Kupitia NIDA
Mafanikio mengine ya Serikali Awamu ya Sita Madarakani kupitia NIDA ni pamoja na Upandishaji vyeo Watumishi. Katika kipindi tajwa jumla ya Watumishi 485 wa Mamlaka wamepandishwa vyeo na kubadilishwa Kada. Mafunzo,:- Watumishi 69 wamehudhuria mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu, Ajira:- Watumishi wapya 22 wameajiriwa.
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Inatoa shukurani za dhati kwa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuiwezesha NIDA kutekeleza majukumu yake kwa mafanikio makubwa katika Kipindi hiki cha mwaka mmoja wa Utawala wake..