Wafanyakazi wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati watembelea Ofisi za NIDA Kinondoni

Afisa Usajili wa NIDA Wilaya ya Kinondoni Bw. Japhet Lagasper (aliyesimama wa pili kutoka kushoto) akielezea kazi zinazofanywa sehemu ya uchukuaji wa alama za kibaolojia (Biometric) kwa Maafisa Habari wa NIDA walipotembelea ofisi hiyo.
Afisa Habari Mkuu wa NIDA Bw. Geofrey Tengeneza (wa pili kushoto) na Afisa Habari Bi. Hadija Maloya wakiangalia namna wananchi wanavyohudumiwa katika sehemu ya uchukuaji wa alama za kibaolojia (Biometric) katika Ofisi ya Usajili ya NIDA Wilaya ya Kinondoni iliyopo Kawe Jijini Dar es Salaam.
Afisa Usajili wa NIDA Wilaya ya Kinondoni Bw. Japhet Lagasper (aliyeshika karatasi kulia) akilelezea hatua za kufuata baada ya kukamilisha ujazaji wa fomu ya Maombi ya Kitambulisho cha Taifa kwa Maafisa Habari wa Kitengo cha Mawasiliano cha NIDA.
Maafisa Habari wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka NIDA, Makao MakuuWakimsikiliza kwa makini Afisa Msajili wa NIDA Wilaya ya Kinondoni Bw. Japhet Lagasper (aliyenyoosha mkono) alipokuwa akitoa maelezo kuhusu kazi zinazofanywa katika sehemu ya kuhakiki na kuingiza taarifa za waombaji kwenye Mfumo wa Usajili (Scanning) kwa Maafisa Habari na Mawasiliano walipotembelea ofisi za NIDA wilaya ya Kinondoni.
Ofisi ya Usajili ya NIDA Wilaya ya Kinondoni iliyopo eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam, karibu na Kituo cha Polisi Kawe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu