Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji atembelea Banda la maonyesho la Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Nanenane – Lindi

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe (MB), ametembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwenye Maonyesho ya 23 ya Nanenane yanayofanyika mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo.

Amepongeza jitihada kubwa za Serikali kuanzisha mfumo wa Taifa wa Utambuzi na Usajili wa Watu, kwani faida za mfumo huo ni nyingi hasa katika kukabiliana na changamoto kubwa ya sasa ambapo wajanja wachache wamejipenyeza kwa kujifanya Raia wa Tanzania na kuchukua nafasi za kazi ambazo zingefanywa na wazawa (Raia).

Amesema kukamilika kwa mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu pia kutasaidia Serikali kupata takwimu sahihi za watu na hivyo kupanga vipaumbele kutegemeana na idadi halisi ya watu, shughuli wanazofanya na mahali walipo; hivyo kuitaka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kufanya shughuli ya Usajili na Utambuzi kwa weledi na umakini mkubwa kwani ndiyo tegemeo kubwa la Taifa katika kufikiwa na malengo na maendeleo yaliyokusudiwa.

NIDA inashiriki kwa mara ya kwanza Maonyesho ya Nanenane mwaka huu kuungana na Wakulima kwa kutoa huduma za Usajili na Utambuzi wa Watu kwa wananchi ambao hawakusajiliwa awali mkoani Lindi, kuchukua alama za kibaiolojia (picha, alama za vidole na saini ya kielektroniki), matumizi ya Tovuti Salama na elimu ya Jumla kuhusu shughuli za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa.

Huduma hizi zinatolewa katika Banda la NIDA lililopo eneo maarufu “TAMISEMI” karibu na Viwanja vya Ngongo. Katika ziara hiyo Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe aliambatana na wenyeji wake; uongozi wa mkoa wa Lindi.

Kauli mbiu ya maonyesho hayo “Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni Nguzo ya Maendeleo, Vijana Shiriki Kikamilifu hapa Kazi Tu”.
IMG_2103
(Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe (MB), akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika banda la Maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwenye Maonyesho ya 23 ya Nanenane yanayofanyika mkoani Lindi katika viwanja vya Ngongo. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami).

IMG_2117

(Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe (MB), akipokea maelezo ya taarifa zilizomo katika kitambulisho kipya chenye saini na tarehe ya mtumiaji. Vitambulisho vipya vilianza kuzalishwa tangu June 1, 2016 na vitaendelea kutumika sambamba na vile vya zamani wakati taratibu za kuendelea kubadilisha vya zamani zikiendelea)

IMG_2111

(Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Eng. Isack Aloyce Kamwelwe (MB), akipata maelezo ya namna Tovuti Salama iliyoanzishwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa inavyofanya kazi, na kupata fursa ya kusoma taarifa zake ndani ya mfumo huo. Akitoa maelezo hayo ni Bi. Valentina Makao, Mchambuzi mifumo ya Komputa).

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Taarifa Kwa Umma

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu