Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoa wa Songwe

Zoezi la Usajili na Utambuzi wa Watu limeendelea leo mkoani Songwe, ambapo zaidi ya Kata 5 tayari zimekamilisha Usajili huo uliolenga kukusanya taarifa sahihi za watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wakiwemo wageni wanaoishi kihalali mkoani humo.

Wakazi wa Songwe na Mbozi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusajiliwa ili kunufaika na manufaa mapana ya Kitambulisho hicho na pia kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora zaidi.

 

Afisa Usajili Wilaya ya Mbozi Ndugu Eckson Mwakyembe akiwa na Mtendaji wa Kijiji cha Mlowo Bi. Judith Mtega wakikamilisha fomu za maombi ya Usajili za wananchi wa vijiji vya Shuleni, Mtakuja, Mlowo na Kiwandani kata ya Mlowo wakati zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa likiendelea wilayani humo.

 

Meneja Mifumo ya Komputa wa ndugu Francis Saliboko akifanyia matengenezo ya kiufundi moja ya kifaa kinachotumika wakati wa usajili katika zoezi linaloendelea Kata ya Mlowo – Mbozi mkoani Songwe.     

 

Maafisa Usajili wa NIDA wakifanya kazi ya kupiga picha na kuchukua alama za kibaiolojia katika zoezi linaloendelea kata ya Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe.   

 

Afisa Usajili Bi. Coletha Peter na Bi. Magreth Moshi wakisaidia taratibu za kuchambua na kuhakiki fomu za maombi ya Vitambulisho za wananchi wa kata ya Mlowo kwa ajili ya hatua ya mwisho ya kupiga picha, kuchuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki.

 

Mwananchi wa kata ya Mlowo akichukuliwa alama za vidole,  picha na kuweka saini ya kielektroniki wakati wa Usajili Vitambulisho vya Taifa. kushoto ni Afisa Usajili Ndugu Baraka Haonga.

Comments on “Usajili Vitambulisho vya Taifa mkoa wa Songwe”

  1. Agape says:

    Ni mda gani inachukua kuipata namba baada ya kujiandikisha maana mimi imepita wiki moja bado namba sijazipata

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Namba ya Utambulisho wa Taifa huzalishwa ndani ya wiki hadi wiki mbili na muda usio zidi mwezi tangu mwombaji anapokamilisha Usajili iwapo maombi ya mwombaji wa Utambulisho wa Taifa yamekidhi vigezo. Shukrani.

      1. Geofrey Tengeneza says:

        Kufahamu iwapo NIN imeshazalishwa

        Tafadhali piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja Na:- 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666,

        Ingia kwenye tovuti ya NIDA (www.nida.go.tz), fungua neno Kitambulisho cha Taifa kwenye menyu kuu kisha fuata maelekezo au fungua kiunganishi (link) -https://services.nida.go.tz/nidportal/get nin.aspx au

        Fika kwenye Ofisi ya Usajili ya NIDA katika Wilaya iliyo karibu nawe.

        Shukrani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Taarifa Kwa Umma

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu