TANGAZO: Tembelea banda la NIDA ili ufahamu Namba yako ya Utambulisho wa Taifa (NIN) kwenye Maonesho ya 14 ya Biashara ya Mwanza East Africa Trade Fair

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwajulisha wananchi wote kuwa huduma ya kufahamu Namba ya Utambulisho wa Taifa (NIN) na Usajili na Utambuzi wa Watu inatolewa kwenye banda la NIDA namba 77 katika Maonesho ya 14 ya Biashara ya Mwanza East Africa Trade Fair yanayofanyika Rock City Mall, Mwanza kuanzia tarehe 30 Agosti hadi 08 Septemba, 2019.

Huduma nyingine zinazotolewa ni pamoja na mwombaji aliyekamilisha usajili kupata fursa ya kujulishwa hatua ya maombi yake ya Kitambulisho cha Taifa yalipofikia, elimu juu ya namna ya taratibu za usajili na hatua zake, kupata Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (Electronic ID Copy) kupitia Tovuti ya NIDA (wwww.nida.got.tz), matumizi ya NIN/Kitambulisho cha Taifa pamoja na kukusanya maoni ya wateja wetu ili kupata mrejesho juu ya huduma zetu.

Mawasiliano: Unaweza pia kupiga namba za simu za Huduma kwa Mteja; 0735 201 020, 0736 201 020, 0686 088 888, 0687 088 888, 0777 740 008, 0743 000 058, 0752 000 058, 0677 146 666, 0677 146 667, 0673 333 444, ili kufahamu Namba ya Utambulisho wa Taifa na maendeleo ya hatua ya Usajili ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa yalikofikia na kupata majibu papo hapo popote ulipo.

MUDA: SAA 24, Jumatatu – Ijumaa na Jumamosi saa 01:30 – 07:00 Mchana

‘MFUMO WA UTAMBUZI WA WATU KICHOCHEO CHA KUONGEZA UBUNIFU KWENYE UZALISHAJI NA BIASHARA KATIKA KUKUZA UCHUMI’

Limetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati,

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

30/08/2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu