Usajili Vitambulisho vya Taifa katika mkoa wa Mwanza na wilaya zake umepamba moto, ambapo wananchi kutoka Wilaya za Kwimba, Ukerewe, Ilemela, Misungwi na Sengerema wamejitokeza kwa wingi kusajili. Kwa wananchi wa Wilaya Nyamagana, taratibu za kuanza kwa Usajili zinaendelea ambapo wataanza usajili rasmi wiki hii.
Katika kufanikisha zoezi hilo Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa pamoja na Watendaji wa mitaa/Vijiji wamejizatiti kwa dhati kuhakikisha zoezi hili linafanyika na kukamilika kwa wakati uliopangwa. Aidha; Wamewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kusajiliwa kutokana na manufaa mapana ya zoezi hilo kwa mwananchi mmoja mmoja na kwa Taifa kwa ujumla.
Zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilayani ya Ukerewe likiendelea, pichani ni baadhi ya wananchi wa kata ya Kakelege wakisubiri zoezi la kupigwa picha na kuchukuliwa alama za Kibaiolojia.
Afisa Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Ndg. Zabron Rusohoka akiwaelekeza baadhi ya wananchi taratibu wanazopaswa kuzifuata wakati wa ujazaji fomu za maombi ya Wilayani Ukerewe.
Umati wa wananchi wa Kata ya Ukerewe kijiji cha Nakatunguru wakisubiri huduma ya Usajili wakati zoezi la Usajili likiendelea Wilayani humo.
Mmoja wa mafafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa akimsaidia mmoja wazee waliofika kwenye kituo cha usajili kusajiliwa.
Mwananchi wa kata ya Nansio akichuliwa alama za kibaiolojia wakati wa zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa
Hawa ni baadhi ya akinamama wa Kituo cha Nansio Ukerewe waliojihimu mapema kusajiliwa wakati zoezi la usajili likiendelea Wilayani humo.
Msaada wa kujua namba yangu ya nida mtandaon wanasema taarifa zako sio sahihi fika ofisini ulipojiandikishia
salaam Ndg. ukijaza taarifa kwa usahihi utapata majibu lah unashauriwa kufika kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi.