Katika Kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imeendesha Zoezi Maalum la Usajili na Ugawaji wa Namba za Utambulisho wa Taifa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Zoezi hili linaloendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam linafanyika kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Jeshi la Polisi, Uhamiaji na Watoa Huduma wa Mitandao ya Simu nchini kwa lengo la kufanikisha mpango wa Serikali wa kukamilisha usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ifikapo Desemba 31,2019.
NIDA inawakaribisha wakazi wote wa Dar es Salaam kufika Mnazi Mmoja kujisajili kwa ajili ya Vitambulisho vya Taifa pamoja na kusajili laini za simu. Maonyesho hayo ya siku tano yanafanyika tarehe 17-21 Juni, 2019.
Pichani ni wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wakipatiwa huduma mbalimbali katika banda la NIDA kwenye maonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Huduma zinazopatikana katika banda la NIDA ni pamoja na huduma ya Usajili, Utoaji wa Nambari za Vitambulisho kwa wateja waliowahi kusajiliwa awali pamoja na dawati la huduma kwa wateja.

Afisa uhamiaji Bw. Mashaka C. Mfanga akikagua fomu za baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliofika kukamilisha zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa katika maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Pichani ni Bw. Shaban Sekwande, Afisa Usajili NIDA akitoa maelezo kwa wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kusajiliwa katika maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.