Kongamano la wadau kutoka sekta mbalimbali wakijadili kuhusu mradi wa Vitambulisho vya Taifa

Wadau kutoka Sekta mbalimbali nchini leo wamekutana katika kongamano maalumu kujadili suala la Vitambulisho vya Taifa na uwezekano wa kukamilika kwa mradi huo ili kuwezesha Taifa kuwa na Kanzidata(database) yenye taarifa sahihi zenye kujibu maswali makuu nani ni nani, yuko wapi na anafanya nini. Lengo ni kurahisisha utoaji huduma na kuwezesha wananchi kujishughulisha na masuala ya biashara kwa kuwa na mfumo rasmi unaowatambua.

Akifungua kongamano hilo, Kaimu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt. Nato Mwamba amesema mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu ni mfumo ambao umesubiriwa kwa siku nyingi kwani manufaa yake ni makubwa katika mifumo mbalimbali nchini hususani mfumo wa biashara na taasisi za fedha nchini

Amesema kutokana na kupanuka kwa matumizi ya teknolojia nchini, huduma nyingi zikiwemo huduma za kifedha zinategemea sana kuwepo kwa mfumo wa Vitambulisho vya Taifa ili kuwezesha watu wengi zaidi kunufaika na huduma zitolewazo kwa sasa kwani wengi wanakwama kwa kuwa hakuna mfumo rasmi unaowatambua. Mafanikio ya mfumo huu ni kufungua milango kwa wananchi wengi zaidi kunufaika na huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa nchini zikiwemo huduma za kifedha na hivyo kuwataka wadau hao kuwezesha NIDA kufikia malengo ya usajili nchi nzima kufikia Disemba 31, 2016 ili mfumo wa Utambuzi wa Taifa uweze kuunganishwa na mifumo mingine.

Akieleza mkakati wa usajili kufikia Disemba 31, 2016, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dkt. Medestus Kipilimba amesema NIDA imejizatiti kutumia taarifa zilizokusanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kuanza usajili utakaowezesha wananchi waliosajiliwa katika daftari la wapiga kura kuhakikiwa na kupata usajili awamu ya kwanza ambao utahusisha namba ya utambulisho kabla ya kupata kitambulisho cha Taifa. Amesema hatua ya kufanya usajili wa awali na kutoa namba ya utambulisho itawezesha wananchi kuanza kufaidi utambulisho wao kwa kuwawezesha kupata huduma mbalimbali. Hata hivyo ili mwananchi aweze kupata utambulisho kamili lazima kukamilisha hatua za usajili kwa kuhakikisha anawasilisha nyaraka muhimu za utambuzi ili kuendelea kupata huduma nyingine.

Kwa mara ya kwanza NIDA itaanza kuzalisha vitambulisho vyenye saini ya mwombaji ambayo itawekwa kwenye uso wa mbele wa kitambulisho na nyumba ya kitambulisho kutakuwa na saini ya mtoaji. Amesema hatua zote katika kukamilisha mpango huo zimekamilika.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau toka Taasisi za fedha nchini, TASAF, Wamiliki wa makampuni ya simu nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Benki ya Dunia (World Bank), SSRA, BIMA, Melinda and Bill Gates Foundation, Tanzania Bankers Association( TBA) na wawakilishi wa Taasisi mbalimbali za Serikali.

fsdt1

(Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akifungua kongamano la wadau kuhusu vitambulisho vya Taifa lililofanyika leo katika ukumbi wa Benki Kuu na kuhudhuriwa na wadau toka sekta mbalimbali nchini)

fsdt6

(Mkurugenzi  mtendaji wa Financial Sector Deepening Trust Sosthenes Kewe akichangia mada wakati wa kongamano wa wadau lililohusu mpango wa Usajili vitambulisho vya Taifa)

fsdt5

(Mkurugenzi wa Fedha toka TASAF Bw. Joshua Nyamko akiwasilisha mada katika kongamano la wadau kujadili Vitambulisho vya Taifa)

fsdt3

(Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Dkt. Modestus Kipilimba akionyesha wadau sampuli ya vitambulisho vyenye saini vitakavyoanza kutolewa hivi karibuni, wakati wa kongamano la wadau kuhusu mpango wa vitambulisho vya Taifa)

fsdt4

(Mr. Sanjay C. Rughani Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini akiwasilisha mada wakati wa kongamano la wadau katika mpango wa usajili vitambulisho vya Taifa)

fsdt2

(Baadhi wa washiriki wa Kongamano la wadau kuhusu mpango wa Usajili vitambulisho vya Taifa wakisikiliza kwa makini mada ya mkakati wa Usajili kufikia Disemba 31,2016 iliyowasilishwa na NIDA)

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu