MKURUGENZI MKUU AFURAHISHWA NA BANDA LA NIDA SABASABA

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Dr. Arnold Kihaule ameeleza kufurahishwa na namna washiriki wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) katika maonesho ya Kimataifa ya 44 ya Biashara ya Dar es salaam (DITF) wanavyotoa huduma kwa wateja pamoja na muonekano mzuri na mpangilio maridadi wa Banda la Mamlaka katika maonesho hayo.

Dkt Kihaule alibainisha kuridhishwa kwake alipotembelea banda la maonesho la Mamlaka hiyo huko sabasaba Ijumaa tarehe 3 Julai, 2020 ili kujionea namna wananchi wanavyohudumiwa na wafanyakazi wa NIDA.

Akiwa bandani hapo, amewapongeza washiriki wa maonesho hayo kwa kutoa huduma ipasavyo na hivyo kutoa taswira chanya ya Mamlaka kwa wananchi na umma kwa ujumla. Amewasihi wafanayakazi hao kuendelea kutoa huduma nzuri kwa kipindi chote cha maonesho na hata baada ya maonesho hayo kuhitimishwa.

Baada ya kuridhishwa na huduma zitolewazo, yaani Usajili, utoaji wa NIN na uhuishaji wa taarifa za Usajili, amewaagiza Maafisa Usajili wa Wilaya za Dar es salaam hasa Temeke kugawa Vitambulisho ambavyo tayari vimeshachapishwa na kufikishwa ofisini kwao lakini bado havijachukuliwa na wahusika. Sambamba na hilo ameagiza pia itafutwe namna bora ya kuvifuata Vitambulisho vilivyopo kwenye ofisi za Serikali za Mitaa ili navyo vitolewe kwa wahusika katika kipindi hiki cha maonesho.

Dkt. Kihaule alipata pia fursa ya kuwasikiliza wadau wa Ushirikishanaji taarifa za NIDA kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar na kuwaelekeza kwa Kamati inayoshughulikia masuala hayo ili kupata huduma stahiki.

Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dr. Arnold Kihaule akisaini kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye banda la maonesho la NIDA katika viwanja vya sabasaba. Aliyesimama kulia ni Bi. Jamila Chande, Afisa Usajili.
Mkurugenzi Mkuu Dr. Arnold Kihaule akiongea na Afisa TEHAMA wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Ally Edoka Yassin alipotembelea banda la maonesho la NIDA.
Afisa Habari Mwandamizi, Bi. Agnes Gerald (katikati) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA Dr. Arnold Kihaule alipotembelea banda la maonesho la NIDA sabasaba 2020. Wengine katika picha ni Kaimu MKuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bw. Geofrey Tengeneza (kulia kwa DG) na Afisa Usajili Wilaya ya Kigamboni, Samuel Ndaro (wa kwanza kushoto).
Mkurugenzi Mkuu Dr. Arnold Kihaule akitoa maelekezo ya kugawa Vitambulisho vilivyoko kwenye ofisi za Wilaya za Mkoa wa Dar es salaam kwa Mwakilishi wa Meneja Usajili, Bw. Samuel Ndaro- Afisa Usajili Wilaya ya Kigamboni.
Mkurugenzi Mkuu Dr. Arnold Kihaule akiwasikiliza wadau wa ushirikishanaji taarifa za NIDA kutoka Benki ya Watu wa Zanzibar walipotembelea banda la NIDA
huko sabasaba.

Comments on “MKURUGENZI MKUU AFURAHISHWA NA BANDA LA NIDA SABASABA”

 1. Zuberi fuki zuberi says:

  Kwanin msitutumie sms kujua kama kitambulisho kipo tayari kuliko kuongeza msongamano huko sabasaba maana naweza kuja halafu kikawa bado ambapo nakuwa sijafanya kitu

  1. Nida says:

   Kwa kawaida kikiwa tayari unajulishwa kupitia namba ya simu uliyoiandika. kama hujapigiwa wala kutumiwa ujumbe, kitambulisho chako kitakuwa hakijachapishwa bado

 2. Henry J. Sam says:

  I’m waiting for my ID Card from last year 2019.
  Could you please tell me when will it be available.
  However already I’ve ID Number which is 19621102161010000122

  1. Nida says:

   Please contact our call center through numbers available to our home page http://www.nida.go.tz for further followups

 3. Henry J. Sam says:

  Requesting MOBILE phone numbers for NIDA officers at Ubungo Manicipal.
  The office telephone numbers can also be of a great help.

  1. Nida says:

   Samahani hatuna namba zao. Tafadhali fika kwenye ofisi husika kwa mawasiliano zaidi

 4. Bundala Mathias says:

  Namba yangu ya nida Hadi leo sijapata

  1. Nida says:

   Tuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15096 kwa kuandika:
   jina lako la kwanza*jina lako la mwisho*tarehe mwezi na mwaka wa kuzaliwa*jina la kwanza la mama*jina la mwisho la mama
   hakikisha unaandika majina kama ulivyojaza kwenye fomu ya usajili, pia kwenye tarehe mwezi na mwaka hakikisha hauweki nafasi wala alama yoyote

 5. makhafuzi says:

  20000927151060000124

  1. Nida says:

   shida ni nini

 6. makhafuzi says:

  good

 7. rigobert Raphael says:

  Nina swaali naweza uliza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu