NIDA YAPONGEZWA KWA KUTOA HUDUMA ZA USAJILI SABASABA

Na. Mwandishi wetu-NIDA

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imepongezwa kwa kushiriki na kutoa huduma za Usajili na Utambuzi wa Watu kwa wananchi wakati wa Maonesho ya Sabasaba.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salumu Ally (MB), kwenye sherehe za kufunga rasmi Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam (DITF) maarufu kama Sabasaba zilizofanyika tarehe 13 Julai, 2020 kwenye ukumbi wa Rashid Mfaume Kawawa, maarufu kama Kobe uliopo ndani ya viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa, Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es salaam.

Balozi Amina aliitaja NIDA na taasisi nyingine zilizokuwa zikitoa huduma kwa wananchi katika maonesho hayo amesema zimetoa huduma nzuri kwa wnanchi waliotembelea maonesho hayo.

Aidha Mhe. Balozi ameipongeza Wizara ya Viwanda na Biashara, TANTRADE, Wafadhili, Kamati za Maandalizi pamoja na washiriki wengine wote kwa kuwezesha na kufanikisha kufanyika kwa Maonesho ya 44 ya DITF licha ya changamoto ya ugonjwa wa COVID 19. Pia amepongeza Kampuni, Taasisi na Mashirika yote yaliyoshinda na kupata tuzo. “Tuzo hizo ziwe ni chachu ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi” Alisema.

Ametoa rai kwa makampuni na taasisi zilizoshiriki kuendelea kuwa wabunifu katika utoaji huduma na uboreshaji bidhaa zao, utoaji wa taarifa sahihi kwa wakati kuhusu bidhaa zao pamoja na utafutaji wa masoko ya uhakika kwa bidhaa ili kuendana na kauli mbiu isemayo “Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu” inayolenga kutanua wigo wa ajira katika sekta mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kukuza Viwanda, shughuli za biashara ili kuinua uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambuisho vya Taifa, Dkt. Arnold Kihaule (wa pili kulia) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Dar Es Salaam (DITF) 2020.
Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Mhe. Amina Salumu Ally (MB) akihutubia wageni waalikwa wakati wa sherehe za kufunga rasmi Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Dar Es Salaam (DITF) 2020. .
Wageni waalikwa wakimsikiliza mgeni rasmi Mhe. Balozi Amina Salumu Ally, Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar alipo wahutubia kwenye sherehe za kufunga rasmi Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Dar Es Salaam (DITF) 2020. .
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Dkt. Arnold Kihaule (wa Pili kulia) pamoja na viongozi wengine wa Taasisi mbalimbali wakiwa wamesimama kumuaga Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ally (hayupo pichani) baada ya kufunga rasmi Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa Dar Es Salaam (DITF) 2020.

Comments on “NIDA YAPONGEZWA KWA KUTOA HUDUMA ZA USAJILI SABASABA”

 1. Nassor Mohamed says:

  Habari, kama jina langu linavyosomeka hapo chini, napenda napenda kupata msaada wa marekebisho ya jina la mwanzo limekosewa lakin nikienda kwenye ofisi za yangu ya wilaya ya NIDA naambiwa siwezi kufanya marekebisho mpaka nipate kitambulisho ambacho sijakipata mpaka sasa tangu mwaka jana na hii inaniaathiri kwa sababu pale napoambatanisha na vyeti vya shule inaonekana kana kwamba ni watu wawili tofauti, naomba msaada wenu.REF: NINI 19881005-15116-00002-24

  1. Nida says:

   Ili marekebisho yafanyike rudi kwenye Ofisi uliyojisajilia kwa ajili ya taratibu za marekebisho hayo, huku hatuna uwezo wa kuona na kufanya marekebisho. Nenda utahudumiwa

 2. John Juma Hamisi says:

  Nilijaza fomu saba saba Dar es Salaam July 8 2020, naombi kama vimesha toka ama namba nijuzwe!
  Ahsante!

  1. Nida says:

   Kufahamu namba yako tuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15096 kwa kuandika:
   jina lako la kwanza*jina lako la mwisho*tarehe mwezi na mwaka wa kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama
   hakikisha huachi nafasi wala kuweka alama yyte kati ya tarehe mwezi na mwaka, pia andika majina kwa usahihi kama yalivyojazwa kwenye fomu yako ya usajili.
   Vitambulisho bado havijatoka

 3. niko mwendampapa amlike says:

  how can i get national id number

  1. Nida says:

   Send SMS to number 15096 by writing:
   your first name*your last name*birthdate (ddmmyyyy)*your mother’s first name*your mother’s last name

 4. Leonard nene says:

  Kitambulisho cha taifa itatoka lini

  1. Nida says:

   Kikichapishwa utajulishwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Taarifa Kwa Umma

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu