NIDA KUSHIRIKI NANENANE KITAIFA SIMIYU

Na: Agnes Gerald

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), inatarajia kushiriki katika Maadhimisho ya Maonyesho ya 27 ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi maarufu, Nanenane Kitaifa yenye kauli mbiu: “Kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi chagua Viongozi Bora 2020” yaliyopangwa kufanyika Mkoani Simiyu kwenye Viwanja vya Nyakabindi kuanzia tarehe 01/08/2020 hadi tarehe 08/08/2020.  

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bw. Geofrey Tengeneza amesema kuwa itashiriki na kuyatumia maonesho hayo ili kutoa huduma za Usajili na Utambuzi wa Watu na kutoa elimu kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi juu ya jinsi Mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu unavyochochea Kasi ya Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini jambo lililochangia katika nchi yetu kuingia katika Uchumi wa Kati ndani ya miaka michache ya serikali ya awamu ya tano ikiwa madarakani.

Bw. Tengeneza amesema, NIDA ni Ufunguo na Nguzo ya Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi nchini. Hii ni kutokana na Serikali kupitia NIDA kujenga Mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu madhubuti na imara wenye kubeba taarifa sahihi za wakazi wote wanaoishi nchini wenye umri wa miaka 18 na zaidi ikijumuisha raia (wananchi), wageni na wakimbizi na hatimaye kutoa Vitambulisho vya Taifa vyenye kuwawezesha Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kutambulika Kitaifa na Kimataifa, hivyo kuweza kupata huduma za kijamii, kiuchumi na kiusalama kirahisi.

Mfumo huo, una manufaa makubwa katika kuchochea ukuaji wa sekta ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo kwa kuwawezesha Wakulima, Wavuvi na Wafugaji kutambulika kirahisi, YEYE NI NANI?, YUKO WAPI?, ANAFANYA NINI? NA ANAMILIKI NINI? katika taifa hili, maswali ambayo yamebeba dhana kuu ya Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu.

“Mfumo huu unawasaidia Wakulima, Wavuvi na Wafugaji kutambulika kirahisi kwa kunawapatia manufaa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukopesheka kirahisi katika taasisi za kifedha kwa kuwa atakuwa na Namba ya Utambulisho ama Kitambulisho cha Taifa” alisema Bw. Tengeneza.

Tengeneza amesema kuwa Mfumo huu unaiwezesha pia Serikali kutoa ruzuku za pembejeo za kilimo na mbegu bora kwa wakulima, zana za Uvuvi kwa wavuvi na za ufugaji kwa wafugaji kirahisi kwani sasa kupitia Mfumo wa Utambuzi wa Watu  ruzuku ina kwenda kwa walengwa.

Ameongeza kwamba Mfumo huo pia unawezesha serikali ama sekta binafsi kutoa fidia za majanga kwa wanao kumbwa na majanga mbalimbali katika shughuli za kilimo, uvuvi na mifugo kama vile majanga ya moto, mafuriko, upepo mkali, wadudu wavamizi na waharibifu wa mazao, magonjwa ya mlipuko, n.k iwapo yametokea, kwani taarifa zao muhimu za Nani ni Nani?, Yuko Wapi? na Anafanya Nini? katika Taifa hili kupatikana kwenye mfumo wa Utambuzi wa Watu.

Bw. Tengeneza ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu ambao hawajawahi kujitokeza Kusajiliwa, kujitokeza na kutumia nafasi hiyo. Amewataka pia ambao wanahitaji kujua hatua ambayo maombi yao ya kupata vitambulisho vya Taifa ilipofikia pia kujitokeza kwani huduma hiyo pia itakuwepo.

Huduma nyingine itakayokuwepo ni pamoja na ya wananchi wanaohitaji kuhuisha taarifa zao za majina, umri na Makazi iwapo hawakuzijaza kwa usahihi ama kwa waliopoteza Vitambulisho vya Taifa, na kutakuwa pia na Dawati la kutoa Elimu kwa Umma.

Shughuli za Usajili na Utambuzi wa Watu zikiendelea katika hatua mbalimbali wakati wa Maonesho

Comments on “NIDA KUSHIRIKI NANENANE KITAIFA SIMIYU”

 1. Joseph Jengwa says:

  Naomba sana kitambulisho changu sijapata kwa muda mrefu na kadi namba ni 19431228-53120-00004-14 kwa jina la: JOSEPH MWASE JENGWA Na nimezaliwa tarehe 28/12/1943

  1. Nida says:

   Kama hujapata bado hakijachapishwa. kikichapishwa utafahamishwa kwa ujumbe wa maneno au kupigiwa simu

 2. Yekonia Pafoni Mwampashi says:

  Kitambulisho changu kimekosewa jina nasaidiwaje?

  1. Nida says:

   Nenda ofs ya NIDA ulikojisajilia kufanya hayo mabadiliko

 3. Visai Athuman says:

  Nilipeka fomu mwezi wa sita lakini hadi sasa taarifa zangu sizipati maana hadi leo hii namba yangu ya nida sijapata naomba msaada wenu 0782668202 VISAI ATHUMAN MCHUMA 11/07/1988

  1. Nida says:

   Tuma meseji kwenda namba 15096 kwa kuandika:
   Jina lako la kwanza*jina lako la mwisho*tarehe mwezi mwaka wa kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama

 4. Bisaya Raphael says:

  Tafdhali naomba kupata namba yangu,nina mwezi sasa bado sijapata,na ni mwanafunzi,nategemea kutumia hizo namba kwa maombi ya mkopo elimu ya juu,nimemaliza form 6

  1. Nida says:

   Tuma meseji kwenda namba 15096 kwa kuandika:
   Jina lako la kwanza*jina lako la mwisho*tarehe mwezi mwaka wa kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama

 5. Nasra Peter nanyaro says:

  Cjapata kitambulisho changu toka nilipojisajili mwaka juz nipo ngerngere mkoa wa morogoro

  1. Nida says:

   Fuatilia ofisi ya NIDA ulikojisajilia

 6. PAULO STEVEN CHARLES says:

  Nimeisahau namba yangu yanida niliandikishia kata ya mabwepande mkoa wa Dare m wilaya yakinondon PAULO STEVEN CHARL 08/09/1993

  1. Nida says:

   Tuma meseji kwenda namba 15096 kwa kuandika:
   Jina lako la kwanza*jina lako la mwisho*tarehe mwezi mwaka wa kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama

 7. Advent Emily Sikana says:

  Naitwa Advent Emily sikana nilizaliwa tar 24/02/1988 sijapata namba ya nida toka nilivyo jiandikisha na kupiga picha naomba msaada wenu Mimi nipp wilaya ya momba Kara ya chitete kijiji cha kitete kitongoji cha mntakomwa

  1. Nida says:

   Tuma meseji kwenda namba 15096 kwa kuandika:
   Jina lako la kwanza*jina lako la mwisho*tarehe mwezi mwaka wa kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama

 8. Rajabu issa rajabu says:

  Samahani ningependa kuuliza je kuna uwezekano was kubadili have sahihi ikiwa niliotumia katika kitambulisho nahitaji ibadilishwe sababu kipind najiandikisha nilikuwa naumwa na nilikuwa na ugonjwa was kutetemeka Sasa kwa Sasa nashindwabkuipiga so naomba utaratibu tafadhir 19880505332120000421 my contact 0767541880

  1. Nida says:

   Nenda ofisi ya NIDA wilaya ulikojiandikisha utaelekezwa hayo mabadiliko

 9. Joseph Jengwa says:

  Naomba kitamburisho changu chenye namba 19431228-53120-00004-14

  1. Nida says:

   Nenda ofs ya NIDA ulikojisajilia kuuliza kama kimetoka utafahamishwa

 10. Godfley peter kikoti says:

  Naomba msaada wakupatiwa namba ya nida toka nimejiandikisha sjapata jina langu godfley peter kikoti mkazi ruaha wilaya kilosa tarehe ya kuzariwa 7/6/1997

  1. Nida says:

   Tuma ujumbe kwenda namba 15096 kwa kuandika: jina lako la kwanza*jina lako la mwisho*tarehe mwezi na mwaka wa kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Taarifa Kwa Umma

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu