Na Calvin Minja – NIDA
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imezindua mfumo mpya wa kidigitali unaomuwezesha mwananchi kujua kitambulisho chake kipo eneo gani kwenye Wilaya aliojiandikisha.
Mfumo huo ni mahususi kwa wananchi wote ambao wamejiandikisha na bado hawajachukua Vitambulisho vyao katika Ofisi za NIDA za Wilaya.
Mfumo huu umekuja baada ya NIDA kuzindua zoezi la ugawaji Vitambulisho kwa Umma, zoezi hilo lilizinduliwa Kitaifa Oktoba 12, 2023 mkoani Mara na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (Mb).
Zoezi la ugawaji wa Vitambulisho kwa umma kwa mkupuo linatagemea kuhitimishwa mwezi Machi, 2024 ambapo kila aliejiandikisha atakuwa amepata Kitambulisho chake.
Huduma hii ya kujua Kitambulisho kilipo inapatikana kwa kupitia tovuti ya Mamlaka www.nida.go.tz kisha utabofya mahali palipoandikwa Kitambulisho cha Taifa ikifuatiwa na palipoandikwa Fahamu Kitambulisho kilipo, au kwa kufungua kiunganishi wezeshi http://vitambulisho.nida.go.tz kisha utachagua Mkoa ambao ulijiandikisha, utachagua Wilaya uliojianikisha na mwisho utachagua jina la Kijiji au Mtaa uliojiandikishia na kuangalia jina lako kwenye orodha kama halitakuwepo utatakiwa kufika kwenye Ofisi ya NIDA ya Wilaya ulipojiandikisha kujua kuna changamoto gani kwenye maombi yako.
“Lengo la kuanzisha mfumo huu ni kurahisisha upatikanaji wa huduma na kumrahisishia mwananchi kujua wapi kitambulisho chake kilipo bila kufika kwenye Ofisi zetu. Nitoe rai kwa wananchi kuchukua Vitambulisho vyao kwa wakati katika Ofisi za Serikali ya Mtaa/Kijiji walichojiandikisha ndani ya muda uliopangwa pia kuwapatia ushirikiano wadau wote wanaohusika kwenye zoezi hili ” Geofrey Tengeneza, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NIDA.
Mpaka sasa NIDA imepokea jumla ya maombi 24,495,804 ya watu wanaohitaji Utambulisho wa Taifa pamoja na Kitambulisho cha Taifa, jumla ya Namba za Utambulisho wa Taifa zilizozalishwa mpaka sasa ni 20,786,171, Vitambulisho ambavyo vimeshazaliswa ni 19,370,666 jumla ya Vitambulisho vilivyosambazwa ni 17,161,600 na Vitambulisho ambavyo vimechukuliwa ni 12,837,523.
Kwa upande mwingine NIDA tayari ilikwisha zindua usajili kwa njia ya mtandao ambapo muombaji anatakiwa kuingia kwenye kiunganishi wezeshi cha https://eonline.nida.go.tz kisha kutafuata maelekezo. Huduma nyingine inayopatikana kwa njia ya mtandao ni huduma ya kuangalia namba ya Utambulisho wa Taifa ambapo mwananchi anafungua kiunganishi wezeshi https://services.nida.go.tz/nidportal/get_nin.aspx kisha anajaza taarifa zake kwa usahihi na kubonyeza neno tuma.
1. Naomba kuuliza kwamba endapo kwa bahati mbaya mda wa mwisho wa kuchukua kitambulisho cha taifa kwenye wilaya ulipojiadikishia utaisha kabla hakijachukuliwa, mwanainchi atafanya nini ili kupata kitambulisho chake ?
2. Je? Ninaweza kumuagiza mtu kunichukulia kitambulisho cha taifa
Salaam Ndg.
Muda wa kuchukulia Serikali za Mitaa ukiisha, Vitambulisho vinarudishwa kwenye ofisi ya Usajili wilayani ulikosajiliwa.
Utaratibu wa sasa kwa wanaoruhusiwa kucukilia/wa ni watoto nawazazi, wagonjwa, wazee, wanandoa ama kwa ambao mwenekiti amejiridhisha kuwafahamu. Anayemtuma mtu ataandika barua na anayemchukulia mtu ataandfika barua ya kukiri kumchukulia mtumaji.
Shukrani.
Axante kwa mrejesho
Hiyo link ya kujua vitambulisho vilipo nayo haifunguki
Mbona inafunguka?
Samahani, nilijiandikisha zaidi ya mwenzi sasa lakini namba haitoki na kila taarifa iko sahihi . Nifanye nini na Nina uharaka sana na Nida number? Nimejaribu kurudi nilipojiandikisha bado nikaambiwa nisibiri zaidi, nimejaribu kutuma ujumbe lakini hakuna majibu yeyote.. naomba mnisaidie niipate Kwa wakati au nielezwe nifanye nini’ Asante
Tafadhali fungua link https://services.nida.go.tz kisha chagua Fahamu NIN kujua namba yako
Habar ivi nida inatumika Kama bima ya afya, na Kama mtu anayo namba ya nida kadi ilipotea afanyaje kupata hiyo kadi
report ya polisi kisha nenda nayo Ofisi yoyote ya NIDA wilaya iliyo karibu na wewe kwa maelekezo na taratibu zaidi ili kuchapishiwa kingine
Naomba kufahamu namna ya kupata kitambulisho Cha nida
Ni miaka sita sasa sijapata
Fungua link https://vtambulisho.nida.go.tz kufahamu kitambulisho kilipo
Samahani ndg
Huduma ya kuangalia kitambulisho cha nida kama nimeshatoka na mahali kilipo kwa sasa imesitishwa ??
Fungua link https://vtambulisho.nida.go.tz kufahamu kitambulisho kilipo
Napata wapi kitambulisho
Maaana wenzangu wamepata mm mpaka hatua hii sijakipata
Na selikali za mitaaa akipo kama kipo tayar naeza kifata gongol la mboto
Kwa kituo cha nida?
Tafadhali Fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz kujua kitambulisho chako kilipo
Habari za majukumu waheshimiwa!
Nanba ya kitambulisho changu nimeipata tangu mwaka 2022, lakini kwa bahati mbaya jina langu la kwanza limekosewa herufi moja IBRAHIM badala ya IBRAIM yaani herufi H ndiyo inayotakiwa kutoka, Na kitu kingine kilichokosewa ni tarehe ya kuzaliwa 08/12/…., badala ya tarehe 18/12/…., kama ilivyo kwenye cheti cha kuzaliwa.
naomba nisaidiwe katika hili kwasababu taarifa za namba yangu ya NIDA hazifanani na taarifa zangu za elimu.
Nasubili mrejesho nikiwa na tumaini la kusaidiwa kwa haraka.
Ahsante!
Nenda Ofisi ya NIDA wilayani kupata maelekezo na taratibu za mabadiliko ya taarifa
Habari najaribu kuangalia namba yangu ya nida online nikafanikiwa kuiyona ila nilikuwa sijai copy sehemu yeyote saizi najaribu kuangalia Tena nashindwa kuipata sijajua tatizo nini wakati taarifa zangu nilizo angalia mwanzo namba yangu ya nida ndio hizo hizo zinazo kataa
Tafadhali fungua link https://services.nida.go.tz kisha chagua fahamu NIN na kufuata maelekezo kujua namba yako
Hbr Ndg…pole pia na majukumu naomba kufahamu namna ya kujua kitambulisho kilipo?
Tafadhali fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz kujua kitambulisho chako kilipo.
Sorry naomba kufahm kitambulish changu kilipo mpak mda huu na nilisikia vimetokasijapata
Tafadhali fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz kisha fuata maelekezo kufahamu kitambulisho chako kilipo
Nahitaj kufahm kitambulish changu sijakipata toka mwak jana
Tafadhali fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz kisha fuata maelekezo kufahamu kitambulisho chako kilipo
khamisjuma296@gmail.com
Karibu tukuhudumie
Ninaitwa mwagala mbusi nyanza nimzaliwa wa kilimanjaro wilaya ya hai kata ya boma ng,ombe kitongoji cha kibaoni nilijisajili katika kupata kitambulisho cha taifa katika mkoa kilimanjaro wilaya yahai nilikua nauliza ninaweza kukipata kitambulisho cha taifa kwanjia ya simu
Hapana, kifuate sehemu kilipo ili ukachukue
Kwanini naingia kwenye mfumo wa kuangalia kitambulisho kilipo lakini inakataa kufunguka page
inawezekana ni shida ya mtandao, endelea kfungua
Mimi nikujaza taarifa zangu, nikituma inaniambia jaza taarifa zako kwa usahihi, nahitaji msaada.
Maana yake kuna kitu unakosea, hasa herufi za majina yako na ya mama.
Nataka kitambulisho changu
Fungua link ifuatayo: https://vitambulisho.nida.go.tz kufahamu kitambulisho kilipo
Nilifanikiwa kupata namba yangu ya nida na niliitumia sehemu mbalimbali, lakini kwa sasa kila nikiitumia naambiwa haipo shida itakuwa ni nini?
Tafadhali tembelea Ofisi yoyote ya NIDA eleza shida hiyo kujua tatizo ni nini na utahudumiwa ipasavyo
Kila nikitumia namba yangu ya nida naambiwa haipo kwa sasa shida itakuwa ni ni i?
Tafadhali tembelea Ofisi yoyote ya NIDA eleza shida hiyo kujua tatizo ni nini na utahudumiwa ipasavyo
Nimefuata kitambulisho changu mahali nilipojiandikisha na taarifa zinaonesha kuwa kitambulisho kilishatoka maana nimejiandikisha 2017 na hakijulikani kilipo nitafanya Nini ili kukipata na Kama nitashindwa ni njia gani mbadala wa kupata kitambulisho changu?
Tafadhali fungua link ifuatayo https://vitambulisho.nida.go.tz ili kufahamu kitambulisho chako kilipo
Naitwa Joseph ikombe katambi naulizia kitambulisho changu Cha NIDA
Fungua link ifuatayo: https://vitambulisho.nida.go.tz kisha fuata maelekezo au piga simu 0232210500 kufahamu Kitambulisho kilipo
Jamani mbona izo link za kuangalia vitambulisho kama vimetoka hazifunguki?
Itakuwa shida ya mtandao. endelea kufungua
Nimejiandikisha Zaidi ya Miaka 4 ,nishapata Namba tu lakini kitambulisho nishafatulia hakijatoka lakin Namba inaonyesha taarifa zangu sahihi sasa sijajua tatizo Ni nini?
Tafadhali fungua link https://vitmbulisho.nida.go.tz kisaha fuata maelekezo au piga simu namba 0232210500 kufahamu kitmbulisho chako kilip
Samahan mm nilikuwa naulizia kama mtu majina yake yamekosewa kwenye kitambulisho Cha nida anaweza kwenda kufanya marekebisho?
Ndio unaweza kufanya marekebisho. kama umeshachukua kitambulisho nenda ofisi yoyote ya NIDA wilaya iliyo karibu na wewe na kama kitambulisho bado hakijatoka nenda ofisi uliyojisajilia kwa maelekezo zaidi.
Habari, samahani kitambulisho changu ofisi nilipojiandikishia hakipo ila nikiangalia kwa njia ya mtandao wa nida online naambiwa kipo ofisi nilipojiandikishia, kwanini ilihali napo hakipo?
Tembelea Ofisi ya NIDA wilaya uliyojiandikishia kwa usaidizi zaidi
Nahitaji kujuwa kama kitamburisho changu kimetoka
Tafadhali fungua link https://vitmbulisho.nida.go.tz kisaha fuata maelekezo au piga simu namba 0232210500 kufahamu kitmbulisho chako kilip
Nashindwa kupata kitambulisho changu
Tafadhali fungua link https://vitmbulisho.nida.go.tz kisaha fuata maelekezo au piga simu namba 0232210500 kufahamu kitmbulisho chako kilipo
Naomba msaada, nilijiandikisha na kukamilisha hatua ya kupigwa picha Wilaya ya Itilima kata ya Mwamtani lakini mpaka Sasa sijapata NIN na nimeshahamia mkoa mwingine, je ninaweza kujiandikisha upya?
Au nifanyeje ili nijue NIN yangu Kama imeshatoka au la!
Tafadhali usijiandikishe tena. fungua link https://services.nida.go.tz kisha fuata maelekezo au piga simu namba 0232210500 kupata msaada zaidi
Nimeshapata kitambulisho Chang lkn Saini haikutoka km nlivyoandika je kuna uwezekano wa kubadilisha
Tafadhali tembelea Ofisi ya NIDA wilaya iliyo karibu nawe kwa maelekezo zaidi
Samahani mimi nilijiandikisha mweZi wa tano mwaka huu mpaka sasa namba ya NIDA sijapata.naomba kuelewshwa kinachoendelea.
Tafadhali fungua link https://services.nida.go.tz kisha fuata maelekezo au piga simu namba 0232210500 kupata msaada zaidi
Kujua kitambulisho kilipo mbn haifunguki muheshimiwa au imesitishwa
Itakuwa ni shida ya mtandao tu
Naitaji kujua kitambulisho change kama tayr kwasababu inaenda mwezi wa tatu tangu nijisajiriii na kupata namb ya nida mkuu
Fungua link https://vitambulisho.nida.go.tz kisha fuata maelekezo au piga simu namba 0232210500 kufahamu kama kimetoka na mahali kilipo
Naomba kuona kitambulisho changu cha NIDA
Hatujakuelewa, unahitaji huduma gani ndugu tukuhudumie