Jinsi ya Kuhuisha Kitambulisho cha Taifa
Jinsi ya Kuhuisha Taarifa za Kitambulisho kilichopotea kwa raia
Kuna hatua mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa na mwombaji aliyepoteza Kitambulisho cha Taifa ili kupatiwa kingine na kuna gharama kidogo mwombaji atatakiwa kuchangia:-
Mwombaji unatakiwa kuwasilisha fomu ya polisi ya upotevu wa mali/vitu, katika ofisi ya usajili ya NIDA ya wilaya ulikosajiliwa ama iliyo karibu nawe ili upatiwe Namba ya Malipo ya Serikali (Controll Number),
Fanya malipo ya TZS 20,000/= NMB/CRDB/NBC au PBZ ikiwa ni kuchangia gharama ya kutengenezewa Kitambulisho kingine
Wasilisha risiti ya malipo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA kukamilisha taratibu zilizosalia za kuanza kuchapwa kwa Kitambulisho kipya.
Gharama za kuchapisha Kitambulisho kilichopotea kwa mara ya pili ni 30,000 na 50,000 kwa mara ya tatu.
Jinsi ya Kuhuisha Kitambulisho kilichochakaa kwa raia
Mwombaji unatakiwa kuwasilisha Kitambulisho kilichochakaa katika ofisi ya usajili ya NIDA katika wilaya ulikosajiliwa ama iliyo karibu nawe ili upatiwe Namba ya Malipo ya Serikali (Controll Number),
Fanya malipo ya TZS 20,000/= NMB/CRDB/NBC au PBZ ikiwa ni kuchangia gharama ya kutengenezewa Kitambulisho kingine.
Wasilisha risiti ya malipo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA kukamilisha taratibu zilizosalia za kuanza kuchapishiwa Kitambulisho kipya.
Gharama za kuhuisha Kitambulisho kilichochakaa kwa mara ya pili ni 30,000 na 50,000 kwa mara ya tatu.
Jinsi ya Kuhuisha Kitambulisho Kilichopotea kwa Mgeni Mkaazi
Kuna hatua mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa na mwombaji Mgeni Mkaazi aliyepoteza Kitambulisho cha Taifa ili kupatiwa kingine na kuna gharama kidogo mwombaji atatakiwa kuchangia:-
Mwombaji unatakiwa kuwasilisha fomu ya polisi ya upotevu wa mali/vitu, katika ofisi ya usajili ya NIDA ya wilaya ulikosajiliwa ama iliyo karibu nawe ili upatiwe Namba ya Malipo ya Serikali (Controll Number),
Fanya malipo NMB/CRDB/NBC au PBZ ikiwa ni kuchangia gharama ya kutengenezewa Kitambulisho kingine:
Mwekezaji $ 100 kwa mara ya kwanza, $150 kwa mara ya pili na $200 kwa mara ya tatu,
Mfanyakazi $ 50 kwa mara ya kwanza, $75 kwa mara ya pili na $100 kwa mara ya tatu,
Wamisionari, Watafiti & Wanafunzi $ 20 kwa mara ya kwanza, $ 30 kwa mara ya pili na $40 kwa mara ya tatu,
Mtegemezi$ $ 20 kwa mara ya kwanza, $ 30 kwa mara ya pili na $40 kwa mara ya tatu,
Wasilisha risiti ya malipo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA kukamilisha taratibu zilizosalia za kuanza kuchapishiwa Kitambulisho kipya.
Jinsi ya Kuhuisha Kitambulisho Kilichochakaa kwa Mgeni Mkaazi
Kuna hatua mbalimbali zinazotakiwa kufuatwa na mwombaji Mgeni Mkaazi aliyepoteza Kitambulisho cha Taifa ili kupatiwa kingine na kuna gharama kidogo mwombaji atatakiwa kuchangia:-
Mwombaji unatakiwa kuwasilisha Kitambulisho chakavu, katika ofisi ya usajili ya NIDA ya wilaya ulikosajiliwa ama iliyo karibu nawe ili upatiwe Namba ya Malipo ya Serikali (Controll Number),
Fanya malipo NMB/CRDB/NBC au PBZ ikiwa ni kuchangia gharama ya kutengenezewa Kitambulisho kingine:
Mwekezaji $ 50, Mfanyakazi $ 25,Wamisionari, Watafiti & Wanafunzi $ 10,Mtegemezi$ 10.
Wasilisha risiti ya malipo kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA kukamilisha taratibu zilizosalia za kuanza kuchapishiwa Kitambulisho kipya.