IDARA YA FEDHA NA UTAWALA.

UTANGULIZI

Idara ya Fedha na Utawala (DFA) ni idara “mama” ndani ya Mamlaka kati ya idara tano (5) zilizopo katika Taasisi hii, idara hizo ni Fedha na Utawala, Huduma za Sheria, Mifumo ya Kompyuta (TEHAMA), Mipango Bajeti na Milki, Pamoja na Uzalishaji Vitambulisho. Sambamba na kuwa na idadi hiyo ya idara, Mamlaka pia ina Vitengo vitano (5) kama inavyoonekana kwenye tovuti hii (katika sehemu ya “vitengo”).

 

MAJUKUMU

Idara ya fedha na utawala ina majukumu yafuatayo;

 1. Kuhakikisha kuwa rasilimaliwatu pamoja na rasilimalifedha zinatumika katika kuleta ufanisi na tija kwa Mamlaka.
 2. Kumshauri Mkurugenzi Mkuu juu ya masuala yote yahusuyo menejimenti ya rasilimaliwatu, fedha pamoja na utawala.
 3. Kutafsiri sheria, kanuni za kudumu za utumishi wa umma, miongozo pamoja na sheria za kazi.
 4. Kupanga na kusimamia mchakato wa ajira ndani ya Mamlaka, kupeleka/kufanya “deployment” ya watumishi, kupandisha vyeo, kusimamia nidhamu ya watumishi, pamoja na maendeleo ya watumishi (staff development) katika Mamlaka.
 5. Kushirikiana na (Liaise with) taasisi nyingine juu ya masuala yahusuyo rasilimaliwatu, fedha na utawala.
 6. Kusimamia na kulinda mali za Mamlaka dhidi ya wizi, upotevu, na hujuma.
 7. Kuhakikisha usalama na afya mahala pa kazi ndani ya Mamlaka.
 8. Kuhakikisha kunakuwepo mifumo mizuri ya usimamizi wa masuala ya fedha.
 9. Kuhakikisha watumishi wanahudhuria mafunzo na semina mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea uwezo kulingana na mpango wa mafunzo uliopo.
 10. Kuhakikisha Mamlaka inakuwa na mifumo mizuri ya motisha kwa watumishi wake.
 11. Kutunza kumbukumbu za watumishi.

MUUNDO WA UONGOZI WA MAMLAKA