Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) yashiriki wiki zima moto na uokoaji Dodoma

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa – NIDA imeendelea kutoa elimu Umma wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Kitaifa, yanayoendelea mkoani Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Katika Maonyesho hayo mbali na elimu ya jumla kuhusu masuala yanayohusu Vitambulisho vya Taifa; Pia Mamlaka imejikita katika kuufahamisha Umma faida za mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu katika masula yanayohusu majanga na uokoaji.

Mbali na elimu hiyo; NIDA inatoa huduma za Usajili na utoaji wa tarifa za hatua ya Usajili kwa wananchi ambao walisajliwa maeneo mbalimbali nchini na hawajafanikiwa kupata Vitambulisho vyao.

Kauli mbiu ya maonyesho hayo kwa mwaka huu inasema “Shiriki kukuza Uchumi wa Viwanda kufunga ving’amua moto kwenye viwanda”.

 

Baadhi ya Maafisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa wakijadiliana jambo wakati maonyesho ya wiki ya zimamoto yanayoendelea mkoani Dodoma. Kutoka kushoto ni Bi. Theresia Charles (Afisa Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta), Bi. Lucina Ramadhani (Afisa Usajili), Bw. Lagasper Japhet (Afisa Miliki) na Bi. Agnes Gerald (Afisa Habari).

 

Afisa Usajili Mkoa wa Dodoma Bw. Khalid Mrisho, akisalimiana na Kamishna msaidizi mwandamizi wa Jeshi la polisi (SACP) Fortunatus Musilim alipotembelea banda la NIDA. Kushoto ni Afisa (NIDA), Bw. Japhet Lagasper.

 

Afisa Usajili wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa Bi. Devotha Ntisi (wa kwanza kulia), akifafanua jambo kwa wananchi waliojitokeza kutembelea Banda na NIDA kwenye  maonyesho ya wiki ya Zimamoto na Uokoaji yanayoendelea jijini Dodoma.

 

Bw. Japhet Lagasper, akifafanua jambo kwa mmoja wa wananchi aliyefika kujifunza faida za Mfumo wa Usajili na Utambuzi wa Watu wakati wa Majanga na Uokoaji katika maonyesho ya wiki ya Zimamoto na Uokoaji Dodoma.

 

Comments on “Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA) yashiriki wiki zima moto na uokoaji Dodoma”

  1. reviews says:

    It’s awesome designed fߋr me to have a web paɡe, wһіch is
    helpful for my knowledge. tһanks admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Fomu za Maombi ya Utambulisho

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu