Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA) yafanya usajili wa vitambulisho vya Taifa kwa Waheshimiwa wa Wabunge

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA), imeanza kusajili Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; wakati wakiendelea na kikao cha Bajeti

Katika Usajili huo NIDA inategemea kusajili wabunge wote ambao hawakuwahi kusajiliwa awali na kupata vitambulisho vya Taifa, pamoja na kugawa vitambulisho

Wabunge wameonyesha mwamko mkubwa katika kutumia fursa hii adhimu, kwa kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wa mbele kutimiza haki yao ya kikatiba ya kusajiliwa na kupata kitambulisho cha Taifa; ambacho kimekuwa na faida nyingi kiuchumi, kijamii na kisiasa

Mpaka sasa NIDA imeshatoa zaidi ya vitambulisho zaidi ya milioni 2.5 na kwa sasa NIDA iko mbioni kuanza usajili kwa kutumia mtaji wa taarifa toka NEC ambapo zaidi ya wananchi milioni 22 watasajiliwa na kupewa namba ya utambulisho ili kuanza matumizi mbalimbali

9

(Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) akiwa na Afisa Usajili Bw. Surera wakati akipata huduma ya usajili kwenye ukumbi wa Bunge. Katika zoezi hilo mbali na kujaza fomu za maombi ya Utambulisho, pia walichukuliwa alama za kibaiolojia picha na saini ya kielektroniki)

8

(Dr. Harrison Mwakyembe (Mb) akisaidiwa kujaza fomu na Meneja Usajili Vitambulisho vya Taifa, Bi. Julian Mafuru)

1-2

(Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. Saed Kubenea akiweka saini ya kielectroniki wakati wa usajili wa kitambulisho cha Taifa Bungeni mjini Dodoma.)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu