Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa imeibuka Mshindi wa kwanza katika Maadhimisho ya Maonyesho ya 40 ya Kibiashara Kimataifa – Sabasaba kama Banda Bora katika Kutoa Huduma Bora na yenye Viwango kwa Umma inayotoa mchango katika Kuwezesha Kuunganisha Biashara na Masoko pamoja na Uwekezaji (Best Exhibitor Trade and Investment Support Dar Es Salaam International Trade Fair – DITF) yaliyoanza tarehe 28/06/2016 – 08/06/2016
Kupitia Utambulisho; NIDA inakusudia kuunganisha biashara na masoko kupitia Kanzi data (database) ambayo itaunganisha mifumo yote ya Serikali na Binafsi katika utoaji huduma. Zipo huduma ambazo tayari zimeanza kutumia mfumo wa Nida katika utoaji huduma ikiwemo sekta ya Benki
Zipo faida nyingi za kuwa na Kitambulisho cha Taifa kiuchumi, kisiasa ,kijamii na Kiulinzi na Kiusalama.
Katika maonyesho ya 40 ya Kimataifa Sabasaba mwaka huu, huduma ambazo zinatolewa ni Usajili wa moja kwa moja kwa wananchi ambao hawana vitambulisho, kusoma taarifa za mwananchi zilizopo kwenye kadi, kutoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya vitambulisho yanayokusudiwa pamoja na kuonyesha njia mbalimbali zinazotumika kusoma taarifa zilizomo kwenye kadi.
(kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NIDA (katikati) akiwa na wafanyakazi wengine wa NIDA kwenye banda la NIDA katika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa-sabasaba mara baada ya kupokea tuzo ya banda bora katika maonyesho hayo).