

 

Afisa wa NIDA akimwelekeza Machinga kuweka alama za vidole kwenye mfumo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Taarifa Kwa Umma

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu