Wananchi mkoani Simiyu watakiwa kujitokeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa

Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kujitokeza kwa wingi kusajiliwa  Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati zoezi hilo likiendelea kwenye Kata mbalimbali za Mkoa huo.

Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa mkao huo Ndg. Rutaihnwa Albert alipotembelea baadhi ya vituo kukagua maendeleo ya zoezi hilo huku akiwataka Watendaji Kata pamoja na wasimamizi kuweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia wananchi.

Katika zoezi hilo wananchi wamekumbushwa kuhakikisha wanafika kwenye vituo vya Usajili wakiwa na durufu (Photocopy) ya viambatisho muhimu vinavyowatambulisha kuthibitisha Umri, Makazi na Uraia  ambavyo ni:- Cheti cha Kuzaliwa, Pasi ya Kusafiria, Vyeti vya Elimu ya Msingi na Sekondari, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha Bima ya Afya, Nambari ya Mlipa Kodi (TIN) na Kitambulisho cha Mpiga kura.

Aidha wananchi ambao hawana viambatisho vyovyote bado wametakiwa kwenye kweney vituo kusajiliwa kwa utaratibu maalumu uliowekwa na NIDA.

Mbali na Simiyu; Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa linaendelea katika mikoa 15 ya Tanzania likihusisha wadau wote muhimu katika kufanikisha zoezi hilo.

 

Katibu Tawala wilaya ya Bariadi Ndg. Rutaihnwa Albert, Mkoani Simiyu akiwa katika ziara ya kukagua vituo huku akitoa maelekezo kwa Afisa Mchambuzi Mifumo ya Kompyuta Msaididizi Ndg. Bakari Ramadhani.

 

Wananchi mkoani Simiyu wakiwa katika foleni kusubiri kuchukuliwa alama za kibaiolojia baada ya kuwa wamekamilisha kujaza fomu za maombi ya Kitambulisho cha Taifa.

 

Msimamizi wa kituo cha Usajili Diana kilichoko mkoani Simiyu, akihojiwa na mwandishi wa habari juu ya maendeleo ya Usajili wa Vitambulisho vya Taifa kituoni kwake.

 

Mwenyekiti Mtaa wa Ditima akiendelea Kusajili wananchi waliofika kituo cha Usajili wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu ili Kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa.

 

Maafisa Usajili Wasaidizi wa NIDA wakiendelea kukusanya taarifa za wananchi kwa kutumia mashine maalumu za kukutasanya taarifa kwenye mtaa wa mkoani Simiyu.

Afisa Usajili Mkoa wa Simiyu Bi. Careen Kuwite akikagua fomu za maombi ya Vitambulisho vya Taifa za wananchi wa Bariadi waliokamilisha hatua za ujazaji fomu za maombi ya Utambulisho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Fomu za Maombi ya Utambulisho

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu