Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inapenda kuwatangazia na kuwakaribisha wananchi wote kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Kibiashara (40), SABASABA. Banda letu liko kwenye Banda maarufu “JAKAYA TENTS”. Tutembelee kupata huduma zifuatazo:-
- Usajili wa Awali, utakaohusisha uchukuaji wa alama za kibailolojia, picha na Saini ya Kielektroniki
- Fahamu muonekano mpya wa Vitambulisho vya Taifa vyenye saini
- Iwapo umefanya maombi ya Vitambulisho na hujapata Kitambulisho hadi leo; kwenye Banda letu utapata fursa ya kujua hatua maombi yako ya kitambulisho yalipofikia na kama hujasajiliwa kabisa pia tunatoa fursa ya kujisajili
- Kufahamu taratibu za kupata Kitambulisho kipya cha Taifa na hatua za kufuata kwa wale waliopoteza Vitambulisho
- Je? Ungependa kujua taratibu za kubadilisha Jina lililokosewa kwenye Kitambulisho au umebadilisha jina na ungependa kupata kitambulisho chenye jina jipya
- Pia tunatoa elimu kuhusu matumizi ya Tovuti Salama yenye uwezo wa kusoma taarifa za mwombaji zilizomo kwenye chip ndani ya Kitambulisho; pamoja na kutoa elimu ya Umuhimu na matumizi ya Vitambulisho vya Taifa
Kwa watakaofika kusajiliwa kwenye banda letu tafadhali fika na nakala (photocopy) ya viambata muhimu vitakavyo kutambulisha kama:
- Cheti cha Kuzaliwa,
- Kadi ya Mpiga Kura,
- Leseni ya Udereva,
- Kitambulisho cha Bima ya Afya,
- Kadi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF, PPF, GEPF, ZSSF n.k),
- Kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi,
- Namba ya Utambulisho ya Mlipa Kodi (TIN)
- Na vyeti vya elimu ya Msingi au Sekondari
Karibu sana NIDA; tuko kukuhudumia
“Vitambulisho vya Taifa kwa uzalishaji na Masoko”