NIDA Yahitimisha Wiki ya Utumishi Umma kwa Usafi

Na Mwandishi Wetu

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wamehitimisha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye Ufukwe wa Coco, Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati, Thomas Nyakabengwe alisema NIDA imeamua kuhitimisha wiki hiyo kwa kufanya usafi ikiwa ni kuunga juhudi za Serikali za kupambana na mifuko plastiki na ugonjwa wa kipindupindu.

Wafanyakazi hao walifagia, kufyeka na kuzoa taka mbalimbali zilizotupwa kwenye ufukwe huo na kuzikusanya kwenye jalala la kukusanyia taka lililopo karibu na vibanda vya wauza mihogo.

Alisema ingawa jukumu la msingi la NIDA ni usajili na utambuzi wa watu ambalo matokeo yake ni kutoa Vitambulisho vya Taifa lakini ni muhimu kushiriki kwenye shughuli za kijamii na kuwa mfano kwa taasisi nyingine za Serikali na binafsi kutenga muda wa kushiriki kwenye shuguli za kijamii.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, Harrison Lukosi aliwashukuru NIDA kwa kujitolea kufanya usafi katika ufukwe huo ambao upo kwenye Mtaa wake na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano wao wa kujitolea kwenye shughuli za kijamii.

Pamoja na kufanya usafi NIDA imeshiriki kwenye maadhimisho hayo kwa kusajili wananchi katika kanda mbalimbali nchini ili kufanikisha azma ya usajili wa laini za simu kwa kushirikiana na Mamlaka ya  Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu yalikuwa na kaulimbiu “Uhusiano Kati ya Uwezeshaji wa Vijana na Usimamizi wa Masuala ya Uhamiaji, Kujenga Utamaduni wa Utawala Bora, Matumizi ya Tehama na Ubunifu katika Utoaji Wa Huduma Jumuishi”

 Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakifanya usafi katika ufukwe wa Coco, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutoa huduma kwa jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu