Maelfu Wapewa Elimu ya Usajili na Utambuzi Nanenane

Na Thomas Nyakabengwe, NIDA

Maelfu ya wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamepewa elimu kuhusu Utambuzi na Usajili katika Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.

Elimu hiyo imetolewa na maofisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wanaoshiriki kwenye maonesho hayo yaliyoanza Agositi Mosi, 2024 kwa wakazi wa mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Rukwa, Ruvuma na Katavi.

Katika maonesho hayo, banda la NIDA limekuwa miongoni mwa mabanda yanayotembelewa na watu wengi ambao baadhi wanaanza kusajiliwa, wanaotaka kufanya marekebisho ya taarifa zao yakiwamo majina na umri na wanaotaka kufahamu kama Namba zao Utambulisho wa Taifa (NIN) zimezalishwa na kupata Vitambulisho vya Taifa.

Maonesho ya Nanenane 2024 yana kaulimbiu “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”

NIDA ni mdau muhimu katika Maonesho hayo kwa sababu inawezesha utambuzi wa wakulima, wavuvi na wafugaji wanapotaka kupata huduma za kifedha ikiwamo mikopo ya mitaji na  kupata pembejeo za kilimo kwa kuzitaja chache. Maonesho ya Nanenane yatafikia kilele chake Agosti 8, 2024.

Comments on “Maelfu Wapewa Elimu ya Usajili na Utambuzi Nanenane”

  1. BALYEFAO TIBWAKAWA HONORATH says:

    Habari za kazi, Mimi ni mwenye majina hapo juu!, naomba mnisaidie kunibadilishia majina kwenye mfumo wenu wa nida,kwani nilijiunga kwenye mfumo wenu wa nida mwaka 2017 nilikuwa nimejisajili BALYEFAO HONORATH TIBWAKAWA,nikawa nimeajiriwa mwaka 2019 January,hivyo tukaambiwa majina ya vyeti kama ni mawili inatakiwa kuwa hivi; BALYEFAO TIBWAKAWA HONORATH, naomba mnisaidie kunibadilishia majina yawe kama utumishi yasomavyo.Nitashukuru kwa ufanisi wenu,

    Mawasiliano:0787100156~ Whatsapp on

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Andika barua kwa Mkurugenzi Mkuu, SLP 12324 Dar es Salaam kuomba mabadiliko hayo ukieleza sababu za mabadiliko hayo. Hakikisha umeambatisha nyaraka zinazothibitisha usahihi wa majina hayo unayoyataka

  2. Abdukarim Ally Hassan says:

    Sijui napataje kitambulisho cha NIDA ikiwa tayari ninayo namba ya NIDA

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Tafadhali fungua link ifuatayo https://vitambulisho.nida.go.tz ili kufahamu kitambulisho chako kilipo

  3. John Mburu Emanuel says:

    Nilikuwa na changamoto ya jina,mim majina noi john mburu Emanuel ila hapo Emanuel ilitakiwa iwe Emmanuel yani iwe na double (m) Sasa nimeenda ofisi za nida mkoani kwangu singida mjini mwezi na nusu Sasa unakata bila mafanikio yeyote naambiwa hawajajibiwa kutoka makao makuu email na nilishalipia kabisa sh.20000 na control number hiyo:991140263591 namba za risiti ya malipo:924232270938148. NIDA YANGU:19920101-43110-00023-23

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Endelea kufuatilia katika ofisi ya NIDA iliyo jirani na wewe kufahamu kama marekebisho yamefanyika

  4. John Mburu Emanuel says:

    Nilikuwa na changamoto ya jina,mim majina noi john mburu Emanuel ila hapo Emanuel ilitakiwa iwe Emmanuel yani iwe na double (m) Sasa nimeenda ofisi za nida mkoani kwangu singida mjini mwezi na nusu Sasa unakata bila mafanikio yeyote naambiwa hawajajibiwa kutoka makao makuu email na nilishalipia kabisa sh.20000 na control number hiyo:991140263591 namba za risiti ya malipo:924232270938148. NIDA YANGU:19920101-43110-00023-23

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Endelea kufuatilia katika ofisi ya NIDA iliyo jirani na wewe kufahamu kama marekebisho yamefanyika

  5. Bahati Silvanus says:

    Nida yangu inasomeka Justine Sylvanus Maindah lakini kwenye vyeti vyangu inasomeka Bahati Hamis Silvanus,je naweza kurekebishwa majina ya fanane na majina ya jwenye vyeti vyangu? Naomba msaada wenu please on 0714100149

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Ndio unaweza kufanya marekebisho. nenda ofisi ya NIDA wilaya iliyojirani na wewe kwa maelekezo na usaidizi zaidi

  6. My brother recommended I might like this website.
    He was entirely right. This post truly made my day.
    You cann’t imagine simply how much time I had spent for this information!
    Thanks!

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Thank you very much

    2. Geofrey Tengeneza says:

      You are welcome

  7. Geofrey Tengeneza says:

    You are welcome

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu