MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imewataka wananchi wote ambao vitambulisho vyao vimepata hitilafu ya kufutika maandishi
kuvirejesha katika ofisi za NIDA ama katika ofisi za Serikali za Mitaa, Kata, Vijiji na Shehia ambako vitakusanywa na kurejeshwa kwa ajili ya kuchapishwa upya bila malipo yeyote kwa mwananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho kutoka NIDA Edson Guyai wamepokea taarifa ya kuwepo kwa Vitambulisho vichache kufutika taarifa zailizochapwa mbele au nyuma ya kitambulisho mfano majina, picha au Namba ya Kitambulisho au tarehe ya kuzaliwa.
Mkurugenzi huyo amesema takwimu za Mamlaka hiyo zinaonyesha kuwa vitambulisho vyenye hitilafu hiyo ni 21,224 sawa na asilimia 0.09 ya vitambulisho 21, 32,098 viliyozalishwa. Ametoa rai kwa mwananchi ambaye Kitambulisho chake kitakuwa na changamoto hiyo akirudishe ofisi ya NIDA au kwa mtendaji alipokichukua ili virudishwe na kuchapishwa upya.
Amesema kumekuwa na upotoshaji kuhusu ubora wa vitambulisho vya Taifa kutokana na changamoto hiyo ndogo iliyojitokeza na amesisitiza kwamba Vitambulisho vya Taifa vinavyotolewa na Mamlaka hiyo vina ubora unakidhi viwango vya kimataifa.
Amedokeza kuwa kwa sasa wataalamu wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tatizo hilo kama ni mashine, wino au kadi. Hii itawezesha kufidiwa kwa kadi hizo kama yalivyo matakwa ya mkataba bila Serikali kuingia gharama yeyote.
Mkurugenzi huyo amesema hitilafu ndogondogo ni jambo la kawaida kutokea katika sekta ya uzalisha wa bidhaa duniani huku akieleza kuwa hata kammpuni kubwa za uzalishaji kama magari na simu za mkononi hupata changamoto kama hizi.
Mwananchi akichukuliwa alama za vidole katika moja ya ofisi za NIDA kwa ajili ya Utambulisho wake wa Taifa
Mwananchi akikabdhiwa Kitambulisho chake katika moja ya ofisi za Serikali ya Mtaa
Mwananchi akipigwa picha kwa ajili ya utambulisho wa Taifa
My nida information
My nida informations
Tell us what should we do for you?
Tell us what should we do for you?
Vitambulisho ni vizuri ila wino uliotumika hauna ubora hata ukiugusa tu utaona unafutika kabisa.binafsi changu kimefutika na nilichukulia morogoro na kwa sasa naishi bagamoyo.pwani sijui nafanyaje?
Nenda nacho Ofisi ya NIDA wilaya uliyopo ili kuripoti na uchapishiwe kingine
Naomba kutumiwa kitambulisho kingine Cha awali kimepotea
Jina Fred Joel Kaoneka
Hakikisha unapata loss report ya polisi, kisha nenda nayo Ofisi yoyote ya NIDA kwa hatua zaidi ili uchapishiwe kitambulisho kingine
NATAKANIDA
Umeshajisajili?
Nida yangu ilikosewa majina badala ya Chrispin Stephano Karanga ikaandikwa Crispin Steven Karanga.
Manisaidiaje nimeshaandika barua makao makuu majibu bado.
Fuatilia majibu ya barua yako
Samahani majina yangu yamechanganywa kwenye nida,la mbele limewekwa Kati,ulitumia njia gani kuwaandikia
Fika Ofisi ya NIDA wilaya iliyo karibu kupata maelekezo na taratibu za kubadilisha taarifa
Kitambulisho changu kilipotea na loss report nimeshapata naomba kujua control namba ili niende ofisini nimelipa kabisa
Tafadhali fungua link ifuatayo https://services.nida.go.tz kisha chagua Namba ya malipo kisha fuata maelekezo utapata Namba ya malipo
Naomba namba ya nida huu mwezi wa tano sijapata
Jina:James josephat pius
Namba hazichelewi kutoka kwani ndani ya siku 7 hadi 14 namba inakuwa imeshatoka. kama bado, tafadhali fungua link ifuatayo https://services.nida.go.tz kisha chagua Fahamu NIN halafu fuata maelekezo. kama bado nenda ofisi uliyojisajilia kwa ufuatiliaji zaidi
Napataje kitambulisho cha NIDA ikiwa sikuwahi kukipata lakini nina namba ya NIDA
Tafadhali fungua link ifuatayo https://vitambulisho.nida.go.tz ili kufahamu kitambulisho chako kilipo
Mie Niko mbali na sehemu niliyojazia nida yangu mara ya kwanza nilikuwa nikiingia online kuicheki no yangu naiyona ila kwa sasa siioni Tena na taarifa nazo jaza ni sahihi ila inakataa
Mbona link ya kuangalia mahali kilipo kitambulisho haifunguki?
Itakuwa ni shida ya mtandao, endelea kufungua
Majina yamekosewa nabadilishaje yawe sahihi
Tembelea Ofisi ya NIDA wilaya iliyo jirani na wewe kupata maelekezo na utaratibu wa kufanya ili ubadilishe