NIDA yazindua Baraza la Wafanyakazi

Kamishna wa kazi Bi. Tulia Msemwa azindua baraza la Wafanyakazi NIDA baada ya ililokuwepo muda wake kufikia ukomo lililofanyika katika ukumbi wa polisi – Officer`s Mess Oyster bay.

Bi. Tulia akizindua baraza hilo amewaasa wajumbe kuhakikisha kuwa wanazingatia kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kutumia baraza kama chombo cha kujadili maendeleo ya  taasisi kwa kuwasilisha hoja za ukweli na kuwa wawazi na waaminifu katika kuwasilisha hoja hizo, kuishauri Menejimenti juu ya ya masuala mbalimbali yakiwemo ya kisera,  kiutumishi na ya maslahi ya watumishi, kukosoa, kurekebisa, kufanya tathmini kutoa maoni na kuhakikisha masuala madogo madogo yanamalizika kwenye vikao vya ndani na makubwa kuwasilishwa kwenye vikao vya Baraza la wafanyakazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold M. Kihaule, amewakumbusha watumishi juu ya kufanya kazi kwa uweledi, kwa kuhakikisha hawaruhusu mianya yoyote ya rushwa kuchomoza kwenye kutoa huduma ya Usajili wa wananchi, kuwa wabunifu, na kutumia lugha nzuri pindi wanapo wahudumia wananchi na kwa upande mwingine amewashukuru kwa ushirikiano wanaoutoa katika kutekeleza majukumu ili taasisi isonge mbele.

Aidha kwa upande wake Bw. Litson Msemwa Katibu wa TUGHE, mkoa wa Kinondoni amewapongeza wajumbe wa baraza na uongozi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa chini ya Uongozi wa Mkurugenzi Mkuu Dkt. Arnold M. Kihaule ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza kwa kutekeleza agizo la serikali linaloitaka kila taasisi kuunda baraza la watumishi ambapo watumishi wanakuwa na fursa ya kupata nafasi ya wawakilishi wa kila Idara na Vitengo kuhudhuria na kuwasilisha hoja zao. ‘nimefurahishwa sana na baraza hili kuonekana kuwepo kwa uwazi unaojengewa mazingira na Mwenyekiti  na ukomavu wa wajumbe kwani hoja zote zilizowasilishwa ni zenye kujenga hivyo inaonyesha ukomavu mkubwa walionao’ ameeleza hayo Bw. Msemwa.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dkt. Arnold M. Kihaule akitoa risala wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi la NIDA, ambapo aliwahimiza wajumbe wote kutekeleza majukumu kwa weledi kwa kuhakikisha hawaruhusu mianya yoyote ya rushwa kuchomoza kwenye kutoa huduma ya Usajili  wa wananchi.

 

Kamishna wa kazi ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Tulia Msemwa (katikati) akikata utepe kuashiria kuzindua baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa baada ya kutoa hotuba na nasaa zake juu ya majukumu ambayo kila mjumbe anapaswa kutekeleza.

 

Meza kuu wakiimba wimbo wa kuhamasisha uwajibikaji na umoja kazini kwa lengo la kuchochea ufanisi kazini wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la wafanyakazi cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kilichofanyika katika ukumbi wa polisi – Officer`s Mess, Oyster bay.

 

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa NIDA, wakiimba wimbo wa kuhamasisha uwajibikaji na umoja kazini kwa lengo la kuchochea ufanisi kazini wakati wa kikao cha kwanza cha baraza la wafanyakazi cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kilichofanyika katika ukumbi wa polisi – Officer`s Mess, Oyster bay.

 

Afisa Usajili wilaya ya Nyangwale mkoa wa Geita, Bw. Hashimu Thabiti, akitoa mchago katika kikao cha uzinduzi wa baraza la wafanyakazi wa NIDA, kilichofanyika katikika ukumbi wa polisi – Officer`s Mess Oyster bay.

Leave a Reply to Thurman Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *