UTANGULIZI:
Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi ni moja ya vitengo vilivyoanzishwa ili kuweza kumsaidia Mkurugenzi Mkuu kwenye shuguli za kila siku za Mamlaka. Kitengo cha Usimamizi kina jukumu la kuhakikisha kinasimamia na kubaini viashiria vya Vihatarishi vinavyoweza kujitokeza kwenye shughuli za kila siku za Mamlaka na kupunguza Vihatarishi hivyo kwa kushirikiana na Idara/ Vitengo vilivyopo.

MUUNDO WA KITENGO.
Kitengo kinaundwa na kamati ya uongozi, ambayo hutoa maelekezo kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu pamoja na kamati ya Usimamizi wa Vihatarishi na ukaguzi. Kamati hiyo hutoa ushauri kwa Mkuu wa Kitengo cha usimamizi wa vihatarishi pamoja na kumshauri Mkurugenzi Mkuu juu ya Vihatarishi vyote vinavyotokea kwenye Mamlaka, mchoro hapo chini unajieleza namna kitengo kilivyoundwa na kinavyofanya kazi.

praygod

 

MIKAKATI YA UBORESHAJI WA KITENGO.
Kutokana na ukweli wa kwamba dhana ya usimamizi wa vihatarishi kwenye taasisi za serikali ni mpya, kitengo kinachukua hatua zifuatazo kwenye kuboresha shughuli za kitengo;

 1. Kuomba mafunzo ya mara kwa mara ya ndani na je ya nchi ili kuboresha ufanisi kwenye kazi kwa maafisa wa kitengo.
 2. Kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa watumishi wote wa Mamlaka ili kueneza dhana ya usimamzizi wa vihatarishi kwa kila mtumishi ili aweze kuona jukumu la kusimamia vihatarishi si la kitengo tu bali ni la kila mtumishi wa Mamlaka.
 3. Kushikiriki kwenye mazoezi na shughuli nyinginezo za Mamlaka ili kuweza kusaidiana kusimamia vihatarishi vinavyoweza kujitokeza.

MAFANIKIO YA KITENGO
Kitengo cha usimamizi toka kuanzishwa kwake pamoja na changamoto zilizopo lakini kinajivunia mafanikio mathalani;

 1. Kitengo kimefanikiwa Kuandaa rejesta kuu ya vihatarishi (Risk Register) ya Mamlaka na rejesta ya kila idara na kitengo kwa ajili ya utekelezaji. Rejesta kuu ya vihatarishi wakuu wa Idara/Vitengo wamekwisha kabidhiwa na imeshaanza kutumika katika kusimamia vihatarishi vilivyobainika.
 2. Kitengo kimefanikiwa kuandaa Mwongozo wa Sera ya Usimamizi wa Vihatarishi katika Mamlaka na umekwisha kusainiwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. MATHIAS CHIKAWE (MP). Mamlaka imeshaanza kuutumia katika usimamizi wa vihatarishi.
 3. Kitengo kimekwishaandaa mpango wa utekelezaji (Action Plan) wa usimamizi wa Vihatarishi kwa kila Idara na Vitengo na kusainiwa na wakuu wa idara na vitengo kwa utekelezaji.
 4. Kitengo kimekuwa kikiendesha Mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka juu ya uelewa wa usimamizi wa vihatarishi.
 5. Kitengo kimekwishanda muongozo wa mafunzo na baadhi ya watumishi wamekwishapitishwa kupatiwa mafunzo ikiwa ni pamoja na watumishi wote wa NIDA Zanzibar na Pemba.
 6. Kitengo kimekuwa kikishiriki mazoezi yote ya utambuzi na usajili na shughuli nyingine na kufanya ukaguzi na kubaini viashiria vya vihatarishi vinavyojitokeza na kuvitafutia ufumbuzi katika hali ya kuokoa zoezi lisiharibike.
 7. Kitengo kina utaratibu wa kuandaa ripoti za kila siku na kuziwasilisha kwa wakurugenzi husika kwa ushauri juu ya viashiria vya Vihatarishi vinavyojitokeza kwenye shughuli mbalimbali za Mamlaka.

MATARAJIO YA KITENGO
Katika kuboresha ufanisi wa utendaji kazi kwa kitengo, Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi kina matarajio yafuatayo;

 1. Kuendelea kufanya kazi na kushauri Mamlaka juu ya mwenendo wa mazoezi yanayoendelea
  Kutoa mafunzo ya uelewa juu ya usimamizi wa vihatarishi pindi kitengo kinapoalikwa kwenye vikao na mikutano mbalimbali ya kiutendaji ndani ya Mamlaka.
 2. Kuendelea kupata mafunzo ya mara kwa mara kwa Maafisa wa kitengo ili kuboresha utendaji wao haswa upande wa uchunguzi.
 3. Kufanya maboresho/mapitio (review) ya Rejesta kuu ya Vihatarishi kwa kila Idara na Vitengo mwishoni mwa mwaka wa fedha 2014/2015.
 4. Kuendelea Kukagua, Kubaini na kusimamia Vihatarishi katika Mamlaka
  Kupata ushirikiano kutoka kwenye idara na vitengo na watumishi wa Mamlaka wakati wa utekelezaji wa majukumu ya kikazi kwa maafisa wa kitengo.