UTANGULIZI.
Wakati wa kuanzishwa kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kupitia Hati maalumu ya uanzishwaji, GN No. 122/2008 mambo yote ya sheria yalikuwa chini ya Kitengo cha Sheria.

Tangu mwaka 2008 hadi 2012 ilionekana wazi kuwa Kitengo cha Sheria kilikuwa kinapata changamoto nyingi za kimuundo ambapo ilipelekea kukifanya Kitengo cha Sheria kuwa Idara. Mwaka 2012 Kitengo cha Sheria kilibadilishwa rasmi kuwa Kurugenzi ya Sheria ambayo ilipewa majukumu kadhaa ya kiutendaji kama yanavyojionyesha hapa chini.

MAJUKUMU.
Majukumu ya Kurugenzi ya Sheria ni kama ifuatavyo;

 1. Mshauri Mkuu wa Mkurugenzi Mkuu.
 2. Kutoa huduma zote za kisheria kwa Mamlaka.
 3. Kutunza nyaraka zote za kisheria za Mamlaka.
 4. Kuiwakilisha Mamlaka katika Mahakama au mabaraza yoyote ya kisheria katika masuala ambayo Mamlaka inahusika moja kwa moja au ina maslahi.
 5. Kumsaidia Mkurugenzi Mkuu katika majukumu ya Katibu wa Sheria wa Mamlaka.
 6. Kupendekeza marejeo ya Sheria na Kanuni zake.

MAFANIKIO.
Tangu Mamlaka ianzishwe mnamo mwaka 2008 hadi sasa Kurugenzi ya Sheria imeweza kufanikiwa katika mambo kadhaa; moja wapo ya mafanikio hayo ni kama ifuatavyo;

 1. Imehusika kikamilifu katika uanzishwaji wa Mamlaka Kisheria kupitia Hati ya Uaznishaji GN No. 122/2008.
 2. Imefanya marekebisho ya Sheria ya Usajili na Utambuzi wa Watu, Sura ya 36
  Ipo katika hatua za mwisho za kutangaza kanuni ndogo za Sheria Na. 36
 3. Imependekeza kuwa Sheria ya Usajili na Utambuzi wa Watu, Sura ya 36itungwe upya. Mapendekezo haya yapo katika Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kupata ridhaa.
 4. Kumshauri Mkurugenzi Mkuu katika mambo yote ya kisheria, kazi ambayo ni endelevu.
 5. Imeendelea kutoa huduma zote za kisheria kwa Mamlaka, pia hii ni kazi endelevu,
 6. Kurugenzi imeiwakilisha Mamlaka katika mabaraza ya kisheria na kufanikisha kushinda katika mashauri ambayo yaliihusu Mamlaka moja kwa moja
 7. Nyaraka zote za kisheria za Mamlaka zimeendelea kutunzwa na Kurugenzi ikiwa ni jukumu endelevu
 8. Jukumu la kumsaidia Mkurugenzi Mkuu kama katibu wa mamlaka limeendelea kufanyika. Hili pia ni jukumu endelevu kwa Kurugenzi.