Halmashauri ya mji wa Babati yajizatiti kukamilisha usajili Vitambulisho vya Taifa

Halmashauri ya Mji wa Babati inaendelea na zoezi la usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea; ambapo wananchi wamehamasika na kujitokeza kwa wingi kusajiliwa.

Akizungumzia zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Babati Ndg. Fortunatus Fwema amesema kiujumla zoezi la Usajili katika Halmashauri yake linaendelea vema isipokuwa changamoto za hapa na pale.

Amezitaja baadhi ya changamoto ni ushiriki hafifu wa wananchi kutokana na msimu wa kilimo asilimia kubwa ya wananchi kuwepo mashambani, mvua na uelewa mdogo wa wananchi katika masuala yanayohusu umuhimu wa Vitambulisho.

Amewataka Wananchi kugawa muda wa kilimo na wa kujiandikisha ili waweze kutumia fursa hii kujisajili na kuagiza watendaji wote walio chini yake kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hili.

 

Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema akielezea umuhimu wa Kitambulisho cha Taifa kwa wananchi ikiwa ni kutambulika na kupata huduma za kijamii kirahisi pamoja na kuwezesha Halmashauri yake kuwa na takwimu sahihi zitakazowasaidia kupanga maendeleo kwa wanannchi wao kwa urahisi alipohojiwa na waandishi wa Radio Manyara.

 

Mwananchi Ally Mohamed (Mwenye Mahitaji Maalum) wa kwanza kulia wa Kata ya Babati ameona umuhimu wa kuwa na Kitambulisho cha Taifa hivyo amejitokeza Kusajiliwa hatua ya pili baada ya kukamilisha kujaza fomu yake aliyoishika mkononi.

 

Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Babati Ndg. Fortunatus Fwema akielezea maendeleo ya zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa na faida zake kwa waandishi kushoto waliofika ofisini kwake kutoka radio Manyara  ambao ni Ndg. John Walter wa kwanza kulia na Ndg. Luka Mondu, kulia ni Afisa Habari Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bi. Agnes Gerald.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu