TAARIFA KWA UMMA: NIDA YASITISHA MATUMIZI YA NAKALA TEPE YA KITAMBULISHO CHA TAIFA (ONLINE ID COPY)

Comments on “TAARIFA KWA UMMA: NIDA YASITISHA MATUMIZI YA NAKALA TEPE YA KITAMBULISHO CHA TAIFA (ONLINE ID COPY)”

  1. Adinani Bashiru Athuman says:

    nina hitaji pata nakala ya kitambulisho cha taifa napataje maana kitambulisho changu kimepotea sasa nahitajika apply jambo wana hitaj nakala ya kitambulisho mnanisaidiaje

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg,
      Huduma ya Nakala tepe imeshasitishwa kitambo.

      Kufahamu iwapo Kitambulisho Kimeshazalishwa
      Tafadhali fika kwenye Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au unaweza kupiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimeshachapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.
      Iwapo utafahamishwa kuwa NIN/Kitambulisho chako bado hakijazalishwa, utatakiwa kuendelea kusubiri huku ukifanya ufuatiliaji baada ya muda. Kwa mwenye uhitaji wa haraka unatakiwa kuwasilisha ombi na vielelezo vya kuthiitisha sababu ya uharaka ulionao kwa Afisa Usajili.

      Shukrani.

      1. Violeth says:

        Utaratibu wakuomba nakala ya kitambulisho Cha NIDA kwa haraka ukoje? Nina shida na nakala hiyo mno maana sijapata kitambulisho chenyewe hadi Sasa nina namba tu

        1. Geofrey Tengeneza says:

          Salaam Ndg. Unashauriwa kupiga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 ili kufahamishwa iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua au unaweza kufika kwenye ofisi ya NIDA katika wilaya ulikosajiliwa.

          Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.

          Aidha huduma kwenye taasisi zilizounganisha mfumo wao na wa NIDA, hutolewa pia kwa mteja iwapo ana Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN).

  2. Marion says:

    Habari
    Mbona namba zenu hazipatikani??

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Tafadhali endelea kupiga bila kuchoka kwani yawezekana kuna mteja anapatiwa huduma kupitia laini ya simu unayoipiga.

  3. Haika Urassa says:

    Habari
    Mbona mimi sijapataga kitambulisho changu tokea 2020 mpaka na leo nilipewa namba tu tafadhali naomba mnisaidie

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. fika Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.

      Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.

      Shukrani.

  4. Wicklif wambi says:

    Naitaji kupata hata angalau namba ya nida make nikienda kwenye ofisi za nida naambiwa haijatoka leoi imeshapita miaka 2 toka nimejiandikisha

    1. Geofrey Tengeneza says:

      NIN YANGU IMECHELEWA KUZALISHWA

      Tafadhali fika kwenye Ofidi ya Usajili ya NIDA kwa utatuzi zaidi kwani unapaswa kumuuliza Afisa anayekuhudumia ili akufahamishe sababu ya NIN kutokuwa tayari kwani yawezekana kuna upungufu kwenye taarifa ulizowasilisha ili ombi lako liweze kwenda hatua za kuzalishwa kwa NIN, huzalishwa ndani ya wiki na muda usiozidi mwezi mmoja iwapo mwombaji kakidhi vigezo vyote baada ya taarifa za mwombaji kuhakikiwa katika hatua mbalimbali.

      Iwapo hutopata ndani ya muda huo ni vizuri kuripoti kwenye ofisi ya Usajili ya NIDA wilayani ili kuhakikiwa taarifa zako kwani yawezekana taarifa zako zina mapungufu.

      Shukrani.

  5. Regina Omollo says:

    Habari
    Mbona mimi nikitaka kudhibitisha kuwa namba niliyonayo ni ya kwangu nikijaza taarifa naambiwa sio sahihi akati ndo taarifa zilizoandikwa unakuta kuna tatizo gani naomba msaada tafadhali

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. naweza fikiri unajaza kwa usahihi lakini sivyo, unaweza kufika ofisini kwa msaada zaidi. Shukrani.

  6. Paul says:

    Kama jina limkosea na kitambulisho kimetoka nigalama kias gan inaitajika ili kubadiri

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam NDg. TZS 20,000/=

  7. EMANUEL SAMSON says:

    Je kwa sas nakala ya nida inaendelea kupatikana maana sehemu nyingi wanadai wanatoa copy au nakala ya vitambulisho vya nida na kama huduma imeruhusiwa tena tafadhal tunaomba maelekezo na official statement kwamba vinapatikana maan hii hilo tangazo ni la muda mrefu kwa hiyo tuna sintofahamu nyingi kama huduma imerejeshwa au bado na je wanaotoa copy wanazitoa wapi?
    Pili vitambulisho vyetu naona vimechelewa tangu 2020 hadi leo havijatoka tunaomba mtusaidie kuweza kupatikana mapema

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. huduma ya Nakala Tepe ya Kitambulisho Mtandaoni imesitishwa kitambo. Aidha siku za karibuni tuliujuza umma kupuuzia huduma hiyo kwani kwa sasa haipo.

      B.
      Tutashukuru iwapo utatoa ushirikiano wa kutuelekeza eneo ambalo huduma hiyo inatolewa ili NIDA kwa kushirikiana na vyombo vya Usalama ifanye ufuatiliaji wa kina kujiridhisha juu ya kinachoelezwa nje ya hapo inakuwa ngumu kupata pa kuanzia.

      C
      Tafadhali unashauriwa kufika Ofisi ya Serikali ya Mtaa/Kijiji/Sheia/NIDA ulikosajiliwa au piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.

      Unaweza kutuma ombi lako https://demo.emalalamiko.egatest.go.tz/complaint ili kuangaliziwa moja kwa moja kwenye mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu.

      Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID kwa haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.

      Shukrani.

  8. Josephat Ogunya says:

    Mimi nina Namba ya NIDA Tayari lakini sehemu nyingi hawataki namba wanataka kiambatanisho nilichofanya nimeandika namba zangu za NIDA na Majina yangu yote nikabandika Picha yangu na Kisha Nikaweka sahihi chini kisha Nikaprint kwenye karatasi na sasa huwa nakitumia kama copy yangu ya kitambulisho cha NIDA. Je? Niko sawa wakati nikiendelea kusubiria hicho chenu cha Orginal ili niendane na Muda wa Soko la mahitaji ya kazi yangu!!!?

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Haiko sahihi.

  9. Nakija mteti says:

    Nimejiandikisha mkoa wa Morogoro kwa sasa niko Arusha, je naweza nikapata kitambulisho changu kwa huku Arusha?

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Ndiyo inawezekana kulingana na taratibu zetu. Shukrani.

  10. JS Media255 says:

    Unajuaje kama kitambulisho chako kipo tiari?

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg.

      Tafadhali fika kwenye ofisi ya NIDA ulikosajiliwa au piga simu kwenye Kituo cha Huduma kwa Mteja 0752 000 058, 0687 088 888, 0777 740 006 au 0677 146 666 kufahamu iwapo Kitambulisho chako kimechapishwa na kilipopelekwa kwa ajili ya kukichukua.

      Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.

      Aidha huduma kwenye taasisi zilizounganisha mfumo wao na wa NIDA, hutolewa pia kwa mteja iwapo ana Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN).

      Shukrani.

  11. Magreth clemence kihaga says:

    Kama jina lako limekosewa na kitambulisho hakijatokaa inakuaje kukubadilisha

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Unashauriwakuripoti kwenye Ofisi ya Usajili Wilaa ulikosajiliwa kwa uhakiki na msaada zaidi. Shukrani.

  12. Asham mohamed namera says:

    Najaribu download copy yangu ya kitambulisho inanikatalia

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Huduma ya Nakala Tepe Mtandaoni, haipo kwa sasa. Shukrani.

  13. Joseph says:

    Je naweza pata kitambulisho ikiwa Niko sehemu togauti na nilikosajiliwa? Na je Kama inawez Jana nafuata njia zipi ili kupata?

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg.

      KUCHUKULIWA KITAMBULISHO CHA TAIFA NA MTU MWINGINE.

      Iwapo umearifiwa Kitambulisho chako cha Taifa kimeshachapishwa, Unaweza kuchukuliwa Kitambulisho hicho na mtu mwingine aliyeko katika wilaya ulikosajiliwa au yoyote. Mtambulishe kwa barua yenye majina yako matatu na yake, NIN zenu na saini. Unayemtuma atatakiwa kuwa na Kitambulisho cha Taifa, kisha atawasilisha barua hiyo ofisi husika.

  14. Joseph says:

    Samahani nauliza nawezaje kupata kitambulisho Cha taifa togauti na sehemu niliko andikisha?

  15. Eugenny Og says:

    Habari Naitwa EUGEN Mimi Sio Kuuliza Mimi Naomba Basi Mnisaidie Kupata Hata Picha Pande 2.Zote Make Google Payments Ili Wanithibitishe Ninapoishi Inaahitaji Kitambulisho Cha taifa Au Cha Mpiga Kula Sasa Sina Na Kura Nipaka Mwaka 2004 Mimi Nakitaji Tarehe 25 Dec Niwe nishapata Nisaidie Nambari Yangu Ya WatsaApp +255768423032 Unikifanikishia Nitakupa Elfu 15000 Majina Ni EUGEN LEONARD KATABAZI 10_03_2003

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Huduma ya Usajili kwa raia kwa mara ya kwanza ni Bure hivyo ni kosa kutaka kulipa huduma hiyo. Unashauriwa kuripoti Ofisi ya Usajili Wilayani kwa utatuzi zaidi. Shukrani.

  16. Gerald Adam says:

    Nahitaji kitambulisho Cha taifa kwa uharaka zaidi sijui nafuata hatua zipi ili kupata kitambulisho hiki tafadhali naomba msaada???

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Mwombaji wa Utambulisho wa Taifa (NID) ambaye bado kupatiwa Kitambulisho cha Taifa, unatakiwa kusubiri na kufanya ufuatiliaji baada ya muda kidogo kupita. Iwapo unahitaji NID kwa haraka, wasilisha ombi na vielelezo vya kuthibitisha uharaka ulionao kwa Afisa Usajili kwa hatua zaidi.

      Shukrani.

  17. Noel says:

    kunauwezekano wakubadili tahalifa kwenyekitambulisho cha taifa

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Ndiyo, iwapo utakidhi vigezo kwani kila taarifa ina vigezo vyake. Shukrani.

  18. Kassim says:

    Habari,
    Nataman sana kujua kuna changamoto zipi zinazokwamisha upatikanaji wa vitambulisho vya NIDA? nimeshafika mara nyingi ofisi ya serikali ya mtaa kuulizia. jibu ni lilelile la BADO. Nipo na namba ya nida tangia 2020. gharama ya ufuatiliaji maana ya muda na pesa za nauli inatumika.
    Litolewe tamko kwa manufaa ya wengi ili kama kuna changamoto ifahamike.

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Tumeutaarifu umma kuvuta subira punde tutawafkia wachache waliosalia katika mwaka huu wa fedham Shukrani.

  19. Nega says:

    Mimi nilijisajili toka 2018 nina NIN number lakm kitambulisho hadi sasa sima nilifatilia ofisi ya wiliaya kimara lakn sikuweza kufanikiwa kupata NIDA yangu nahitaj msaada

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Tafadhali piga simu Kituo cha Huduma kwa Mteja kwa namba 0677 146 666, 0777 740 006, 0752 000 058 au 0687 088 888 au tembelea Ofisi ya Usajili ya NIDA iliyo karibu nawe ili kufahamu kama kitambulisho chako kimeshachapishwa. Karibu

  20. Sokoine sipitieki says:

    Napataje nakala ya kitambulisho changu id copy

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Ndg. Sokoine kama ni online copy, huduma hiyo ilishasitishwa kitambo hivi sasa haipo. kama ni Kitambulisho chenyewe tafadhali piga simu Kituo cha Huduma kwa Mteja kwa namba 0677 146 666, 0777 740 006, 0752 000 058 au 0687 088 888 au tembelea Ofisi ya Usajili ya NIDA iliyo karibu nawe ili kufahamu kama kitambulisho chako kimeshachapishwa. Karibu

  21. Moses says:

    Mamlaka ya vitambulisho vya uraia tatizo nini mtu tangu mwaka 2018 mpaka leo mwaka 2023 hajapewa kitambulisho

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Moses,
      Tumeutaarifu umma kuwa, wananchi ambao bado hatujawafikia, punde tutaweza kuwafikia wote kwa mara moja hivyo nikuombe uvute subira kwani tunatambua ni wajibu wetu kukuhudumia, Dhamira tunayo kwa kiwango kikubwa. Punde dhamira yetu itaweza kufikia hitaji lako.
      Shukrani

  22. FABIAN MAHALA says:

    NINA NAMBA YA NIDA NATAKA KUPATA TAARIFA ZANGU

    1. Geofrey Tengeneza says:

      Salaam Ndg. Fabian,

      Unashauriwa kuripoti kwenye ofisi ya Usajili kwa msaada zaidi wa utatuzi.

      Shukrani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu