Wananchi mkoani Simiyu watakiwa kujitokeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa

Wananchi wote wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la uandikishaji Vitambulisho vya taifa (NIDA) linaloendelea mkaoni humo.

Wito huo umetolewa na Afisa Tawala Wilaya ya Bariadi ndg. Rutaihnwa Albert ambaye pia amewataka watendaji wa Kata pamoja na wasimamizi kuweka utaratibu mzuri wa wananchi Kusajiliwa pindi wanapofika kwenye vituo vya Usajili.

Aidha wananchi wametakiwa kufika kwenye vituo vya usajili wakiwa na nakala (photocopy) ya viambatisho vyao muhimu vinavyo hitajika kuwasajili ambavyo ni Cheti cha Kuzaliwa, Pasi ya Kusafiria (Passport), Vyeti vya Elimu ya Msingi na Sekondari, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha Bima ya Afya, Nambari ya Mlipa Kodi (TIN No.) na Kitambulisho cha Mpiga kura pamoja na kuzingatia taratibu za usajili pindi wanapokuwa kwenye vituo.

 

Zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa sasa linaendelea katika mikao 15(kumi na tano ya Tanzania) ambapo kwa mkoa wa Simiyu zoezi  linaendelea kwa Kata za  Senani, Mwamanenge na Ipililo.

Wananchi mkoani Simiyu wakiwa katika foleni kusubiri kuchukuliwa alama za kibaiolojia baada ya kukamilisha zoezi la kujaza fomu za maombi ya Kitambulisho cha Taifa.

 

Mwananchi wa kijiji cha Ditima akiwa katika meza ya Mwenyekiti wa Mtaa akisubiri fomu yake kukaguliwa na kusainiwa ili aweze kwenda kuchukuliwa alama za kibaiolojia zinazojumuisha kupigwa picha, kuweka saini na kuchukuliwa alama za viganja(finger print).

 

Mmoja wa wananchi akijaza fomu ya maombi ya Kitambulisho cha Taifa wakati Mwenyekiti wa mtaa wa Ditima akichambua fomu walizojaza wananchi na kuwapatia ili wakashiriki katika hatua ya pili ya Usajili ikiwa ni kuchukuliwa alama za kibaiolojia.

Comment on “Wananchi mkoani Simiyu watakiwa kujitokeza kusajiliwa Vitambulisho vya Taifa”

  1. Gibitere martin says:

    asantee hii imekuwa hatua muhimu kwetu kama watanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Namba za vitambulisho zilizotengenezwa

Tarehe idadi
10 August 2016 (....)

Ukurasa wetu wa Facebook

Ramani ya Ofisi Zetu