Jaji Mkuu wa Tanzania Mh Chande Othman atembelea banda la Maonyesho la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA leo Jumapili 03 Julai 2016 viwanja vya Mwl Nyerere sabasaba na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa kwenye Banda hilo pamoja na kuona muundo mpya wa kitambulisho chenye saini ya mmiliki na ya mtoaji wa kitambulisho hicho
(Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Chande Othman akipata maelezo kutoka kwa kaimu wa kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami wakati alipotembelea banda la NIDA kwenye maonesho ya sabasaba. Kushoto ni waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles John Mwijage)
(Jaji Mkuu wa Tanzania Mh. Chande Othman akiangalia sampuli ya kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na NIDA wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kwenye maonyesho ya sabasaba).